Miaka mingine mitano ya maumivu!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Kama JK ataapishwa kesho kuwa rais wetu, tutashudia safari ya kwanza kwenda US kutalii na safari nyingine nyingi zitafuatia ili kufidia zile ambazo hakusafiri wakati wa kampeni! Atatumia zaidi ya tsh 2bn/- kutoa semina elekezi kwa wakuu wa wilaya na mikoa, nk. Kwa uzoefu tuliouona kwa miaka 5 iliyopita, tuhesabu maumivu mengine kwa miaka 5 ijayo! Au mnasemaje wandugu?
 
Kama JK ataapishwa kesho kuwa rais wetu, tutashudia safari ya kwanza kwenda US kutalii na safari nyingine nyingi zitafuatia ili kufidia zile ambazo hakusafiri wakati wa kampeni! Atatumia zaidi ya tsh 2bn/- kutoa semina elekezi kwa wakuu wa wilaya na mikoa, nk. Kwa uzoefu tuliouona kwa miaka 5 iliyopita, tuhesabu maumivu mengine kwa miaka 5 ijayo? Au mnasemaje wandugu?
Wanafunzi wataendelea kukaa chini, hao ni wale waliobahatisha kuwa na ada. Wagonjwa watakosa dawa, madaktari, baranara mbovu, bei za vyakula, nauli etc juu. Wakati huo huo t shirts za ccm, kanga na kofia zitakuwa zimechakaa na shs, 5000 za kuhamasishwa zilishaisha siku ile ile. Du, hali ni ngumu jamani.
 
sorry, kwenye title ni "maumivu" badala ya "mamivu!" Mod nisaidieni kurekebisha title!
 
Tutegemee matumizi mabaya hata zaidi ya fedha za umma kwani ni lala salama ya mafisadi kuhakikisha wanarudisha fedha walizozipoteza kwenye kampeni na kuvuna zaidi na zaid. Pia tutegemee kuongezeka kwa idara nyingi sana serikarini lengo likiwa ni kuhakikisha fedha zinachotwa sana, hiyo ikiandamana na kuongezeka kwa kodi katika vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na PAYE huku makampuni mbalimbali yakisamehewa kodi bila msingi maalumu. Nidhamu katika matumizi ya fedha ndio itaisha kabisaa na kusababisha mfumuko wa bei za bidhaa zote mara tatu zaidi na dola itauzwa zaidi ya 5000/= by the end of those 5yrs. Na tuwemo....
 
Hela zote zilizotumika kuweka mabango nchi nzima lazima zirudi zote kabla ya kuanza kufikiria masuala ya Maendeleo. Hali ya umaskini lazima itaongezeka zaidi ya ilivyo sasa. inflation itaongezeka n.k

Watz, fungeni mkanda zaidi.

:puke:
 
kwanza kitu cha kwanza mwaka mmoja utakuwa wa kurudisha hea zao walizohonga na kununulia matshirt na makofia thena baada ya hapo utajaza mwenyewe
 
kama tukiamua kufanya zile hesabu rahisi za cross multiplication utagundua ukweli huo, sema kwa mfano: kama sukari mwaka 2005 ilikuwa sh.600 mpaka 2010 imefika sh 1600-200, je kwa miaka mingine 5 itakuwa saw na shilingi ngapi? ukifanya hivyo kwa kila bidhaa utagundua nyakati ngumu zijazo. Jadili yafuatyo pia ili ujiridhishe, mosi, kwamaba huu ni muhula wa mwisho wa mkuu wa kaya, je unafikiri atafanya kazi ipasavyo huku akijua fika anaondoka madarakani na hatarajii tena kugombania nafasi hiyo? maisha yatakuwaje? Naam, nasikia kwa mbali sauti za huzuni, mateso na machungu, naona kwa mbali nuru ikitiwa giza, naona maisha magumu, na kila mmoja anajitahidi kujishibisha kwa punje za mtama na makombo ya wale waketio madhabahuni na kugawana keti ya taifa. Sioni dalili za kuwepo na amani, upendo unafifia, naona rushwa kubwa kubwa zinaongezeka, nayaona mateso meni kuliko wakati mwingine wowote, watu wanajitahidi kuitafuta kesho yao, lahasha haipatikani, manabii wanakatatiliwa na hawana nafasi tena. Kila mwenye nguvu anachukua chake mapema na kuondoka hatimaye nchi inaabaki tupu. Hee kumbe nilikuwa naota tu. Haya waungwana.
 
Bei ya petroli na dizeli itafika sh 2000 kwa lita kabla ya mwaka mpya 2011. Kisingizio itakua kama kawaida kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia. Kwa hiyo nauli za mabasi zitapanda na mfumuko wabei utaongezeka. Umaskini utaongezeka na watu watazidi kukata tamaa ya maisha bora!
 
Ni miaka ya matanuzi ya kufa mtu kwa Mkwere and the company; kwa sisi wengine ni maumivu kwa kwenda mbele.

Pamoja na maumivu tutakayopata, ni marufuku kukata tamaa. Tutapigana mpaka utawala wa haki Tz upatikane.
 
Hela zote zilizotumika kuweka mabango nchi nzima lazima zirudi zote kabla ya kuanza kufikiria masuala ya Maendeleo. Hali ya umaskini lazima itaongezeka zaidi ya ilivyo sasa. inflation itaongezeka n.k

Watz, fungeni mkanda zaidi.

:puke:
Ndege ipo tayari kupaa, ni kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi, sijui kuelekea wapi? Mungu utusaidiye ndg zetu Albino wasije wakacharangwa mapanga ndani ya hii miaka mitano.
 
Bei ya petroli na dizeli itafika sh 2000 kwa lita kabla ya mwaka mpya 2011. Kisingizio itakua kama kawaida kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia. Kwa hiyo nauli za mabasi zitapanda na mfumuko wabei utaongezeka. Umaskini utaongezeka na watu watazidi kukata tamaa ya maisha bora!
Zimekwisha anza kupaa hata kabla zoezi la kuhesabu na kujumlisha (kiana) kura halijamalizika.
 
hana wa kumuuliza 2015 amefanya nini kwenye ahadi kedekede na magirini alizowadanganya wadanganyika
 
Ni kipindi ambacho tutamkumbuka Nyerere zaidi kuliko vipindi vyote na watu watalishuhudia hili machoni mwao na mioyoni mwao!! Maana alisema kijana bado hajakomaa na haitatokea kwamba atakomaa tena...!!
 
na asisaha kwenda CHINA wall kutalii.....sisi tutabaki kula majani na wala si nyasi..coz nyasi tulikula wakati wa mkapa ili kununua ndege
 
Back
Top Bottom