Tupac kwenye hit em up alisema F...k Mac J, F...k Big and all bad boy staffs f..k you too and if you wana go to badboy lab. F...k you too. And all staffs in ccm and all wana join it F...k you too
 
Wakuu, kuelekea mheshimiwa rais Magufuli kutimiza miaka miwili tangu alipoapishwa na kuingia madarakani Novemba 5 2015, ni vema sisi kama great thinkers tusiishie kuongea tu pasi na mashiko
kupitia uzi huu, yujiachie sasa kwa kuonesha mafanikio na kufeli kwa awamu hii ya tano kwa muda wa miaka miwili
kwa upande wangu, kiujumla rais kafanikiwa na spidi aliyonayo inarizisha japo mapungufu yapo pia

Mafanikio ya haraka tu ni, mapambano dhidi ya watumishi hewa na vyeti feki,
ujenzi wa reli standard gauge, ujenzi wa fly over, kuthibiti safari za nje na matumizi yasiyoya lazima, ajira kwa vijana japo si kwa wingi, ujenzi na ufunguzi wa viwanda kila kona ya nchi, vita ya kulinda maliasili kama madini nk

Mapungufu
Bomoabomoa, uminywaji wa demokrasia, matukio ya kinyama kifanywa hadharani kama kupigwa risasi na utekaji, uhuru wa bunge na bunge live hakuna nk


Kwa hakika tukiungana kwa pamoja, rais atatuvusha watanzania kuelekea uchumi wa kati na tanzania ya viwanda.
 
one of the biggest failure ambayo inanikera sana ni KUWAGAWA WATZ.

hayo ya uchumj na mengine ni changamoto tu na pengine ni matokeo ya kuwagawa wananchi,

uchumi anaweza kuustablelize lkn hili la kupandikiza chuki, ubinafsi na udouble standard aisee sio mzuri kabisa,

Namuombea kwa hili maana najua madhara ya chuki.
Mungu ampe hekima mh. Raisi ktk hili.

awe baba wa waTz wotee...
 
Mafanikio labda yale maduka ya MSD community yamesaidia sana mana pale nje Muhimbili wale maboya wa maduka ya phamarcy kuna dawa wanauza 12,500 ila maduka ya Msd ni 2,500 tu hapo nampongeza.
..........OTHERWISE
he is such a total failure kwa kila sekta...afu anaropoka na kukurupuka hana busara za uongozi....hana leadership skills...ubabe ubabe mwingi afu much know ....hana exposure ya mambo mbalimbali... yani ana ule shamba wa kizamani afu anajiona bonge la mjanja...kumbe bonge la Juma KILAZA.

Inshort, You can take him out of CHATO but you can't take CHATO out of him!
Ni mtazamo tu...moderator wasijetokwa na mapovu maana wanamuabudu siku izi ukimkosoa tu mode anakuBan!
 
URL]
 
Ubaguzi...anabagua wananchi wake wazi wazi kabisa....mfano nyie wa mwanza mlinichagua sitawabomolea....wale wa tetemeko kawaambia sikuleta tetemeko hivyo siwapi msaada....
 
He is result oriented person, analeta matokeo chanya kwenye maeneo ya msingi kama vile: elimu, miundo mbinu, afya, na kurudisha nidhamu ya uwajibikaji. Haya mambo mimi nampongeza sana Raisi wangu. Matatizo yapo kwenye demokrasia, uhuru wa watu kutoa maoni yao na uhuru wa vyombo vya habari haya mambo yamemshinda. Uvumilivu wa kisiasa na diplomasia hivi vitu vimemshinda kabisa, unapokua kiongozi lazima ukubali kukosolewa na uwaache watu wakosoe na pia uwe na uwezo wa kutatua migogoro bila ya kutumia msuli.
 
Kagera-sikuomba tetemeko
Mwanza-human face
Dar-bomoa
Mwanaccm akihama-majizi yanakimbia
Mpinzani akihamia ccm-anaunga mkono kazi nzuri
Vyeti hewa-wafukuzwe kasoro bashite anakamata madawa

My take.
Siasa za chuki, ukanda/ukabila nk zinapaka tope juhudi zote anazofanya
 
Wakuu, kuelekea mheshimiwa rais Magufuli kutimiza miaka miwili tangu alipoapishwa na kuingia madarakani Novemba 5 2015, ni vema sisi kama great thinkers tusiishie kuongea tu pasi na mashiko
kupitia uzi huu, yujiachie sasa kwa kuonesha mafanikio na kufeli kwa awamu hii ya tano kwa muda wa miaka miwili
kwa upande wangu, kiujumla rais kafanikiwa na spidi aliyonayo inarizisha japo mapungufu yapo pia

Mafanikio ya haraka tu ni, mapambano dhidi ya watumishi hewa na vyeti feki,
ujenzi wa reli standard gauge, ujenzi wa fly over, kuthibiti safari za nje na matumizi yasiyoya lazima, ajira kwa vijana japo si kwa wingi, ujenzi na ufunguzi wa viwanda kila kona ya nchi, vita ya kulinda maliasili kama madini nk

Mapungufu
Bomoabomoa, uminywaji wa demokrasia, matukio ya kinyama kifanywa hadharani kama kupigwa risasi na utekaji, uhuru wa bunge na bunge live hakuna nk


Kwa hakika tukiungana kwa pamoja, rais atatuvusha watanzania kuelekea uchumi wa kati na tanzania ya viwanda.

Mafanikio:
  1. Karudisha nidhamu iliyopotea muda mrefu Serikalini
  2. Kajitahidi kuuimarisha Uchumi wa Tanzania na Pesa kidogo kuwa na thamani
  3. Kaonyesha kwamba ni Kinara mzuri wa Kupambana na rushwa / ufisadi nchini
  4. Kaonyesha Ujasiri kuwa hayumbishwi na hatetereki kitu ambacho ni muhimu kwa Rais yoyote yule
  5. Kaonyesha kuwa ni msema kweli na kile akisemacho huwa anakimaanisha
  6. Kaonyesha kuwa ni Jemedari wa ukweli katika kuzipigania na kuzilinda Rasilimali za Tanzania
  7. Kaonyesha kuwa si Mnafiki na hapendi kuchezewa hovyo hasa katika Utendaji
Mapungufu:
  1. Mwoga wa Kisiasa
  2. Vimelea vya Ukabila bado havijamtoka
  3. Anapenda kusikiliza uwongo na kuuchukia ukweli
  4. Hana Diplomasia hasa katika utendaji na maamuzi yake ya kila siku
  5. Amepishana na ile Kauli ya Mungu isemayo Mpende Adui yako ambapo Yeye anawachukia Maadui zake
  6. Anapenda mno kusifiwa kitu ambacho Kiuongozi si kizuri kwani hata Shutuma nazo humjenga zaidi Mtu
  7. Ana hasira sana ila hana umakini wakati hivi viwili vinatakiwa viende sambamba
Ni hayo tu Mkuu.
 
Hizi hutuba tushakariri inatosha kila siku marudio tu Yale Yale kama.mwimbo wa taifa.
 
Cherehani 4 kuwa kiwanda ni hatua Kubwa sana katika uchumi hajapata kutokea Cherehani kupewa hadhi iliyokosa miaka nenda rudi
 
Ni vema kwanza tukaanza kuwakumbusha watanzania kuwa Wakoloni wakileta maendeleo Makubwa sana from ziro ground.
Yaani waafrika kabla ya ukoloni wakikua hawana mifumo rasmi ya kisiasa na kiuchumi.
Wakikua na teknolojia duni sana.

Hawakua na hiki leo tunachokiita miundo mbinu kama mabarabara,viwanja vya ndege, bandari na reli.

Waafrka kabla ya ukoloni Hawakua na ajira rasmi n.k.

Mambo mengi leo tunayoyaita maendeleo yaliletwa na mkoloni.

Mkoloni alitumia nguvu kubwa kufanikisha hayo mandeleo kutokana na watu waliokuwepo wakati huo kutokua na elimu ,kutoelewana kwenye lugha ya mawasiliano ,ubaguzi wa rangi kwa kuona kuwa mwafrika ni mjinga sana asiye na thamani sawa na mzungu.
Pia waafrika walikua hawajawahi kuona sehemu yoyote vitu kama treni ,viwanda n.k ili wahamasike kwa kujua umuhimu wake.

Waafrika walipita katika wakati huo mgumu sana kwenye historia ya maisha yao kutokana na uloloni na maendeleo yao.
Kws kiwango kikubwa walionufaika zaidi na maendeleo ni wakoloni, viongozi wa dini na waafrika waliobahatika kupata elimu.

Tuanze kwa kuwaelimisha watu kuwa ni kwa nini waafrika waliletewa maendeleo makubwa na wakoloni lakini bado walipigania uhuru.
Je, ni uhuru gani waliokuwa wanaupigania kama maendeleo yalikua yameletwa kwa kiwango kikuba.
Nidhamu kazini wakati wa mkoloni ilikua kubwa, hapakuwa na watumishi hewa n.k.

Bila shaka waafrika walimaanisha uhuru wa kujitawala na kuwa sehemu ya uongozi .
Wafrika walipigania haki sawa kwa wote.
Walipigania usawa na heshma kwa wote.
Walipigania uhuru wa kisiasa.
Walichukizwa na utawala wa mabavu n.k.


Leo miaka 57 tangu babu setu walipokataa kubadharauliwa ,kudhaliloshwa , kubaguliwa, kunyimwa haki ya kisiasa na kujieleza hata hivyo tunataka tena kurudi huko tena tunarudishwa na baadhi ya waafrika wenzetu waliopata uongozi kidemakrasia.
Hakuna jipya chini ya mbingu lakini uongozi unaorharau uhai wa mtu mmoja asiye na hatia ni hatari sana.
Uhai umetolewa mara moja tu na hauna mbadala. Maendeleo ya vitu yalianzishwa na mkoloni na yamepiga hatua kubwa sana japo kwenye macho ya wanasiasa yanatafsiriwa tofauti kama mbinu za kujipatia umaarufu.

Ni miaka michace tu iliyopita tumeshasahauliswa maendeleo makubwa na miradi ya mabilioni iliyofanywa na serikali ya awamu ya nne. Tumekubali kubeza kila kitu kilichofanywa na serikali ya awamu ya nne kwa ajili ya kukweza baadhi ya watu ambao wakati huo walishiriki kuyaatekeleza na kupata sifa za kila aina.


Tukirudi leo hii watanzania na waafrika kwa ujumla wamepata elimu ya kutosha kukaa na kupanga namna bora ya kupata maendeleo yao bila kuumiza au kupoteza uhai wa watu bila sababu.


Awamu ya nne kwa mfano mradi mmoja tu wa Mabasi ya Mwendo kasi umegharimu fedha nyingi ambado labda wa Taalam wa mambo ya uchumi wanaweza wakatuambia kama leo kuna mradi unaofikia hata nusu ya gharama ya mradi ule.
Hata hivyo Serikali ya awamu hiyo haikutumia nguvu kubwa kujisifia na kuwanyamazisha wakosoaji.


Kwa kifupi tu ni kwamba maendeleo yoyote duniani yanapaswa kuletwa bila kudhalilisha utu wa mtu.
Kama mtu anabomoleshwa nyumba basi ni vema akalipwa fidia ili asipoteze jasho lake.

Awamu ya Tano imeridhi maendeleo makubwa ya awamu ya nne na tatu chini ya mfumo wa kidemokrasia.

Na ni wajibu wa awamu ya tano kuendeleza pale ilipoachia awamu ya nne.
Kwa kurekebisha mambo yale machache yasiyofaa na kuleta mazuri zaidi bila kuathiri haki na uhuru wa watu hasa mtu mmoja mmoja.
Kama mtu ana makosa basi akamatwe apelekwa gerezani na sio kupotea kama Ben Saanane na Roma Mkatoliki.
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom