Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Baada ya kusikia CV ya Saed Kubenea nikapigwa na butwaa kwamba jamaa kumbe hata darasa la saba hakumaliza vizuri na shule ya sekondari aliyosomea haijui na wala hakumbuki jina lake, sasa nikajiuliza nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa Gazeti la Mwanahalisi enzi hizo kabla ya kufungiwa na ndiyo niliamini kabisa kwamba kilikuwa chanzo cha habari ambazo ni nadra sana kuzipata kupitia vyombo vingine vya Habari na kusema ukweli niliamini karibia kila nilichokisoma kwenye hilo gazeti, leo nimekuja kugundua Mwandishi wa hili Gazeti hili Saed Kubenea hata shule hakumaliza, na alikuwa anatulisha habari za Uongo! Nimestaajabu sana, kumbe siku zote tumekuwa tukielimishwa na failure kweli nchi yetu ni zaidi ya uijuavyo!
Niliilaumu Serikali walipolifungia hili Gazeti, sasa leo hii nimeamini kwamba Serikali walikuwa sahihi kabisa na kuanzia leo nitaamini maamuzi ya Serikali kwani nimetambua kwamba huwa hawafanyi jambo bila ya sababu ni swala la muda tu na ukweli hujitenga!