Leo ni miaka miwili kamili tangu Rais Magufuli aape kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 05/11/2015. Katika miaka hii miwili kama ambavyo nimekwisha sema kwenye post zangu hapo awali, ni kwamba Rais amekwisha jipambanua ni wa aina gani na mwenye malengo gani kwa maslahi ya Taifa. Katika kipindi hiki cha miaka miwili tumeona maboresho katika sekta mbalimbali za umma zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi. Tumeona maboresho katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya usafiri (ardhini, majini na angani), uchumi wa nchi n.k.
Katika hili la uchumi tumeshuhudia vita vikali anavyovipagana, hasa katika sekta ya madini, licha ya kukatishwa tamaa na baadhi ya Watanzania wenzake. Ni vita inayoonesha matumaini mapya kwa wananchi. Tumeona jinsi Wazungu wenyewe wanavyogeukana na wengine kufikia hatua ya kujiuzulu nafasi zao kisa ni fedha wanazotakiwa kutulipa. Hayo yote ni kwa sababu ya msimamo usiyoyumbishwa kwa Rais Magufuli.
Mbali na maboresho hayo hapo juu, pia tumeona Rais Magufuli akiwa amefanikiwa katika kujifanyia “Self-Branding”. Ameonesha wazi kwamba maana ya ushirikiano si kwamba kila siku lazima wewe ndo uende kwa jirani kupiga hodi, jirani naye anaweza kuja kwako bado mkawa katika mahusiano mazuri. Tumeona viongozi wengi wa nchi wakipishana kuja kukutana na Rais Magufuli na kusaini naye mikataba mingi ya ushirikiano katika sekta mbalimbali. Hakika “Hapa Kazi Tu” tumeiona wenyewe kwa macho yetu.
Kwa upande mwingine nina “Dummy Government” ambayo naifanyia tathmini endapo ingeshika dola. Na hiyo si nyingine bali ni serikali ya “Safari Ya Matumaini”. Najiuliza hivi hawa wangeshika dola, tungeweza kuona mabadiliko chanya haya yote tunayoyaona katika serikali hii? Naiona hiyo serikali kama ni serikali isiyokuwa na “Human Resource” wa kutosha. Najiuliza Mawaziri na Manaibu Mawaziri wangewatoa wapi ukizingatia Wabunge wengi wao wanaonekana kutokuwa na uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo. Mfano Kubenea angepewa Wizara, ingekuwaje? Nawaza tu, any cabinet reshuffle if any ingetoa wapi hao watu? Au ndio kusema hata kama kuna uozo basi tungeenda nao kwa awamu mzima kwa sababu tu hakuna watu mbadala?
Huenda mpaka sasa wangekuwa bado wanajipanga. Wangekuwa bado wanajengeana uzoefu kutokana uwezo wao mdogo na kujijenga wao kama Serikali ya Chama kilichotoka katika upinzani. Wakati Mh. Edward Lowassa akihamia upinzani alisema kwamba kulikuwa na watu wengi ndani ya CCM ambao wangemfuata huko aliko, lakini hicho hakikutokea. Hata hivyo najaribu kuwaza kwamba kama watu hao wangemfuata kwa kile kinachosemekana kuwa aliwaahidi vyeo katika serikali yake, basi hiyo “Serikali Ya Matumaini” ingejaa wanafiki na mafisadi wanaopenda kujinufaisha wao binafsi at the expense of maskini wengi. Kuna uwezekano mkubwa maendeleo haya ambayo yamekwisha fikiwa na Rais Magufuli yasingekuwepo kwenye Serikali ya “Safari Ya Matumaini”.
Waswahili wanasema “Sumu haijalibiwi kwa kuionja”; hongera Watanzania kwa kukataa kuonja “Sumu ya Matumaini”.