Miaka mitano ya wapinzani kupata ajira za maana nchini

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kati ya awamu zote ni awamu hii ndiyo vijana wengi wasio na ajira za kuaminika wamepata ajira kwa kupambana na serikali. Vijana wengi wa Chadema wamepata ajira nzuri na kubwa serikalini jambalo lilikua nadra siku za nyuma.

Vijana wa CHADEMA na viongozi wa upinzani wamekua ma DC means wanasimamia kamati za ulinzi na usalama huko wilayani. Anna anasimamia kamati ya Ulinzi na Usalama Kilimanjaro na wengine wengi

Vijana hata wazee wengi wamepewa halmashauri kuzisimamia na wengine wameajiriwa bungeni na maisha yao yanasonga.

Wakati vijana na wazee Hawa wakipata ajira kirahisi wapo vijana wa kijani ambao wengi wanafutwa kazi ili nafasi iwe wazi kwa kijana na mzee wa upinzani.

Naambiwa hata hivi karibuni wapo watu itabidi wampishe ofisi mashinji, wampishe ofisi Nasary, wampishe ofisi Mbatia, wampishe ofisi Maalimu seif, na wengine wengi ambao bila kupewa ofisi wapate kuishi mambo hayataenda.

Kwa muktadha huu, watu wanatafuta kuishi na ili uishi nikuigonga nyundo serikali wakuone unajua na unaweza wakusajili uwatumikie wananchi.

Mwalimu aliwahi kusema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na sasa yanatimia, hakuna namna ambayo utaishi bila kuonyesha unaweza toka vyuoni na hata mtaani. Wazingue wakutie ndani then ukiwa ndani watatuma watu wakukuuliza unataka nini wewe waambie nataka kitengo nikapambane na Hawa walionitia ndani, wanakupa kitengo wanakupa V8 wanaelekeza upewe saluti, polea saluti kamshirikishe na mwenzio azingue atiwe ndani waje wamuulize anataka nn wampe mchongo mwisho wa siku watuhumiwa mtakuwa mnatembelea mshangingi na kutanua kitaa. That's life in Tanzania, no politics any more. Shtuka, wazingue
 
Wabunge 19 wa viti maalum wa CHADEMA ni ajira mpya inaandaliwa baada ya kufukuzwa hao wote.

Hovyo kabisa,walimu,madaktari,wauguzi,askari hali zao ngumu kimaisha halafu wao wanatumia fedha ktk mambo ya kijinga.
 
Imekuaje raia wa TANZANIAA wanaishi kama wageni kwenye Taifa Lao? Maana hawajali lolote wala chochote kuhusu serikali na mambo yanayofanyika ndani ya serikali, ili mradi maisha Yao yanasonga mbele kwa kupata ubwabwa na mboga wanaona ni Sawa tu.

Ukimya wao unaweza Sema Wana Taifa lingine tofauti na hili, Kwamba hapa wamekuja kutafuta tu na hawana haja ya Kutengeneza mazingira kwa ajili ya kizazi kijacho.

Tume fika pahala raia wa Tanzania bila aibu anasema yeye siasa haimuhusu kwasababu sio mwana siasa! Anyway hapo utasema labda walinyimwa elimu ndio maana wanatoa kauli kama hizo.

Tuzidi kuwaombea hawa raia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom