Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
MIAKA MIWILI YA ACT WAZALENDO, WAWEZA KUZIKOSOA SIASA ZA CHAMA HIKI?
Leo ni tarehe 5/5/2016 ni miaka miwili kamili tangu chama chetu kipate usajili wa kudumu, na kwa kipindi chote hicho chama chetu kimepitia misukomisuko mikubwa sana.
Misukosuko yote hiyo ilisababishwa na mfumo wenyewe wa chama, mfumo wa kuwatengeneza wanasiasa na wanachama wake, waendane chama hata wafuate siasa za masuala badala ya siasa za matukio na siasa za kusakama watu.
Chama chetu kimeanzishwa katika nchi ambayo vyama vyake vya siasa zina itikadi na falsafa zilizoainishwa vizuri katika katiba zao na machapisho yao, lakini haviendeshwi chini ya itikadi na falsafa zao, na kubwa zaidi wanashindwa kuishi ama kusimamia hizo itikadi.
Kwasababu hiyo na ukizingatia wanasiasa ni walewale na wanachama wanatoka katika umma uleule wa watanzania ambao tangu CCM dishi lake la siasa za ujumaa na kujitegemea liyumbe kiasi wasijulikane kama ni wajamaa au mabepari haujawahi kupata chama chenye kujipambanua kiitikadi na kifalsafa kivitendo, na kwasababu hiyo walikipokea au waliingia ndani ya ACT huku wakiendeleza maisha ya kiCHADEMA ama kiCCM, na chama kazi yake kubwa ni kuhakikisha kinawatoa katika maisha ya kimazoea, maisha ya kuishi bila kufuata taratibu na mipaka tulio jiwekea wenyewe.
Kama mlipata habari za migogoro ndani ya ACT kipindi kile, basi mjue haiukuwa migogoro bali ilikuwa kazi ya mfumo wa chama kuhakikisha viongozi na wanachama wake wanaishi chini itikadi na falsafa ya chama, na kwasababu hiyo basi, mafanikio yetu kwa miaka miwili yamekuwa MAKUBWA zaidi ukilinganisha na changamoto za hapa na pale.
Yako mengi, lakini katika uchaguzi uliopita, uchaguzi ambao ushabiki wa UKAWA na CCM ulivyotoa fursa mbili aidha Magufuli au Lowassa, chama chetu kikiwa ndio kina mwaka mmoja na kigeni kabisa katika siasa za Tanzania, kilifanikiwa kupata mbunge mmoja na madiwani wasiopungua 50.
Kwavyovyote vile haikuwa kazi nyepesi hata kidogo kujaribu kupenya kati ya UKAWA na CCM, lakini hatukuwa na namna sababu tulihitaji kujenga chama mbadala chenye lengo la kubadili mitazamo ya watanzania kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Viongozi wetu wana sifa nyingi nzuri na zinazo watofautisha na viongozi wa vyama vingine, lakini sifa yao kubwa ambayo ni nzuri sana ni kusikiliza, kusoma na kufuatulia.
Kwasababu hiyo basi, naomba nichukue fursa hii kuwaomba mtoe maoni yenu au mitazamo yenu juu ya siasa za chama chetu na kubwa zaidi nitafurahi sana nikisoma maoni ya KUKOSOA zaidi kuliko ya KUPONGEZA, sababu ili tusonge mbele kwa maslahi ya taifa letu, tunahitaji kukosolewa zaidi kuliko kupongezwa.
Kiongozi wa chama Zitto Z Kabwe
Mwenyekiti wa chama Anna Mghwira
Katibu wa uenezi Ado Shaibu
Mashauri wa chama Kitila Mkumbo
Tuko nao humu na watasoma michango yenu kama wanavyosoma siku zote, na kwa vyovyote vile hatawatapuuza sababu wao si watu wa kupuuza.
Njano5
Whatspp/call 0622845394