Miaka mitano tu kwa Dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka mitano tu kwa Dr. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BWAXY, Sep 8, 2010.

 1. B

  BWAXY Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na
  mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili,
  tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni,
  wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na
  azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake
  popote pale walipo..

  Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere
  kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini
  wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya
  wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani.
  Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.

  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa
  kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila
  woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa
  amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga
  kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?
  Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili
  ajibu bila unafiki!

  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr
  Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana
  na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao
  Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa
  mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa
  ni nini?

  Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora,
  na Mwanza. Waulize mpango wao CCM kama si kuwapa wahindi wanaoleta
  mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi
  wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa
  vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na
  akina Carl Peters.

  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni
  sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo
  lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata
  moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini,
  wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado!
  Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na
  vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni
  sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu
  ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na
  Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na
  wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya
  shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili
  ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji
  yao.

  Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia Mashirika ya umma kuleta tija na
  kutumia hela za wanachama kwa mafufaa ya wanachama, achana na CCM
  wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa nini
  kuwajengea nyumba wanachama wake, mifano michache ni wizi wa mchana wa
  kujenga uzio wa stendi ya mabasi Morogoro kwa shilingi milioni 800, na
  serikali inafumba macho? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anayeweza
  kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea
  watu wala bila kulipiza visasi.

  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya
  walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba
  anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa
  sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba
  za mwalimu. Katika hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule
  uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri
  alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule
  wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake.
  Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili
  imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara
  kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!

  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja
  mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia
  nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto
  utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata
  madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa
  chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa
  nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na
  Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?

  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo Botswana kwa sababu ya
  maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa
  kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya
  umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima
  wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya
  watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua
  tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??

  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi?
  Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni
  akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini
  wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?

  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza
  kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa
  kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national
  parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko
  maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.

  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi
  kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa
  nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika
  kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu
  haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi
  wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache
  woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona
  zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi,
  inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.

  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo
  ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi.
  CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio
  waendelee kututawala na kutunyonya.

  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni
  kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu
  nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote
  zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe
  huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako
  wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu
  haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa
  waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..
   
 2. j

  john wayson Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania tunakila sababu ya kufanya mabadiliko, kwani yote anayosema Dr Slaa yanawezekana, wakati Tanzania ilipopata uhuru kutoka mikono ya wakoloni, haikuwa na kitu, lakini haya yaliwezekana, mwl nyerere aliiongoza nchi hii, maskini, lakini kwakipindi hicho elimu kilitolewa bure, si kufundishwa tu ndo bure no, nikuanzia kalamu, daftari, nauli ya kutoka nyumbani kwenu hadi shule, unapewa kitu inaitwa warrant ya kusafiria kwa wanafunzi, leo hii tupo kwenye technologia, rasilimali nyingi zimegunduliwa,lakini hali ya nchi inazidi kuwa mbaya.

  Elimu imekuwa ghali kupita maelezo,matibabu ndo usiseme, ujenzi, ni juzi tu tumefanya uchaguzi 2005, kilo ya sukari ilikuwa tsh 600/= leo nenda kanunue mimi sikwambii, huenda wengine wanakula kwa mama hawajui haya ndo maana tunashabikia siasa mapenzi, kumpeleka mtoto chuo kikuu kwa sasa si chini ya milion 10/= kwa mwaka. labda kasoma miaka mitano, hivi wewe mkulima wa mtama ma mahindi unandoto za kumsomesha mwanao! kama unabisha haya nenda kaulize Imtu wasoma kwa bei gani, H. kairuki wanasoma kwa bei gani, kcmcollege, hizi vyuo viko Tanzania siyo ulaya.

  Halafu haohao wanafunzi wakihitimu mshahara wanalipwa shilingi ngapi kwa mwezi waulize, si bado tunacheka! tunashabikia siasa za wake za watu, tujiulize je huo wizi wa mke wa mtu umeathiri uchumi wa Tanzania kwa kiasi gani, ukilinganisha richmond na epa! mikataba, mibovu.

  Hivi watanzania hapo tunajifunza nini! umaskini huuhuu unatufanya tuchague viongozi wasio na sifa kwa sababu tu wametoa chochote, miahadi,ya uongo,just imagine mtu anaamua kununua toleo nzima la gazeti isambazwe bure kisa tu inahabari kumchafua mgombea fulani jina, jamani huu ukarimu uko wapi katika kudhamini shughuli za maendeleo! HIVI HUU NI UTU KWELI.

  Kuna yatima wangapi,watoto wanaoishi ktk mazingira magumu wengine hawana hata kitu cha kula jamani si ingekuwa bora hata ukawanunulia hao chakula wakakushukuru! Tunapoongelea haya hatumainishi tunatafuta umaarufu la hasha, tunamzungumzia mtanzania wa kawaida yule wa kijijini kipato chake, afya yake, elimu yake, elimu inayotolewa kwenye shule za kata, ya mwl moja kufundisha mikondo minne, si bora isiwepo kabisa hii shule! dispensary ina medical attendat, maana yake yule mhudumu anayefanya usafi, ndo daktari, ndo nurse, phamasist, ndo lab technologist, unataka kusema Tanzania haina vyuo vya kusomesha watu hao,vipo na wanahitimu kila mwaka wengi tu kwanini wasifike huku kwetu kijijini kufanya kazi!

  Akina mama wanakufa na uzazi, watoto wankufa malaria,pneumonia, diarrhoea, lakini watu wanashabikia siasa za mapenzi, huko mijini wanasahau vijijini kukoje, fika uone, labda ni ulize, hivi tangia uhuru mpaka leo wangapi, wamesha wahi kuona mtoto wa kigogo wa serikali,si sungumzii balozi wa nyumba kumi, wala afisa mtendaji wa kijiji, wala siongelei uongozi ngazi ya wilaya, nadhani umenielewa na lenga nini, anafanya kazi kwenye ofisi ya mtu kama mhudumu wa ofisi, au mwl ngazi za chini, chekechea, nurse attendat,vihi wewe unafikiri mungu aliwapendelea akili sana, no nimazingira tu, anasoma shule nzuri, yenye waalimu wakutosha, mazingira mazuri ya kujifunzia,vitendea kazi ya kufundishia na kujifunzia vyakutosha.

  kwa sababu uwezo upo, nafasi inaruhusu, au kama huamini aje huku kwetu kwenye shule za kata za mwlalimu moja, madarasa 4 halafu uone atapata division ngapi! matibabu wenzetu klinic ya mtoto tu kupata chanjo nairobi, south afrika, uk, usa. shida ninini! pesa ipo, kupimwa tu uzito wa mwili,hadi uswis kitu ambacho hata mchuuzi wa magunia ya mazao angeweza kufanya pale sokoni.

  Ok si lalamiki kwa sababu sina no, ni kwa sababu na sisi huku kijijini tunapiga kura, tuchague viongozi wenye vision ya maendeleo wanaolenga kuweka usawa kati ya mwenye nazo na asiye nazo, kwasababu kitakacho tokea baada ya mda ujao hata sisi tunaorubuniwa kwa visenti na kuchagua viongozi wasio na sifa, vitatuathiri, viongozi wasiofanya utafiti kabla ya kuamua kutenda jambo ambalo litaiweka nchi yetu katika hali mbaya, kiuchumi, kimaendeleo, kielimu, viongozi wetu wana copy na ku pest vitu kutoka nje bila kuangalia madhara yatakayo jitokeza baadaye, kwa mfano,

  vijana wetu wengi wanao soma shule za kata wengi wao wanaishia division 4 akijitahidi point 30 amesoma lakini hajaelewa kitu kwa sababu hakufundishwa vizuri, anarudi kijijni, sasa hivi kuna mgambo kila mahali, anakwenda mgambo anajifunza silaha na mbinu nyingine za kijeshi. anarudi kijijini hana kazi, what do you think, he/she is going to be! kama si kuja kukuwinda wewe unayeshabikia siasa za vijiweni, badala ya kufikiria mustakabali wa nchi yetu.

  Haya ni mawazo yangu tu, ila fanya uamuzi wa busara kuchagua kiongozi unayeona ataleta maendeleo, dont consider ushabiki, urafiki, uanachama, coz if wount cost me it will cost you, if not you your unt, uncle,ect please look out of box.
   
 3. c

  chama JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ni Dr. Slaa tu aliyeasi kanisa Katoliki, kuongea si kutenda
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Acha kudanganya. Dr. Slaa hakuasi Kanisa Katoliki. Ameacha kazi za Kipadri, lakini bado ni Mkatoliki. Kuasi Kanisa Katoliki ni kuacha kuwa Mkatoliki. Hakufanya hivyo. Na hata angekuwa ameacha Ukatoliki hicho hakingekuwa kigezo sahihi cha kumfanya asiwe kiongozi mzuri. Hapo Magogoni ni kwa Kaisari, sio Kanisani.

  Naanza kujiuliza kama CCM ikibadilisha matokeo ya kura tena itakuwaje? Maana wakati wa kesi ya kupinga Dr. Slaa kushinda ubunge, tulisikia ushahidi mahakamani jinsi CCM inavyobadilisha matokeo ya kura (Kama kuna mtu mwenye proceedings za lile kesi naomba aziposti hapa. Zina masomo maalumu).

  Kulishatokea madai hapa kwamba kumekuweko na mkutano wa watu wa TAMISEMI ambapo mama mmoja alipewa kazi ya kusimamia uchapishaji wa karatasi za kura za pembeni. Dalili mbaya, inafaa tuanze kuwa macho sana.

  CCM haitaweza kushinda kihalali. Wananchi wameichoka sana. Na wamepata kiongozi wa kuwafaa sasa, yaani Dr. Slaa.

  Binafsi nina hakika 100% kwamba Tanzania itazidi kudidimia na kudharauliwa kama itairudisha CCM madarakani. Kwa upande mwingine, imagine mwanzo mpya, with Dr. Slaa as President, and a bold and competent man like Tundu Lissu as AG. It would be so nice!
   
 5. j

  john wayson Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila nikilala nakumbuka maneno fulani kwenye biblia Mungu alisema watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa! mimi naona kunabaadhi ya watanzania hata paka wa nyumbani anawazidi akili, kwa sababu paka akijisaidia atahakikisha ameficha, kama hakuna mchanga basi hata kwenye unga kama ukiwa wazi, kulala atalala mahala pazuri, kitandani kwenye nyasi nzuri ect,

  lakini mtanzania mwenzangu, kwanza amepigika over 37 years hatambui hilo, pili, haangalii kesho, tatu hajali mwenzake, nne yuko tayari kuuza hata uhai wake au wa ndugu yake kisa tu kaahidiwa kitu kidogo tu, Tumepata mkombuzi wakutusaidia kurejesha heshima ya nchi yetu, tunampiga vita, ingekuwa afadhali hataakipigwa vita na hao mafisadi maana unga unakaribia kumwagika, laajabu, anayeongea sana na kusemasema maneno machafu ni haohao waungua jua wenzetu,

  embu niambie wewe unayetetea sana ccm, kwenye epa ulipewa bei gani! kwenye richmond ulipata % ngapi! kwenye mikataba ya migodi ulipata ngapi!, jamani hizo vijisenti vya kampeni ambazo mwisho wake tarehe 31 then nikupigika kwa miaka 5. hivi nikwanini hata hata hatushtuki, mpka nchi wahisani wamepunduza mchango wao kwenye budget ya serikali kisa ufisadi, jamani tunafunguliwa macho lakini hatutaki kutazama, mabalozi wa nje nchini tanzania wame appriciate kuwa Dr Slaa ndo angefaa kuwa rais wa hii nchi tangia 2005, sasa sisi wenyenchi wala hatushangai kwanini wamesema hivyo,

  Angalia marekani na nchi zingine zenye watu wanao tumia akili wanavyo fanya, awamu hii wakichukua chama hiki awamu nyingine chama kingine, wana compare utendaji kazi, hawadanganyiki ovyo, wanapima mambo, hizi njaa kama hazitatuua mungu asaidie, Tumefika hatua ya kutukanwa na wagombea, akawaambia wananchi hata msipo nichagua nitashinda tu, nakweli akatangaswa mshindi,usishangae ni wapi huko, ndani ya Tanzania hii hii. amekuwa mbuge over 25yrs, hilo jimbo barabara mbovu mpaka basi, hospitali ndo usiseme, shule ndo basi,

  sasa kuna sababu gani ya kuendelea kuburuzwa! kipi ngumu mbona twa badilisha chakula, nguo, njia za kupita, magari ya kusafiria, tunashindwa nini wa Tanzania, au uelewa ndogo! lakini hapana nakataa,tunaelewa,ila... yeboyebo, na kofia tutazimiss kwani tumeshazoea kuwa vibao vya matangazo, kila mahali pamechorwa picha na maandishi, unaonaje hapo zinatutosha kweli! kwanini basi usipewe walau blanket shuka sare za wanao kwendea shule, walau upunguze budget home, na kuimbishwa nyimbo za ajabuajabu, watoto wao wako shule huko uk. wa kwetu shule za kata na teacher mojo.

  Jamani hii serikali natamani dunia iishe tu, sasa hivi wamekuja na sera ya kiswahili iwe lugha ya kufundishia kuanzia primary hadi university, lakini watoto wao wanasoma nje kwa kiingereza ili waje kuwa viongozi baadaye, kwani inafaa kuwa rais wanchi wakati hujua kiingereza, marekani wanaongea kiswahili, china je, japan, uk, sasautawezaje kwenda nje kuomba misaada bwana, je wawekezaji wakija utaongeaje nao tayari kigezo tosha ya kukunyima uongozi na shule yako ya kata, chuo kikuuchako cha kiswahili, chali! unalakusema,

  hakuna kuuza vinyago, wala tingatinga barabarani kwa wazungu watakuja kuuza wakenya, sisi tudumishe lugha, kama si upungufu wa akili nini! kunanchi gani duniani ambayo uchumi wake umekuzwa kwa uimara wa lugha? eti wanatoa mifano ya china,japan, ufaransa, unafikiri siri iko kwenye lugha! nenda marekani kanunue kitu kimeandikwa made in china, nenda ujerumani wanatunia kijerumani lakini bidhaa nyingi sokoni vimeandikwa made in china nenda ufaransa, wanatumia lugha yao lakini bidhaa made in china, kunafaida ya lugha tuache mambo ya kutengeneza hoja ambazo hazitusaidii, leo tuende kubadilisha taarifa za vitabu mbalimbali viwe kiswahili, hizo garama si tungejenga maabara kwenye shule za sekondari na vyuo.

  wale watu wanafundisha wanao technologia tangia wakiwa primary tena kwa vitendo, na shule zina waalimu wa kutosha na maabara za kutosha,
  huku kwetu mwanafunzi anapigishwa theory nyingi ambazo hazina hatamsaada, anaambiwa microscope inatumika kuangalia vitu vidogo vionekane vikubwa, hapo ni shule ya msingi, hajaona microscope, secondary, anaendelea nayo microscope is an instrument or device which is used to magnify smallest things to be seen larger, form four hapo, atakwenda form five and six, bado hajaona microscope kwa sababu shule haina vifaa wala maabara ya kufundishia ataona wapi, akienda chuo kikuu tena cha afya au labda ya kilimo na mifugo ndo atakuja kukiona, anaanza kushangaa kumbe kitu nilichokuwa nakisoma ndicho hichi bwana, sasa mpaka ajue matumizi yake parts zake miaka yake ya kozi tayari. anaondoka, wewe unategemea atakuja kufanya ugunduzi gani? halafu tunasingizia lugha, siyo lugha ni siasa chafu ambayo imewafunga watu wasione mbele,

  Watanzania tutabakia kucopy na ku pest vitu vya wazungu tusipo badilika,
  mwl nyerere alisema maendeleo ya nchi huletwa kwa siasa safi, elimu bora, bidii, na afya bora, sasa siasa ndo hii tena ya ving'ang'anizi utadhani hii nchi wamepewa urithi na mungu, elimu ndo hii imechakachuliwa hadi basi, mitaala inabadilishwa kila kukicha mpaka waalimu wenyewe wanashindwa kufundisha, afya ndio usiseme,msd imekuwa kituo cha upatu. sasa tutawezaje kupona tusipojali sera nzuri namna hii alioleta Dr Slaa. ya elimu bure, matibabu bure, treni ya umeme, vinawezekana kwa kuwa hakutakuwa naufisadi

  mungu akupe nini! wala usiumize sana akili ni rahisi, tarehe 31 mwombe muumba wako, nenda kwenye kitu cha karibu nawe, ili usichelewe kwenda kanisani, kama umeswali ijumaa usichelewe kwenye utafutaji wako wanao wakalala njaa, kama umesali jumamosi fanya vivyo hivyo, chukua kitambulisho chako, maana na amini wewe ni njanja hujakiuza, angalia picha za viongozi wako, tafakari kampeni zao, weka alama ya vema pale ambapo unaona vizazi vyako vitapona. hapo sikuamulii ila agalia mbali, make changes. mbarikiwe wapendwa.
   
 6. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi huu uhakika uwa mnaupata kutokana na data gani? unapoona chama cha upinzani hakina mikoa ambayo kina uhakika wa kushinda fahamu muda bado haujafika, na kwa ninachokiona on ground usijeshangaa Dr. Slaa asiposhinda ata kwenye wilaya mmoja.
   
Loading...