Miaka zaidi ya 10 Baada ya Janga la Kikwete bado Watanzania hatujui tunataka Rais mwenye Sifa zipi!

Huwezi ukatuambia JK alikuwa wa hovyo kuliko Ben ukiwa na mawazo huru kichwani pasipo kuwa na chuki yeyote..

Huwezi ukatuambia Nyerere na Mwinyi walikuwa ni bora halafu ukatuambia JK alikuwa wa hovyo pasipo chuki yeyote..

Tunaposema fulani alikuwa wa hovyo kwenye nafasi fulani bila shaka tunamajibu kuna fulani alitumikia nafasi hiyo kwa ubora wa hali juu.. Toka uhuru Tanzania chini ya CCM haikuwa kupata Rais bora kwa kuangalia vigezo vyenye umuhimu kwenye nafasi ya Urais, Nyerere tunampa tu heshima kama mzee wetu lakini ukweli pasipo unafiki alishindwa kufanya yale ya muhimu kwa maendeleo ya Taifa zaidi ya kujijengea heshima binafsi na ndoto za kuwa Rais wa Africa kwa kufanya yale yenye manufaa ya kisiasa kwake..

Ya awamu ya pili na ya tatu kila mtu timamu anayajua tena afadhali ya huyo Mzee Mwinyi maana alikabidhiwa nchi ikiwa na hali mbaya lakini Ben hapana tusiwe wanafiki JK anastahili credit kubwa sana vs waliomtangulia..

Hivi unafahamu JK alijenga KM nyingi za barabara kuliko Marais wote waliomtangulia ukiunganisha, hivi unafahamu JK aliacha MW nyingi za umeme kuliko waliomtangulia ukiunganisha, idadi ya vyuo vikuu vilivyojengwa, hospitali kubwa za rufaa Benjamini mkapa dom na mloganzila na taasisi ya moyo KWELI UNAMUITA HUYU WA HOVYO..

Mkuu nakuunga mkono. JK is better than Mkapa. Magufuli anendelea kufanya vizuri zaidi. Mungu amsaidie afikie malengo yake.
 
Hapa wala si mambo ya kuhukumu kiongozi baada ya kumaliza muda wake..mambo yote yako wazi kwa nini utathmini baada ya miaka 10 wakati miaka hii 3 tu imefunika miaka 10 ya yule aliyetangulia??? Kwanza habari ya REA aliyebuni kuleta huo mpango ni Mkapa, hizo barabara unazosema hata kama ni nyingi vyovyote vile..kama zinajengwa chini ya kiwango ni sawa na bure..na hilo ndilo linaondoa sifa zote nzr za seikali awamu ya 4, hakuna umakini, wizi na ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe na utegemezi wa kiwango cha juu..huwezi jenga nchi na mentality attitude za hivi..SAHAU! unasema TANESCO kujengewa uwezo kumiliki vyanzo vya kufua nishati..unaelewa unachosema kweli, kipindi waziri wa nishati karamagi anasafiri na mihuri kwenda london kuuza rasilimali na kufunga mikataba ya wizi ndiyo kujengea uwezo TANESCO??? Kilichotokea mambo ya richmond ndiyo kujengea uwezo TANESCO??? madeni yote ya TANESCO uliza yalikuwa makubwa awamu gani??? watu wanatengeneza uhaba wa umeme makusudi ili wauzie serikali umeme, maji yanatumiwa vibaya mtera na kidatu ili watu wauzie serikali umeme...na kiongozi mkuu yupo hana habari kabisa juu ya hujuma km hizi!! Hizo hospitali umetaja ndiyo kipaumbele kuboresha sekta ya afya??? unajenga JKHI wakati wamama wanajifungulia watoto chini sakafuni, kama siyo laana hiyo ni nini?? au wanalazwa mzungu wa nne ndio sawa hivyo?? mwenzake wa sasa vituo vya afya zaidi ya 300 vipya vinajengwa vikiwa na huduma zote za msingi hasa za mama na mtoto, na hayo ndiyo yanahitajika kuinua sekta ya afya nchi kama hii..Hiyo elimu unayosema unajenga UDOM nani atafika UDOM km huku chini kuko ovyo???shule karibu zote za sekondari za serikali zilikuwa hoi bin taabani kimiundo mbinu..majengo yalikuwa yamechakaa, mabweni yanavuja, library zilikuwa zmebaki jina tu..unajenga vyuo unaacha kule wanatokea wafike huko juu??kipaumbele gani cha namna hiyo kama si bora kufanya ili ionekane angalau tumefanya!! sasa hivi ndani ya miaka hii 3 shule zote za sekondari za serikali zimefanyiwa ukarabati mkubwa majengo yamerudi kuwa mapya tena ili watoto wasome kwenye mazingira yanayostahili elimu kutolewa..Lakini mbaya zaidi kujenga tabia ya wizi, uzembe, kutowajibika, ulalamishi na utegemezi..kweli utajenga taifa imara lenye watu wa tabia za hivi..angeendelea kidogo tu nchi ingerudi utumwani tena! si lazima uwe kama ule wa enzi kabla ya uhuru lakini utumwa mamboleo..nchi inaongozwa na kundi dogo la watu wanaoishi ughaibuni! unasifu safari za watu kwenda china unaelewa maana yake?? unageuza nchi yako kuwa BAZAAR COUNTRY halafu unaona umepiga hatua?? huo si ni ujuha..Mwisho..pamoja na safari zote hizo ndani ya miaka 10 unaweza kuonyesha, viwanda au uwekezaji wowote hasa kwenye sekta zinazoajiri watu wengi nchini, kilimo au hata utalii ulifanyika kama zao la safari hizo..ukitaja hata miradi 3 tu, yote niliyoandika nayafuta!!!
Naunga mkono hojaaa....Magufuli ametisha sanaa. Nashukuru Kikwete kuruhusu JPM apite kwenye vikao vya juu vya teuzi za chama CCM na kuwa rais wetu.
 
Kikubwa ninachojifunza hapa ni kwa watanzania kujitafakari unapochaguliwa kuwa kiongozi kuacha legacy ya uongozi bora. Tusipende kugombea uongozi KWA maslahi binafsi bali kwa maslahi ya umma.

Tuwakatae viongozi wa namna hii wanapojitokeza ndani ya vyama vya siasa. Wakati mwengine huwa napata taabu sana nikiangalia vyama vya siasa tulivyonavyo kama vinajitambua au la.

Hivi kwamfano hivi vyama vilivyopo sasa ukiacha CCM mnaona vina viongozi wanaoweza kusimamia rasilimali za taifa letu au ni wachumia TUMBO?
 
Yaani Magufuli awe bora kuliko JK?. Mleta mada mtakuwa unachekesha kwelikweli!
Miradi mingi aiyozindua Magufuli mingi ilishaasisiwa na JK, Sizungumzii planning, nazu gumzia kuwa tayari imeshaanza

1. Daraja la Kigambon
2. Daraja la Kilombero
3. Mtambo wa mawasiliano TCRA
4. Hospitali ya Mloganzila
5.Keshokutwa Magufuli atazindua Terminal3 -JKN airport DSM
6. Mradi wa Maji Ruvu Juu
7. Flyover ya Tazara

Hii miradi yote aliizindua/Ataizindua Magufuli lakini yote hiyo ilishaanza Ujenzi kipindi cha JK na mpaka anaondoka madarakani mwaka 2015 mingi ilikuwa inakaribia kukamilika

Tukija katika Miradi iliyokuwa katka planning
1. SGR Kikwete aliipandia ndege hadi China kunegotiate mradi huo, na wakakubaliana Exim bank itukopeshe
2. Mradi wa kujenga Barabara ya baharini kupitia Coco-beach

Kwenye Elimu Kikwete aliperform vizuri sana
1. Udahili wa Wanafunzi ulionezeka mno, Kupitia kujenga shule za Kata kwa Wingi mno, wanafunzi wengi zaidi walipata mkopo, na vyuo vikuu vingine vilijengwa mfano UDOM, Nelson Mandela etc
2. Barabara zilijengwa kila kona ya nchi, huwezi kusema barabara zilikuwa chini ya kiwango wakati Jemedari wa kusimamia ujenzi wa barabara hizo ni huyu Magufuli na yeye anatake credit kwa kazi hiyo na ndiyo iliyouingiza Ikulu kwa jinsi alivyokuwa akijituma

Kipindi cha Kikwete
1. Matendo ya utekaji watu, upigaji wanasiasa risasi, watu kupotezwa haikuwa kwa kiwango kinachotokea katika utawala wa sasa

2. Kipindi cha JK vyama vya siasa vilipewa haki zao za kufanya siasa tofauti na utawala wa sasa unaominya haki za kisiasa za vyama kwa kuleta hoja zisizo za kisheria eti vikafanye siasa majimboni, wakati sheria inaviruhusu vyama hata kama havina mbunge kufanya siasa nchi nzima

3. Kipindi cha JK hatukuona mambo ya ajabuajabu kama vile kupora korosho za watu, watu kufunguliwa kesi nzito za uhujumu uchumi halafu DPP kujitoa kuwa hana nia ya kuendelea na kesi.

4. JK angalau aliwaweka ndani mawaziri wa BWM kwa ufisadi, watu kama Mramba, Magufuli yeye analalamika kuwa huko nyuma kulikuwa na ufisadi lakini hajamuweka ndani Waziri yeyote wa awamu zilizopita, hii maana yake anapamabana na ufisadi kwa sato wadogo wadogo na si MANYANGUMI ya kisiasa

5. JK aliruhusu bunge liwe na meno, Magufuli kayakwangua bunge limebaki kibogoyo, Kipndi cha JK hata sisi wananchi tuliweza kuona bunge LIVe lakini Magufuli anataka tumuone yeye LIve

Kumlinganisha Magufuli na JK ni sawa na kulinganisha Moto wa Mabua na Moto wa Gesi, JK ni moto wa gesi hauna kelele lakini unaunguza zaidi
 
Ile ishu ya rundo la watu kujitokeza kuanzia ngazi ya chama kwa kila mmoja kuamini anaweza kuongoza nchi, lilinisikitisha sana, tena sana. Hata huo udiwani tu wagombea hawajitokezi rundo namna ile, sembuse urais! Pamoja na kurudisha nidhamu za watumishi wa serikali, anapaswa pia kuhakikisha taasisi ya urais inajengwa katika mtindo ambao mtu akijipima mwenyewe tu anaona hatoshi.
 
Maendeleo ya kwanza kwa binadamu ni uhuru wake, hivyo magufuli haamini kwenye haki za binadamu na uhuru wake hafai kabisa kuwa rais

Magufuli ameongeza umasikini nchini badala ya kuupunguza

Magufuli ameongeza deni la taifa maradufu bila kujua hizo pesa anakopa na kupeleka wapi ikiwa kila miradi mikubwa tunaambiwa ni fedha zetu za ndani

Magufuli hapambani na ukosefu wa ajira nchini

Magufuli anatengeneza nchi ambayo imegawanyika kiitikadi za kisiasa tofauti na kipindi cha Kikwete ambapo hali angalau ilikuwa siyo mbaya kama sasa

Kwa kifupi magufuli ni bomu haswa kuliko Kikwete, huyu hafai hata kuwa mkuu wa familia

Mnaomchukia Kikwete na kumuona magufuli ni bora ni wajinga sana maana hamjui shida ambazo Watanzania wanazipata awamu hii kuliko awamu ya Kikwete

Kikwete alikuwa mbovu sana ila kwa huyu Magufuli ni bora ya Kikwete

Ni sawa na kufananisha jambazi na kibaka ambapo ni bora kibaka kuliko jambazi, maana jambazi yeye hana utu yuko tayari kuua ili mambo yake binafsi yaende

Rais asiye heshimu misingi ya katiba na sharia zake alizoapa kuzilinda na bado unamuona anafaa kuwa rais ni bora ukawahi matibabu ya akili kabla ya hali kuwa mbaya zaidi
Duhh " Umeongea vyema sana mkuu... Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naaam mbaya wa watanzania ni ccm swadakta kabisa " .... nakubaliana na wewe ni ajabu kubwa kabisa kwa watu wa taifa hili kukaa na kujipa matarajio kwamba ccm inaweza ikawapatia viongozi bora watakao livusha taifa kwenye jangwa lenye shida nakuifikisha nchi kaanani
Laiti kama mngejua kuwa tatizo ni #ccm..!!
Mle kila mtu ana choyo.. mle kila mtu anataka kula tena ale kumzidi mwananchi na wengineo wote ndani ya chama..!!
Mle hata akiingia malaika leo.. lazima mabaya yake yatatamalaki..!!
Mle kumeoza...!!
Ukiwemo lazima unuke shombo..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Tusifanye tena majaribio"
Hili neno hili ndio limenivuruga kabisa na yote niliyosoma tangu mwanzo.
Sijui nifuate paragraphs za mwanzo ama za mwisho

Sijui Rais yupi kabezwa na yupi kasifiwa, naona hamna

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
GuDume, ni vigumu sana kupata MTU mwenye sifa za kiongozi mzuri katikati ya ya jamii ya watu wasio na sifa nzuri.
Jamii yetu imekosa watu, INA mijitu.
Jamii inafikiria kuiba na kujilimbikizia Mali, jamii ya watu wavivu wasiotaka kujituma, kutafakari kwa kina na kuwajibika, jamii yenye watu wanaotembea mifukoni na vumbi la Congo badala ya vitabu.
Hili ni taifa la watu wasiojua wanataka nini na hafakirii taifa litakuwa wapi baada ya vizazi vitano vijavyo.
Hahaha jamii inayo tembea na nini mfukoni !!? Dahh haha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi ukatuambia JK alikuwa wa hovyo kuliko Ben ukiwa na mawazo huru kichwani pasipo kuwa na chuki yeyote..

Huwezi ukatuambia Nyerere na Mwinyi walikuwa ni bora halafu ukatuambia JK alikuwa wa hovyo pasipo chuki yeyote..

Tunaposema fulani alikuwa wa hovyo kwenye nafasi fulani bila shaka tunamajibu kuna fulani alitumikia nafasi hiyo kwa ubora wa hali juu.. Toka uhuru Tanzania chini ya CCM haikuwa kupata Rais bora kwa kuangalia vigezo vyenye umuhimu kwenye nafasi ya Urais, Nyerere tunampa tu heshima kama mzee wetu lakini ukweli pasipo unafiki alishindwa kufanya yale ya muhimu kwa maendeleo ya Taifa zaidi ya kujijengea heshima binafsi na ndoto za kuwa Rais wa Africa kwa kufanya yale yenye manufaa ya kisiasa kwake..

Ya awamu ya pili na ya tatu kila mtu timamu anayajua tena afadhali ya huyo Mzee Mwinyi maana alikabidhiwa nchi ikiwa na hali mbaya lakini Ben hapana tusiwe wanafiki JK anastahili credit kubwa sana vs waliomtangulia..

Hivi unafahamu JK alijenga KM nyingi za barabara kuliko Marais wote waliomtangulia ukiunganisha, hivi unafahamu JK aliacha MW nyingi za umeme kuliko waliomtangulia ukiunganisha, idadi ya vyuo vikuu vilivyojengwa, hospitali kubwa za rufaa Benjamini mkapa dom na mloganzila na taasisi ya moyo KWELI UNAMUITA HUYU WA HOVYO..

Hapo pa Nyerere kutaka kuwa Rais wa Afrika......Kama huyu mzee asingeingilia na kuvuruga mipango ya Kwame Nkurumah ya kutaka kuiunganisha Afrika kwa mara moja ungekuta sasa tuna United States of Africa
 
Mkuu rwamuli;

Nadhani Ben hakufanya makosa wakati anamaliza mda wake, bali makosa yalifanyika 1995 wakati Ben anateuliwa kugombea. Naskia mwaka huo (1995) JK alimzidi Ben kura za maoni, Ila kwa sababu ya umri, Ben akateuliwa kushika kijiti kwa makubaliano kuwa 2005 wakati Ben anamaliza mda wake, JK atagombea. Na ndivyo ilivyokuwa.
Kama ni makosa nadhani yalianzia huko, kumpa JK ahadi ya urais 10 miaka 10 kabla was a mistake.
Mleta mada umetembelea kwenye chaki vizuri sana, makosa yalianza kwenye mchakato wa urais kweny kipind cha Mkapa wakt anamaliza muda wake. Laiti kile kijiti angepatiwa Dr. Salim Ahmed Salim hakika tusingekuwa na uozo huu tulionao. Mimi namlaumu Ben na Hendisamu kwa haya yote waliyotuachia wameyataka wao
Japo Jpm kidogo huwez mlinganisha na aliyepita.
 
Back
Top Bottom