Miaka mitatu ya jasho kwenye Forex na ukweli mchungu niliojifunza, still 'GAME ON'!

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
3,910
2,000
Niseme tu ukweli, upepo wa Forex ulivoingia Tanzania na mimi sikuwa nyuma. Nilijitoa na mimi kimasomaso kuisaka fursa.

Kwa takribani miaka 3 kwenye game la Forex, imekuwa ni miaka ya kujifunza zaidi. Sikuweka nia ya kupata chochote kwa mda wa short term. Niliamua kupeleleza sana hii biashara, na kwa kufanya hivo ikanifanya nika expand territory kwenye kujifunza masoko yote ya fedha yanavofanya kazi (watu wanajua tu Forex, lakini masoko ya fedha yana insruments nyingi sana; Cryptos, Stocks, Bonds, Futures, Commodities, Options etc)

Baada ya kujitoa haswa na kuchimba hii kitu, kuna ukweli fulani naanza kuupata ambao nadhani ili mtu uweze kutoboa kwenye hii biashara lazima uuelewe mapema

1) Forex ni ukweli, ni kweli Forex ipo na ni kweli pia kuna watu wanatengeneza pesa na utajiri kupitia Forex. Hata hapa Tanzania wapo. Na kuna wengine wanatengeneza tu pesa ya kawaida kujikimu na maisha yao. So kama wewe ulikuwa na ndoto kujiingiza kwenye hii biashara usiogope kuingia, na mimi ntakushauri uingie maana hii kitu ni kweli.

2) Hakuna superstar wa Forex, mtu asikudanganye eti mimi ni master wa Forex, kwamba nina uwezo wa kuwa natengeneza pesa. (BIG NO). Watu wengi sana wanakuwa wanadanganyika na wale vijana wa Instagram, wakiamini ndio magwiji wa Forex dunia nzima. Hakuna kitu kama hicho. Usidanganyike ukapoteza mapesa yako kwa watu wadanganyifu.

3) Self learning is the key, huu ndo msing haswa wa kujua kitu chochote 'Jifunze mwenyewe na ukifanye kiwe hobby' unakuta mtu anajisumbua kutafuta mentors mpaka south africa anachoma mapesa mengi kujifunza kitu ambacho kinapatikana bure kwenye internet. We hujiulizi kichwani, 'kama ingekuwa hao mentors wanatengeneza pesa kwenye Forex, ni kwanini watumie resources nyingi kuandaa madarasa ya kufundisha watu? Jibu la hili swali linapatikana kwenye point namba 2 'Hakuna superstar wa Forex'. Ukiwachimba sana mentors utagundua asilimia kubwa wamechezea vichapo vikali sana kwenye Forex.

4) Forex au financial market haihitaji kupumzika (itakuhitaji uwe active almost 24/7 kwenye kufanya analysis), hapa ndo mtiti unapoanza ndo mana watu wanazidi kuona Forex ni difficult job on earth. Na sema hivo kwa sababu masoko ya fedha yapo constantly dynamic kutegemeana na flow ya news either (Economic, political etc) na uzuri hizi news huwa tunazipata bila ubaguzi. Ukiwa trader unatakiwa kila habari ya kidunia unayoipata uifanyie analysis na kuona ni jinsi gani ita affect movement za financial markets. Analysis sio kuchora chora yale mamistari kwenye chart halafu uwe kama mchawi useme eti EURUSD iko bullish. Kufanya analysis itakuhitaji vitu zaidi ya hivo.

Kwenye hii hoja namba 4 ndipo inapokuja lile swali la kwanini Retail traders wengi in the long run wataishia kupata hasara while institutional traders huwa wanaishia kupata faida. Jibu la hili swali lipo kwenye ANALYSIS.

Institutional traders kama yale mabenki makubwa kina Morgan Sachs na Goldman Stanley, huwa yana mpaka vitengo vya kufanya research. Yaani mfano pair kama EURUSD, unakuta kuna watu washaangalia angle zote za uchumi kuanzia kwenye issues kama Inflation, Interest, Investors sentiment, issue ya Corona labda, yaani kwa ufupi ni kama mtu anafanyiwa operesheni, wanamulika in and out. Halafu sasa baada ya hapo ndo wataalamu wa ku trade wanadeal na zile charts na ma volume but wanakuwa guided na research.

Mtu usipokuwa mvivu, unaweza kufanya kama wanavofanya goldman sachs, lakini huwezi fanya hayo yote kama akili yako haija concentrate na kama haupo committed. (So concentration, commitment, open minded ni silaha muhimu sana hapa)

5. Usi concentrate completely kwenye Forex, forex ni sehemu tu ya financial market;
kwa mfano wangu mimi hii miaka mitatu ya kujifunza, ilinifanya kupanua wigo wangu mpaka kwenye stocks, na nilifanikiwa pia kuwekeza kwenye stock markets nje ya Tanzania na hapa Tanzania. Na huwezi kuamini returns has been super so far. Yaani ni kwamba akili yako isifikirie Forex tu kila mda. Ipanue iende pia kwenye masoko ya fedha mengine. (Diversification: mfano kwenye utajiri wako unaweza ukadiversify hivi (30%- stocks, 20% - bonds, 25% - Cash na 25% - cash ya ku trade) yaani kitu chenye muonekano huo.

6. Kamwe usiweke fikra za pesa mbele, utafeli mapema ukifanya hivo; hii imekuwa ngumu kidogo kwa watu wengi. Yaani unapoambiwa Forex, unaanza kuziona pesa, hii sio sahihi, inapelekea watu kuwa na tamaa, na ukishakuwa na tamaa hauwezi kusonga mbele kwenye hii biashara, itakuwa ngumu ku stick na style yako ya ku trade, itakuwa ngumu ku stick na kufanya analysis, utakata tamaa mapema.

*******
Kuhusu performance yangu kwenye forex, ni ya kawaida, na kwa sababu nimekuwa mtu wa kujifunza kila siku i am becoming so much optimistic about the future. Naona kabisa kuna kitu kikubwa kinakuja, sio tu kwenye Forex ila kwenye angle nzima ya masoko ya fedha (refer point namba tano). Financial market ni ulimwengu wa kipekee sana sana, nisehemu pekee unapoweza kunusa pesa kwa puwa, kama unavoweza kunusa harufu ya damu.
 
secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
3,679
2,000
Hujui kitu ww bado mweupe sana....!!?
watu tupo kwenye fx mwaka wa 13
mm sio bingwa na wala sijui bado hiyo fx
but my strategy ni kufanya analysis na ku-control losses cheza na lot size.....
kwa mfano kama una account ya usd 5000
cheza na lot size ya 0.10,0.20, na 0.30 ukiona loss imeenda beyond 150usd close hiyo trade......
then angalia opportunity zingine.....
 
kateka

JF-Expert Member
Nov 30, 2012
502
500

Mambo mengi karibia yote hata mimi katika kujifunza kwangu nimebaini hivyo isipokuwa kwenye Namba 4 sijaafiki kwa asilimia 100. all in all umeeeleza vitu vya msingi sana ambavyo vinaweza kuwa kama mwongozo kwa mtu anayeingia kwenye hii biashara kwa mara ya kwanza.
 
Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
9,188
2,000
Wewe ndio umeongea ukweli sasa. Hamna unafiki hata chembe, utapeli wala kujisifia.
Hii forex ni biashara kama biashara nyingine tu, cha muhimu ni kusoma upepo/ramani ya namna soko lilivyo na litakavyoendelea kuwa siku za mbeleni.
Sio mtu unajua kabisa mahindi mwaka huu ni kidogo na yapo bei juu alafu wewe unakazana kununua kwa bei hiyohiyo kwaajili ya kuja kuuza mwaka ujao ambao utakuwa ni mwaka wenye neema ya mvua huku ukiona kabisa kila mtu kalima mahindi. Utafilisika na utakufa kwa presha!

Biashara yoyote ni kuangalia ulipo na utakapokuwa mbeleni..... Tamaa bila kuusoma mchezo huko ni kukaribisha mauti
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom