Miaka Miwili ya Rais Magufuli: Hapa Kazi Tu Vs Safari Ya Matumaini

B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Messages
383
Likes
318
Points
80
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2015
383 318 80
Leo ni miaka miwili kamili tangu Rais Magufuli aape kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 05/11/2015. Katika miaka hii miwili kama ambavyo nimekwisha sema kwenye post zangu hapo awali, ni kwamba Rais amekwisha jipambanua ni wa aina gani na mwenye malengo gani kwa maslahi ya Taifa. Katika kipindi hiki cha miaka miwili tumeona maboresho katika sekta mbalimbali za umma zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi. Tumeona maboresho katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya usafiri (ardhini, majini na angani), uchumi wa nchi n.k.

Katika hili la uchumi tumeshuhudia vita vikali anavyovipagana, hasa katika sekta ya madini, licha ya kukatishwa tamaa na baadhi ya Watanzania wenzake. Ni vita inayoonesha matumaini mapya kwa wananchi. Tumeona jinsi Wazungu wenyewe wanavyogeukana na wengine kufikia hatua ya kujiuzulu nafasi zao kisa ni fedha wanazotakiwa kutulipa. Hayo yote ni kwa sababu ya msimamo usiyoyumbishwa kwa Rais Magufuli.

Mbali na maboresho hayo hapo juu, pia tumeona Rais Magufuli akiwa amefanikiwa katika kujifanyia “Self-Branding”. Ameonesha wazi kwamba maana ya ushirikiano si kwamba kila siku lazima wewe ndo uende kwa jirani kupiga hodi, jirani naye anaweza kuja kwako bado mkawa katika mahusiano mazuri. Tumeona viongozi wengi wa nchi wakipishana kuja kukutana na Rais Magufuli na kusaini naye mikataba mingi ya ushirikiano katika sekta mbalimbali. Hakika “Hapa Kazi Tu” tumeiona wenyewe kwa macho yetu.

Kwa upande mwingine nina “Dummy Government” ambayo naifanyia tathmini endapo ingeshika dola. Na hiyo si nyingine bali ni serikali ya “Safari Ya Matumaini”. Najiuliza hivi hawa wangeshika dola, tungeweza kuona mabadiliko chanya haya yote tunayoyaona katika serikali hii? Naiona hiyo serikali kama ni serikali isiyokuwa na “Human Resource” wa kutosha. Najiuliza Mawaziri na Manaibu Mawaziri wangewatoa wapi ukizingatia Wabunge wengi wao wanaonekana kutokuwa na uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo. Mfano Kubenea angepewa Wizara, ingekuwaje? Nawaza tu, any cabinet reshuffle if any ingetoa wapi hao watu? Au ndio kusema hata kama kuna uozo basi tungeenda nao kwa awamu mzima kwa sababu tu hakuna watu mbadala?

Huenda mpaka sasa wangekuwa bado wanajipanga. Wangekuwa bado wanajengeana uzoefu kutokana uwezo wao mdogo na kujijenga wao kama Serikali ya Chama kilichotoka katika upinzani. Wakati Mh. Edward Lowassa akihamia upinzani alisema kwamba kulikuwa na watu wengi ndani ya CCM ambao wangemfuata huko aliko, lakini hicho hakikutokea. Hata hivyo najaribu kuwaza kwamba kama watu hao wangemfuata kwa kile kinachosemekana kuwa aliwaahidi vyeo katika serikali yake, basi hiyo “Serikali Ya Matumaini” ingejaa wanafiki na mafisadi wanaopenda kujinufaisha wao binafsi at the expense of maskini wengi. Kuna uwezekano mkubwa maendeleo haya ambayo yamekwisha fikiwa na Rais Magufuli yasingekuwepo kwenye Serikali ya “Safari Ya Matumaini”.

Waswahili wanasema “Sumu haijalibiwi kwa kuionja”; hongera Watanzania kwa kukataa kuonja “Sumu ya Matumaini”.
 
hashim mwamba

hashim mwamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2016
Messages
1,032
Likes
1,079
Points
280
Age
27
hashim mwamba

hashim mwamba

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2016
1,032 1,079 280
 
UNDENIABLE

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Messages
2,305
Likes
455
Points
180
UNDENIABLE

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2013
2,305 455 180
Imekula kwetu big time. Tunaishi km hatuishi. Katubadilikia km sio yeye vile. Mungu anamwona.
 
I

Interested Observer

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2006
Messages
1,480
Likes
523
Points
280
I

Interested Observer

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2006
1,480 523 280
Leo ni miaka miwili kamili tangu Rais Magufuli aape kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 05/11/2015. Katika miaka hii miwili kama ambavyo nimekwisha sema kwenye post zangu hapo awali, ni kwamba Rais amekwisha jipambanua ni wa aina gani na mwenye malengo gani kwa maslahi ya Taifa. Katika kipindi hiki cha miaka miwili tumeona maboresho katika sekta mbalimbali za umma zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi. Tumeona maboresho katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya usafiri (ardhini, majini na angani), uchumi wa nchi n.k.

Katika hili la uchumi tumeshuhudia vita vikali anavyovipagana, hasa katika sekta ya madini, licha ya kukatishwa tamaa na baadhi ya Watanzania wenzake. Ni vita inayoonesha matumaini mapya kwa wananchi. Tumeona jinsi Wazungu wenyewe wanavyogeukana na wengine kufikia hatua ya kujiuzulu nafasi zao kisa ni fedha wanazotakiwa kutulipa. Hayo yote ni kwa sababu ya msimamo usiyoyumbishwa kwa Rais Magufuli.

Mbali na maboresho hayo hapo juu, pia tumeona Rais Magufuli akiwa amefanikiwa katika kujifanyia “Self-Branding”. Ameonesha wazi kwamba maana ya ushirikiano si kwamba kila siku lazima wewe ndo uende kwa jirani kupiga hodi, jirani naye anaweza kuja kwako bado mkawa katika mahusiano mazuri. Tumeona viongozi wengi wa nchi wakipishana kuja kukutana na Rais Magufuli na kusaini naye mikataba mingi ya ushirikiano katika sekta mbalimbali. Hakika “Hapa Kazi Tu” tumeiona wenyewe kwa macho yetu.

Kwa upande mwingine nina “Dummy Government” ambayo naifanyia tathmini endapo ingeshika dola. Na hiyo si nyingine bali ni serikali ya “Safari Ya Matumaini”. Najiuliza hivi hawa wangeshika dola, tungeweza kuona mabadiliko chanya haya yote tunayoyaona katika serikali hii? Naiona hiyo serikali kama ni serikali isiyokuwa na “Human Resource” wa kutosha. Najiuliza Mawaziri na Manaibu Mawaziri wangewatoa wapi ukizingatia Wabunge wengi wao wanaonekana kutokuwa na uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo. Mfano Kubenea angepewa Wizara, ingekuwaje? Nawaza tu, any cabinet reshuffle if any ingetoa wapi hao watu? Au ndio kusema hata kama kuna uozo basi tungeenda nao kwa awamu mzima kwa sababu tu hakuna watu mbadala?

Huenda mpaka sasa wangekuwa bado wanajipanga. Wangekuwa bado wanajengeana uzoefu kutokana uwezo wao mdogo na kujijenga wao kama Serikali ya Chama kilichotoka katika upinzani. Wakati Mh. Edward Lowassa akihamia upinzani alisema kwamba kulikuwa na watu wengi ndani ya CCM ambao wangemfuata huko aliko, lakini hicho hakikutokea. Hata hivyo najaribu kuwaza kwamba kama watu hao wangemfuata kwa kile kinachosemekana kuwa aliwaahidi vyeo katika serikali yake, basi hiyo “Serikali Ya Matumaini” ingejaa wanafiki na mafisadi wanaopenda kujinufaisha wao binafsi at the expense of maskini wengi. Kuna uwezekano mkubwa maendeleo haya ambayo yamekwisha fikiwa na Rais Magufuli yasingekuwepo kwenye Serikali ya “Safari Ya Matumaini”.

Waswahili wanasema “Sumu haijalibiwi kwa kuionja”; hongera Watanzania kwa kukataa kuonja “Sumu ya Matumaini”.
Akili ni ......... kila mtu ana zake.
In the 50 plus years of CCM bado unaongea haya!!
Very low IQ
 
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Messages
383
Likes
318
Points
80
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2015
383 318 80
Akili ni ......... kila mtu ana zake.
In the 50 plus years of CCM bado unaongea haya!!
Very low IQ
Very Low IQ too. Sijasema Fifty Years of CCM, bali 2 Years of Magufuli. Sasa abrupt development mliyokuwa mnatuahidi mlitaka mlidhani tuna Low IQ kama nyie? We analysed the situation thoroughly tukagundua ni ujanja ujanja tu ndo mliokuwa nao
 
DR MANJALA

DR MANJALA

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Messages
281
Likes
134
Points
60
DR MANJALA

DR MANJALA

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2013
281 134 60
Teuzi zilishafanyika utaumia kama jerii muroho
 
Usher-smith

Usher-smith

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2015
Messages
6,742
Likes
5,733
Points
280
Usher-smith

Usher-smith

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2015
6,742 5,733 280
Kwa hali ilipofikia sasa
Tunahitaji safari ya matumaini aisee
 
swissme

swissme

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Messages
13,338
Likes
17,330
Points
280
Age
18
swissme

swissme

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2013
13,338 17,330 280
PHD HEWA.

SWISSME
 
O

olyanu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Messages
1,840
Likes
1,059
Points
280
O

olyanu

JF-Expert Member
Joined May 30, 2017
1,840 1,059 280
Hongera sana na wewe kwa kudhihirisha ma 0 brain mlivyo wengi bongo
 
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Messages
383
Likes
318
Points
80
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2015
383 318 80
Teuzi zilishafanyika utaumia kama jerii muroho
Sihitaji uteuzi mie bro, fursa nilizonazo zinanitosha kabisa kuendesha maisha yangu. We endelea tu kumuimbia huyo tapeli wa kisiasa unayetegemea atakuletea maendeleo overnight.
 
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Messages
383
Likes
318
Points
80
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2015
383 318 80
Hongera sana na wewe kwa kudhihirisha ma 0 brain mlivyo wengi bongo
Zero brain kama ya kumsifu kwa mapambio mtu ambaye mara ya kwanza mlimponda kwamba hasafishiki kwa kitu chochote. Yaani pale hamkujua tu, ndio ulikuwa mwisho wenu kisiasa as you are now decelerating. Tukifika 2020 hamtakuwa tofauti na UPDP
 
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Messages
383
Likes
318
Points
80
B

Benmpo

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2015
383 318 80
Kwa hali ilipofikia sasa
Tunahitaji safari ya matumaini aisee
Wakati wenzio wako kwenye safari ya uhakika, we endelea kubebeshwa matumaini kichwani mwako ambayo hayatatekelezeka daima.
 
M

Mligo Augustino

Senior Member
Joined
Nov 29, 2017
Messages
101
Likes
207
Points
60
M

Mligo Augustino

Senior Member
Joined Nov 29, 2017
101 207 60
"Ukweli utawapeni uhuru wa kweli"
Ni kweli ya kwamba Raisi JPM kwa muda mfupi wa miaka 2 ameonyesha UBUNIFU wa mambo makubwa na yenye TIJA kwa Taifa letu. Ukweli huo unathibitishwa na litania ya mbo aliyoyabuni kama ifuatavyo:
1.Ujenzi wa reli ya kisasa.
2.Kufufua shirika la taifa la ndegr.
3.Kulinda rasilimali za nchi(madini,wanyamapoli nk).
4.Upanuzi wa bandari
5.Ujenzi wa flyovers(Dar&Mwanza).
6.Upanuzi wa barabara ya Dar to Kibaha.
7.Ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege nchini.
8.Ujenzi wa meli na vivuko(Nyasa,Dar,Victoria nk).
9.Ujenzi wa hospitali mpya za mikoa(Njombe nk).
10.Kukomesha rushwa na ufisadi nchini.
11.Uboreshaji wa hiduma za afya(kununua madawa viwandani).
12.Uboreshaji elimu(elimu ya msingi bure).
13.Mifumo ya malipo,utunzaji kumbukumbu za serikali kuwa kielectronic(e-government).
14.Kuongeza thamani ya zao la korosho.
15.Kuamusha roho ya uzalendo.
16.Kuthamini fani(professions) za watu.
17.Kutumia kwa haki taasisi za umma kujenga miradi ya taifa(TBA,SUMA JKT nk).
18.Kuleta usawa wa kijamii ktk taifa.
19.Kuondoa fedha feki mitaani(kufuta uchumi wa bandia).
20.Kufanya uhakiki wa mifumo mbalimbali(watumishi hewa,wanafunzi hewa,maskini hewa-TASAF, mbolea hewa,nk).
21.Kujenga nidhamu na uwajibikaji kazini(public service).
22.Kusamehe wafungwa waliohukumiwa kunyongwa(ni mara ya kwanza tangu kuumbwa taifa hili).Ameitendea haki ibara ya 45 ya katiba.
23.Kubana matumizi serikalini.
24.Kufufua na kukirudisha chama cha mapinduzi kwa wananchi.
25.Serikali kuhamia Dodoma.
26.Kudumisha amani ya nchi.
27.Kuanzisha viwanda(sera).
29.Kuanzisha wakala wa barabara za TAMMISEMI.
30.Kupunguza mishahara ya wakurugenzi wa taasisi za umma.
31.Kuendelea na ujenzi wa barabara zinazounganisha mikoa.
32.Kufanikiwa mkakati wa ujenzi wa bomba la mafuta TZ.
33.Ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezo Dodoma.
34.Kukomesha(kupunguza) ufisadi bandarini.
35.Kuanzisha ajira za mikataba maalum kwa wakurugenzi wa taasisi za umma.
36.Kuweka mkakati wa kisheria wa kupunguza utitili wa vifuko ya kijamii.
37.Kulinda mazingira nchini.
38.Kupunguza migogoro ya wafugaji na wakulima
39.Kuboresha na kujenga mifumo ya upatikanaji wa maji nchini.
40.Kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini(REA).
41.Kuwa na baraza la mawaziri dogo,lakini lenye uwajibikaji mkubwa.
42.Kuhakiki mali zote za CCM na kuziwekea usajili salama.
43.Kuthamini na Kufanyia kazi ushauri wa kitaalam unaotolewa na vyombo vya dola(hasa usalama wa taifa).
44.Kuwathamini na kuwa upande wa wananchi wa kawaida.
45.Serikali kuwa na "meno" bila kujali utajiri wa mtu.
46. Kuzuia balozi zetu ktk nchi mbalimbali kuwa sehemu ya kupeleka watu walioshindikana.
47.Kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii.Hakuna cha bure.Hapa kazi tu.
48.Kulinda soko na thamani ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.
49.Kuchukua hatua kwa wakati.
50.Kujenga bwawa kubwa la S.guarge la kuzalisha umeme MW 2100.
Note: Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo Raisi Magufuli ameyafanya kwa miaka 2.Angekuwa mtu mwingine au mchi nyingine mambo haya yangefanyika kwa miaka zaidi ya 20.Huu ni ubunifu wa hali ya juu ambao haujawahitokea mahali popote duniani. Magufuli is a gift from God.He is an extra-ordinary human being.Watanzania tuungane ktk kumuombea sana, ili aendelee kutufanyia miujiza mbalimbali ya maendeleo kwa taifa letu.Watu kama hawa wako wachache sana duniani.Na hawazaliwi ovyo. Viva Magufuli.God bless you all the time. Endelea kutenda mema.Hata Yesu alichukiwa na baadhi ya watu kwasababu ya kutenda mema.
 
I

Isa khamisi

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2017
Messages
331
Likes
306
Points
80
I

Isa khamisi

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2017
331 306 80
Nakubaliana na wewe anafanya mambo hata marais wote wastaafu walikuwa hawadhubutu kufanya kwa kuheshimu katiba ,sheria na taratibu za nchi na kuwaachia wafungwa wengine ambao hawakustahili kuwachiwa kwa makosa waliyoyafanya
 
Tukundane

Tukundane

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Messages
9,167
Likes
3,537
Points
280
Age
53
Tukundane

Tukundane

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2012
9,167 3,537 280
Hata pyupyu za hadharani kwa wakosoaji nazo zimejitokeza katika utawala wake,kwa Mara ya kwanza Ben na mwandishi wa habari wameyeyuka kimalaika,askofu mtanzania kwa kuzaliwa kahojuwa uraia wake.
 
weed

weed

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Messages
2,124
Likes
2,173
Points
280
weed

weed

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2012
2,124 2,173 280
51-KUWABOMOLEA WATU MAJUMBA NA VIBANDA VYAO.
dsc1687_0_o.jpg
 
Forum statistics

Threads 1,235,809
Members 474,742
Posts 29,236,731