Miaka miwili ya Rais Samia Arusha inapiga hatua kubwa kubwa sekta ya afya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,980
Katika miaka miwili ya uongozi wa Rasis Samia Suluhu Hassan mengi yamefanyika katika mkoa wa Arusa lakini nimefurahishwa na yaliyofanyika katika sekta ya afya. Kwa uchache mambo hayo ni pamoja na:

Katika sekta ya afya, Mkoa wa Arusha umeongeza vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 383 kutoka mwaka 2020/21 hadi kufikia vituo 421 mwaka 2022/23 ikiwa ni ongezeko la vituo 38 sawa na asilimia 10, hali ambayo imewapunguzia wananchi hasa wa maeneo ya vijijini kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za matibabu, serikali imejenga jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika hosptali ya rufaa ya mkoa ya Mount Meru pamoja na kutoa huduma za CT-SCAN ambazo awali hazikuwepo.

"Pia katika hospitali ya wilaya ya Longido limejengwa jengo la wagonjwa mahututi (ICU), pia tumefanikiwa kujenga na kukarabati vituo vya afya 25, zahanati 45 na nyumba za watumishi 26 ndani.

Kutokana na huduma kusogezwa karibu na wananchi Idadi ya vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka wastani wa vifo 100/100,000 kwa mwaka 2020/21 hadi kufikia wastani wa vifo 89/100,000 kwa mwaka 2022/23.​
 
Kutokana na huduma kusogezwa karibu na wananchi Idadi ya vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka wastani wa vifo 100/100,000 kwa mwaka 2020/21 hadi kufikia wastani wa vifo 89/100,000 kwa mwaka 2022/23.
Impact bado ndogo, tuendelee kupambania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom