Miaka miwili baadaye...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kijijini Leo Hii leo inatimiza miaka miwili tangu ianze na kuongoza kwa namna ya pekee mapambano ya kifikra, yenye lengo la kubadili mtazamo wa wananchi wa Tanzania kuhusu nchi yao ili waweze kujitoa zaidi, kujisahihisha zaidi, na kuitumikia kuliko wakati mwingine wowote wa historia yetu kama Taifa.

Matangazo ya kwanza ya KLH News yalianza kurushwa kupitia http://www.mwanakijiji.podomatic.com miaka miwili iliyopita na katika hilo tumekuwa tukiongoza kwa kutolea maoni masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii, na kimaisha yanayowahusu Watanzania.

Licha ya kutoa maoni na mijadala tumeweza pia kuwaletea mahojiano na watu mbalimbali mashuhuru ambao wamekuwa na taathira kubwa katika maisha ya Watanzania mahali popote walipo. Mwaka jana licha ya mahojiano mengi ambayo tuliweza kuleta na ambayo yanakumbukwa sana ni yale ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Asha Rose Migiro mara tu baada ya kuteuliwa kwake.

Tumeweza kushiriki katika mijadala mbalimbali inayohusu taifa letu kwa maandishi au kwa sauti na pia kusimama na wale wote ambao tunaamini hawatendewi haki na serikali ya nchi yao. Mwaka jana tuliweza kusimama kidete kulileta suala la vijana waliokwama Ukraine na mwaka huu tumeanza kwa kusimama tena na vijana wawili waliokamatwa pasipo sababu na maafisa usalama.

Tunaahidi tutaendelea siyo tu kuwa wa kwanza kuwaletea habari lakini pia kusimama pamoja na wale wote wanaodhulumiwa, wanaoonewa na wale ambao kwa namna moja au nyingine wanajikuta wako upande wa dhulma.

Na zaidi ya yote tunaahidi kuendelea kuongoza mapambano ya mabadiliko ya kifikra yenye lengo moja kubwa; kuamsha dhamira na mawazo ya Watanzania ili:

1. Waweze kujua wanastahili vitu vyema cha kwanza miongoni mwao kikiwa ni viongozi bora
2. Waweze kujiamini kuwa na wao wanaweza; wanaweza kujenga Taifa la kisasa na lenye utawala bora wa sheria na la kidemokrasia.
3. Waweze kutambua kuwa nchi hii ni yetu sisi sote na wale walioko madarakani wako kama dhamana na kuondolewa kwao kupitia sanduku la kura siyo kuwaonea bali ni kwa ajili ya kutafuta kilichobora zaidi (angalia 1 hapo juu)

Hili ndilo lengo letu na lengo hili linaongozwa na kauli mbiu isemayo "Hapendwi mtu, haogopwi mtu, hapendelewi mtu na haonewi mtu; yote yanazungumzika".

Tunapoanza mwaka huu wa tatu, tunajikuta tukitoa mwaliko kwa waandishi wa habari, wapiga picha, na waandika maoni (columnists) na bloggers kuungana nasi katika kuwafikia watu wengi zaidi na kuwaletea Watanzania habari mapema iwezekanavyo. Yeyote ambaye anataka kujitolea katika kushirikiana nasi tafadhali atuandikie kupitia klhnews@klhnews.comThis e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it

Katika kushirikiana huko tutafungulia sehemu nyingine za tovuti hii zikiwemo sehemu za Blogs ili watu waweze kuanza kublog na kuwa na sehemu zao za kutolea maoni. Kwa pamoja tutaweza na mmoja mmoja tutashindwa kwa pamoja!

Mwaka huu wa tatu, ni mwaka wa vitendo zaidi kuliko maneno ya kizalendo!! Kama unapenda kupatiwa mpango wa mwaka wa tatu utakaotoka wiki ijayo ambao ni kwa kuombwa tu tafadhali andika kwa mwanakijiji@klhnews.comThis e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it na uone ni jinsi gani unaweza kushirikiana nasi.

Asanteni: KLH News Management
 
Hongera sana. Ulitusaidia sana wakati JF ilipokuwa haiko hewani kujua nini kinaendelea katika sakata lile.
 
My man,

Happy Birthday!

Nakumbuka kama jana, tushafikisha miaka miwili tayari? Upande mmoja naona kama jana, lakini nikiangalia kazi iliyofanyika na watu tuliowahoji inakuwa kama miaka 10!

Kutoka hapa kama wanavyosema "The sky is the limit".Katika historia ya Tanzania online media zilizoleta impact umeshaingia, tufanye jitihada ya kufanya makubwa zaidi.Tunapowasaili tusiwaletee undugu sana, hata kama tunawaamini (seldom) tu play devil's advocate sana kama Tim Russert mazee.

Nuff rispect and big up unoself.
 
Happy Birthday KLH News
Na hongera sana mwanakijiji kwa kazi nzuri.
 
My man,

Happy Birthday!

Nakumbuka kama jana, tushafikisha miaka miwili tayari? Upande mmoja naona kama jana, lakini nikiangalia kazi iliyofanyika na watu tuliowahoji inakuwa kama miaka 10!

Kutoka hapa kama wanavyosema "The sky is the limit".Katika historia ya Tanzania online media zilizoleta impact umeshaingia, tufanye jitihada ya kufanya makubwa zaidi.Tunapowasaili tusiwaletee undugu sana, hata kama tunawaamini (seldom) tu play devil's advocate sana kama Tim Russert mazee.

Nuff rispect and big up unoself.

Kama utani ndugu yangu, na kama mzaha ukanionesha njia ya kuweka sauti. I'm forever grateful for that simple link.. http://www.podomatic.com Sikujua tungefikia hapa!! and yes! the sky now is the limit, if it it dare limit us we'll move it too!!
 
could not have done it without the dedicated and loyal support of hundreds of frequent visitors, contributors, fans, and critics. I truly thank each and everyone of you those I know by names and those who remain nameless!

Thanks a million and I promise you to work more diligently and always putting my country its people first no matter what!!!

Your Host!

M. M. M.
 
KLH News hongera sana.... MKJJ (oops, naona ni M.M.M) hongera sana Mkuu.... Kwa kweli miaka miwili inaweza kuonekana ni michache sana kwa wasiojua dedication (muda, costs) ambazo mtu anatakiwa aweke kufanikisha hiki ambacho KLH News imeweza kufanya na naendelea kufanya... Kwangu kwa kweli kutengenisha kati ya KLH News na JF inakuwa ngumu sana sababu toka tulipopata matatizo kule JF na MMM akatusitiri through ujumbe kule kwa Issa Michuzi, kila nikishindwa kuiona basi breki ya kwanza ni kule kwa kaka yake JF, KLH ambapo kama kawaida huwa kuna yaliyojiri na kama kuna mushkeli kwenye JAMVI letu basi kuna habari ya kulikoni!!!

Viva mapinduzi ya kimtandao Tanzania, viva wanaMapinduzi!!!!

Keep up the Good WORK!!
 
Back
Top Bottom