Miamala ya kifedha yenye thamani ya trilioni 13 yafanyika kupitia kampuni za simu

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
TCRA1.jpeg

Kampuni za simu zinazotoa huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita Novemba na Desemba mwaka jana zimekusanya kiasi cha Sh. trilioni 13.07.

Kaimu Meneja wa Habari Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuna ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao hapa nchini.


Amesema kuwa katika miezi miwili iliyopita mwaka jana ambapo Novemba walikusanya Sh.trilioni 6.47 na Desemba Sh.trilioni 6.60 jumla ya makusanyo yote ni sh. Trilioni 13.07 kuptia kampuni za simu zinazohusika na huduma ya miamala.

Alitaja kampuni zilizohusika na maiamala hiyo ni pamoja na Zantel(Easy Pesa),Tigo (Tigo pesa), Vodacom(Mpesa), Aiterl(Airtel Money na Halotel (Halopesa).

Aidha aliwataka wananchi kujihadhari na utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi huku mamlaka na vyombo vya usalama vinashughulikia suala hilo

Chanzo: Mtanzania.
 
Watatuibia sana, kila siku Huduma zao juu, kodi wanalipa wanayotaka wao!!! Wengine hawalipi asilani
 
Tirion 13!? Aisee pesa ndefu hiyo.....Kwa maana hiyo hata TRA wanacheza tu mbele ya TCRA
 
Mkuu mimi nimesikia kwamba hizo ni transactions na siyo makusanyo kama alivyoandika mtoa uzi. Nimeona kwenye TV wakisema kiasi cha Tshs 13 trillion kimekuwa transacted kwenye mifumo ya simu
Nadhani transctions zitakua na athar kweny pato la taifa
 
Those are transactions and not collections! Ni jumla ya fedha ambazo hiyo mitandao imefanya transaction zake.
Acha kupotosha mkuu,yaani kampuni zote za simu zinazofanya biashara hiyo ya fedha zifanye transaction za trillion 13 tu kwa miezi 2!? Mimi peke yangu km wakala kwa siku nafanya miamala ya thamani ya zaidi ya milioni 50 kwa siku. Nadhani kuna kitu hukuelewa..!!
 
Pamoja na ukataa huu wamefanya biashara ya trillion 13 je wakati wa hali nzuri ya biashara ilikuwa trillion ngapi. Kweli serikali ilipoteza pesa nyingi sana. Hongera TCCR na Wizara ya fedha.
 
Acha kupotosha mkuu,yaani kampuni zote za simu zinazofanya biashara hiyo ya fedha zifanye transaction za trillion 13 tu kwa miezi 2!? Mimi peke yangu km wakala kwa siku nafanya miamala ya thamani ya zaidi ya milioni 50 kwa siku. Nadhani kuna kitu hukuelewa..!!
Hahaha wewe ndio Hujaelewa. Cha ajabu naona uvivu kukuelezea
 
Kma wemekusanya trillion 13 kwanini jana Rais bado anaomba msaada wa ujenzi wa reli na thamani yak ni Trillion 20. Mimi siamini kabsa km ni kweli.
 
View attachment 463183
Kampuni za simu zinazotoa
huduma ya fedha kwa njia ya
simu za mkononi katika
kipindi cha miezi miwili
iliyopita Novemba na
Desemba mwaka jana
zimekusanya kiasi cha Sh.
trilioni 13.07.
Kaimu Meneja wa Habari
Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Semu
Mwakyanjala amesema kuna
ongezeko kubwa la
matumizi ya huduma za
kifedha kwa njia ya mtandao
hapa nchini.

Amesema kuwa katika miezi
miwili iliyopita mwaka jana
ambapo Novemba
walikusanya Sh.trilioni 6.47
na Desemba Sh.trilioni 6.60
jumla ya makusanyo yote ni
sh. Trilioni 13.07 kuptia
kampuni za simu
zinazohusika na huduma ya
miamala.

Alitaja kampuni zilizohusika
na maiamala hiyo ni pamoja
na Zantel(Easy Pesa),Tigo
(Tigo pesa), Vodacom
(Mpesa), Aiterl(Airtel Money
na Halotel (Halopesa).
Aidha aliwataka wananchi
kujihadhari na utapeli
unaofanywa kwa kutumia
simu za mkononi huku
mamlaka na vyombo vya
usalama vinashughulikia
suala hilo.

Source; Mtanzania.

Mabank wajifunze kuwa kuwapo kwao mijini tu kunazorotesha uchumi hasa kwakua vijijini wanashindwa kufanya miamala kwa ukosefu wa fedha. Wasilie lie tu kuwa serikali imechukua pesa zake huku wao wakishindwa kuwatengeza wateja wao kwa kuwawezesha.
 
View attachment 463183
Kampuni za simu zinazotoa
huduma ya fedha kwa njia ya
simu za mkononi katika
kipindi cha miezi miwili
iliyopita Novemba na
Desemba mwaka jana
zimekusanya kiasi cha Sh.
trilioni 13.07.
Kaimu Meneja wa Habari
Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Semu
Mwakyanjala amesema kuna
ongezeko kubwa la
matumizi ya huduma za
kifedha kwa njia ya mtandao
hapa nchini.

Amesema kuwa katika miezi
miwili iliyopita mwaka jana
ambapo Novemba
walikusanya Sh.trilioni 6.47
na Desemba Sh.trilioni 6.60
jumla ya makusanyo yote ni
sh. Trilioni 13.07 kuptia
kampuni za simu
zinazohusika na huduma ya
miamala.

Alitaja kampuni zilizohusika
na maiamala hiyo ni pamoja
na Zantel(Easy Pesa),Tigo
(Tigo pesa), Vodacom
(Mpesa), Aiterl(Airtel Money
na Halotel (Halopesa).
Aidha aliwataka wananchi
kujihadhari na utapeli
unaofanywa kwa kutumia
simu za mkononi huku
mamlaka na vyombo vya
usalama vinashughulikia
suala hilo.

Source; Mtanzania.

Kampuni zilikusanya au zilifanya biashara yenye thamani hiyo?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tirion 13!? Aisee pesa ndefu hiyo.....Kwa maana hiyo hata TRA wanacheza tu mbele ya TCRA
TRA wapo mjini pesa wameziacha kule kwa wenye mali...assets, vijijini. Structure na programming ya uchumi wa Tanzania ni mbovu...watu wengi wameachwa nje ya mfumo wa uchumi mkubwa. Walio kwenye mzunguko rasmi ni waajiriwa na wafanya biashara walio sajiliwa...Miamala ya pesa kwa simu ime unganisha watu wengi...Hii inaonyesha kuwa watu wengi hawajaratibiwa kiuchumi...Waziri wa frdha na mipango lazima alione hili...Tanzania siyo masikini kama tunavyo aminishwa...uchumi wa Tanzania umeegemea kwenye cash zaidi huku kukiwa na ukosefu wa miundombinu ya fedha huko rural ambapo kuna informal transactions na pia market structure ina sababisha high transaction costs..
 
Hiyo ni faida inawezekana tu hata ukipiga hesabu ndogo....tu kwa siku 76*2000000=152000000*30=4,560,000,000.....aiseee hyo ni vocha tu tena ya jero kwa ratio ndogo ....JPM ni jembeeeeee mpka 2025
 
Back
Top Bottom