Miaka nenda rudi ya madeni, hakuna Ulaya au Amerika walipotaifisha mali

Umenena kuna siku ndugai kapokelewa china na msafara plus watoto wazuri wa kichina yaani mapokezi ya vip, nadhani ajenda nyuma yake awatetee Bandari ya bagamoyo ipite, wachina wanajua Sana kuwamangungo watawala wa kiafrica yaani wanashangazwa wakienda china kusaini mikataba.
Wachina katika suala la hela wapo tayari kufanya chochote. Kama kuna manunuzi unataka kufanya, manunuzi makubwa labda tuseme kuanzi dola laki 5, hata ungemtaka mkewe au binti yake, anakupa. Kwenye pesa, mchina, utu anaweka pembeni.
 
Miaka ya katibuni, baadhi ya watanzania na waafrika kwa ujumla, wameweehukia mikopo ya kutoka Chima. Tna wengine kufikia kuwadharau wahisani na wakopeshaji wetu wa asili ambao ni mataifa ya Ulaya na America.

Kwa ujinga tu, wengine wakafikia kuwaita hawa watoaji misaada na wakopeshaji wetu wa asili, yaani nchi za Ulaya na America, kuwa ni mabeberu wanaopora rasilimali za Afrika, na huku wakiongezea kuwa wamempata rafiki mpya, mwenye mapenzi mema na Afrika, Mchina.

Pamoja na Afrika kuelemewa na madeni makubwa toka nchi za Ulaya na America, haikuwahi kutokea wakopeshaji hao kuchukua vitega uchumi vya nchi mdaiwa, kama viwanja vya ndege au bandari, hata mara moja, kama anavyofanya Mchina.

Nadhani,memesikia, Airport ya Uganda imechukuliwa na wachina kwa sababu Uganda imeshindwa kulipa deni kwa wakati. Bandari ya Mombasa inanyemelewa kwa sababu hizo hizo. Airport na Shirika la umeme Zambia, vipo mbioni kuchukuliwa. Bandari ya Gambia imechukuliwa kwa sababu hizo hizo.

Hivi China, inapochukua vyanzo hivyo vikubwa vya mapato vya mataifa haya maskini, huo ndio upendo wao kwa Afrika au ni mbinu ya kuididimiza Afrika?

China inanufaika sana kutoka Afrika kuliko nchi za Afrika zinavyonufaishwa na China. Afrika limekuwa ndiyo soko kubwa la bidhaa zake duni na zisizo na ubora. Haijaridhika na hayo yote, sasa wanataka kuja moja kwa moja na kubeba hata kile kidogo ambacho nchi za Afrika inacho.

Kwangu mimi, China inaitumbukiza kwenye umaskini mkubwa Afrika kwa bidhaa zake duni. Waafrika kwa sababu ya umaskini, wanalazimika kununua bidha hizi duni za China ambazo ni aghali sana. Nasema ni aghali sana, kwa sababu, ukinunua kiatu toka China cha shilingi laki 1 kinadumu miezi 6, ukinunua kiatu toka Italy sh laki 2, kinadumu miaka 6, kipi ni aghali zaidi? Kiatu cha China kinachodumu miezi sita ni sawa unatumia sh 100,000÷6 kwa mwezi. Ina maana kila mwezi imekugharimu zaidi ya sh 16,000. Cha Italy, kilichodumu miaka 6 (miezi 72) ina maana kila mwezi imekugharimu 200,000÷72, sawa na sh 2,777. Na hiyo ipo kwenye magari, jenereta za umeme, na kila aina ya machine.

Bidhaa za China ni bei nafuu wakati unanunua, ukienda kwenye matumizi, bidhaa za China ni aghali sana.

Kama una kiwanda au shughuli yako inayotumia mashine mbalimbali, na unataka kufanya shughuli zako kwa uhakika, ziepuke sana bidhaa za China. Utafilisika, huku wachina wakitajirika bila ya kukuonea huruma.

Ukoloni wa Mchina utakuwa mbaya zaidi kuzidi hata biashara ya utumwa iliyofanywa na mwarabu. Mataifa ya Afrika yajihadhari sana Mchina. China inaiona Afrika kama ndilo bara litakaloifanya ibadilishe maisha ya wananchi wake, ambao wengi wapo kwenye umaskini mkubwa.
Aya yako ya pili kutoka mwisho nakupinga, hivi kama sio mchina kuleta pikipiki hizi bodaboda hali ingekuaje. Mchina ana madhila yake ila mazuri yake ni mengi zaidi kwa afrika
 
Hizi bodabado kuna pande 2. Moja ni kwenye upande wa faida, na nyingine ni hasara.

1) Kwenye faida ni kwamba hizi boda boda watu wengi wana uwezo wa kúzinunua

2) Kwenye hasara, ni kwamba hazina ubora. Nyingi zinakufa ndani ya miaka 2. Unalazimika kufanya matengenezo wakati wote. Pikipiki kama ya mjapani, Honda, inaitwa roho ya paka, sijui kama huwa inakufa, kama inakufa ni baada ya miaka mingapi. Utanunua kwa bei kubwa lakini utaitumia kwa miaka mingi, bila kuhitajika kufanya matengenezo ya mara kwa mara. Aliyenunua pikipiki ya mchina, atanunua hata 6, wewe bado una ile ile moja.
 
Hao wa ulaya wanatuibia kwa njia nyingine, wao wanacontrol masoko ya rasilimali zetu kama vile madini etc.

Halafu kama Mchina anachukua asset hilo ni kosa ls viongozi wa Afrika, walikuwa wapi wakati wanaingiza vipengele hivyo kwenye mikataba?

Mchina hakulazimishi kuchukua mkopo kwake ni njaa yako tu
 
Ni kweli, ni bora Samia aendelee kujibanza kwa haya mabeberu, tunajuana nayo muda mrefu, kuna madeni wanatudai ya miaka ya 1970's huko ila bado wanatupa hela na kutukopesha pia, Mengine huwa wanayasamehe juu kwa juu! Mabeberu wanachotaka wao nchi yako iwe na demokrasia, haki za binadamu, kufuata sheria (Which sioni kama ni masharti magumu sana kwa jamii inayojitambua)!! Watu primitives wanaotaka kukandamiza binadamu wenzao ndiyo huwachukia mabeberu. Mfano, Korea Kaskazini kuna mtu kahukumiwa kifo sababu ni kusmuggle series ya squid game kutoka Korea Kusini (Ni ukatili uliopitiliza).
Ile bandar ya Bwagamoyo,mbona tunasikia yeye ndiye anapewa,hivi tutapona kweli? Sasa naamini mtanikumbuka.Nawashauri waganda wawavamie kwa bunduki,marungu,mapanga waachie mali za Waganda.au tufuate nyayo za nduli.Nchi yetu,kiwanja chetu eti aje Mchina akichukue? Si patawaka moto,Ina maana hata jeshi la kuchukua hiyo nchi hakuna,ndege za Uganda zitatua kwenye kiwanja cha China Airport Kampala.Baadaye Hii ya hapa itaitwa China Bwagamoyo Habours Tanzania.
Mungu tusaidie.
 
Miaka ya katibuni, baadhi ya watanzania na waafrika kwa ujumla, wameweehukia mikopo ya kutoka Chima. Tna wengine kufikia kuwadharau wahisani na wakopeshaji wetu wa asili ambao ni mataifa ya Ulaya na America.

Kwa ujinga tu, wengine wakafikia kuwaita hawa watoaji misaada na wakopeshaji wetu wa asili, yaani nchi za Ulaya na America, kuwa ni mabeberu wanaopora rasilimali za Afrika, na huku wakiongezea kuwa wamempata rafiki mpya, mwenye mapenzi mema na Afrika, Mchina.

Pamoja na Afrika kuelemewa na madeni makubwa toka nchi za Ulaya na America, haikuwahi kutokea wakopeshaji hao kuchukua vitega uchumi vya nchi mdaiwa, kama viwanja vya ndege au bandari, hata mara moja, kama anavyofanya Mchina.

Nadhani,memesikia, Airport ya Uganda imechukuliwa na wachina kwa sababu Uganda imeshindwa kulipa deni kwa wakati. Bandari ya Mombasa inanyemelewa kwa sababu hizo hizo. Airport na Shirika la umeme Zambia, vipo mbioni kuchukuliwa. Bandari ya Gambia imechukuliwa kwa sababu hizo hizo.

Hivi China, inapochukua vyanzo hivyo vikubwa vya mapato vya mataifa haya maskini, huo ndio upendo wao kwa Afrika au ni mbinu ya kuididimiza Afrika?

China inanufaika sana kutoka Afrika kuliko nchi za Afrika zinavyonufaishwa na China. Afrika limekuwa ndiyo soko kubwa la bidhaa zake duni na zisizo na ubora. Haijaridhika na hayo yote, sasa wanataka kuja moja kwa moja na kubeba hata kile kidogo ambacho nchi za Afrika inacho.

Kwangu mimi, China inaitumbukiza kwenye umaskini mkubwa Afrika kwa bidhaa zake duni. Waafrika kwa sababu ya umaskini, wanalazimika kununua bidha hizi duni za China ambazo ni aghali sana. Nasema ni aghali sana, kwa sababu, ukinunua kiatu toka China cha shilingi laki 1 kinadumu miezi 6, ukinunua kiatu toka Italy sh laki 2, kinadumu miaka 6, kipi ni aghali zaidi? Kiatu cha China kinachodumu miezi sita ni sawa unatumia sh 100,000÷6 kwa mwezi. Ina maana kila mwezi imekugharimu zaidi ya sh 16,000. Cha Italy, kilichodumu miaka 6 (miezi 72) ina maana kila mwezi imekugharimu 200,000÷72, sawa na sh 2,777. Na hiyo ipo kwenye magari, jenereta za umeme, na kila aina ya machine.

Bidhaa za China ni bei nafuu wakati unanunua, ukienda kwenye matumizi, bidhaa za China ni aghali sana.

Kama una kiwanda au shughuli yako inayotumia mashine mbalimbali, na unataka kufanya shughuli zako kwa uhakika, ziepuke sana bidhaa za China. Utafilisika, huku wachina wakitajirika bila ya kukuonea huruma.

Ukoloni wa Mchina utakuwa mbaya zaidi kuzidi hata biashara ya utumwa iliyofanywa na mwarabu. Mataifa ya Afrika yajihadhari sana Mchina. China inaiona Afrika kama ndilo bara litakaloifanya ibadilishe maisha ya wananchi wake, ambao wengi wapo kwenye umaskini mkubwa.
Jiwe alipoona mikopo ua china haingiliwi maswala ya utawala bora na demokrasia akakimbilia huko akidai ni marafiki wa muda mrefu.

Bagamoyo Port tu ilimtoa baru😅😅😅
 
Ile bandar ya Bwagamoyo,mbona tunasikia yeye ndiye anapewa,hivi tutapona kweli? Sasa naamini mtanikumbuka.Nawashauri waganda wawavamie kwa bunduki,marungu,mapanga waachie mali za Waganda.au tufuate nyayo za nduli.Nchi yetu,kiwanja chetu eti aje Mchina akichukue? Si patawaka moto,Ina maana hata jeshi la kuchukua hiyo nchi hakuna,ndege za Uganda zitatua kwenye kiwanja cha China Airport Kampala.Baadaye Hii ya hapa itaitwa China Bwagamoyo Habours Tanzania.
Mungu tusaidie.
CCM na mikataba ya siri. Chifu mangungo treaty
 
Sio lazima kwa WaAfrica kukopa.....mfano kwa sasa Tanzania ilipaswa kutumia resources zake kujiletea maendeleo..na kuachana na hii mikopo ya kijinga kijinga, ....

Hakuna mwema kwa mwafrica, lamsingi ni mwafrica atumie maarifa na akili zake mwenyewe kujiletea maendeleo yake mwenyewe akiachana na urafiki wa kipumbavu na wapumbavu..
Wasipokopa watapata wapi pesa za kushinda angani kwenye ndege kuzulula huku na kule??
 
Kwa mchina sidhani kama kuna mtza anamkamata hata milioni moja kwa mwezi mshahara,hovyo Sana hawa watu
Nashangaa baadhi ya watu wa hovyo wanaifagilia china. Ni vile tu wanajali matumbo yao. China ni mtu wa kutujenhea barabara tu na kumwacha aende zake. Hawana utu wale.
 
K
Wakorea kaskazini hawana tofauti na waafrika wote wanahitaji ukombozi.Kim kaibaka korea kama kampuni yake binafsi anaishi kifalme huku watu wake dhoofu hali kabisa.
Kuna wapuuzi hawana exposure au kwa maslahi ya matumbo yao wanatetea upuuzi wa Jon Kim
 
Ni kweli, ni bora Samia aendelee kujibanza kwa haya mabeberu, tunajuana nayo muda mrefu, kuna madeni wanatudai ya miaka ya 1970's huko ila bado wanatupa hela na kutukopesha pia, Mengine huwa wanayasamehe juu kwa juu! Mabeberu wanachotaka wao nchi yako iwe na demokrasia, haki za binadamu, kufuata sheria (Which sioni kama ni masharti magumu sana kwa jamii inayojitambua)!! Watu primitives wanaotaka kukandamiza binadamu wenzao ndiyo huwachukia mabeberu. Mfano, Korea Kaskazini kuna mtu kahukumiwa kifo sababu ni kusmuggle series ya squid game kutoka Korea Kusini (Ni ukatili uliopitiliza).
Pesa zenyewe mseveni alikuwa anakopa anafanyia uchaguzi wa kupora wapinzani magari ya washa washa wakati waganda hata maji ni tatizo kubwa.
 
Nimestuka miez iliuopita nimenunua tv imekaa wiki mbil display ikatoa mwanga mweupe kuashiria imeungua nikavuta nyingine mwendo huo huo nikasema labda vyanzo vyangu vya umeme vinapower kubwa nikavuta nyingine kilichofuata nikaenda mkoromea muuzaji ndipo akanichana ukweli sasa najiuliza hivi hiyi tbs kazi yake nini mbona tunapigwa wao wanakenua meno hivi hawaoni haya

|√uma |_ao
View attachment 2024221
Pole sana Mkuu. ile tasisi imejaza watu wa chama tu. Usitegemee efficiency ya maamna.
 
Waafrica mnalia lia sana, tengenezeni vya kwenu na mkopeshane wenyewe acheni kutegemea wengine, kwani wao nani aliwasaidia, na hakuna pesa ya bure acheni ujinga na hamlazimishwi kuchukua hiyo mikopo,na hata hiyo mikopo tukipewa inaishia kwa mafisadi tuu bora watukomeshe ili tuiache, mmejaza ardhi nzuri na mabonde yaliyojaa maji lakini mpaka leo bado tunaagiza mchele na sukari, tujilaumu wenyewe na tubadilike
60yrs of independence under CCM
 
M
Wachina ni majambazi wakubwa, Kwanza wenyewe huko kwao kuna wananchi ni maskini nafuu hata ya TZ, wanaidanganya dunia kwa maujenzi ya mavitu makubwa makubwa kwenye majiji wakati wananchi wao vijijini hata vyoo hawana, wananyea kwenye ndoo na kumwaga kinyesi porini! Leo hii China kuna watu bado wanaosha nguo zao kwenye streams za maji machafu! Jiwe angeendelea angetapeliwa na hawa watu, maana alikuwa anawahusudu sana! Wazungu wana madhaifu yao, ila siyo watu wa shortcuts na uongo uongo
Mzungu ukikopa pesa zake ueleze kwa uwazi unaemda kufanyia nini na uoneshe hicho kitu ulichofanyia a-to-z. Viongozi wa afrika hawapendi uwazi, uadilifu wala ushirikishwaji. Ndio maana wanachukia mikopo ya wazungu wanakimbilia ya China.
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom