Miaka mingi bila kupata mtoto: Dada ajutia dhambi alomtendea mpenziwe wa awali!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Kuna dada alikuwa akisoma SUA miaka ya 2000 mwanzoni. Kwa bahati alikuwa na mahusiano na Mhadhiri mnyarwanda pale SUA. Akiwa ktk mahusiano hayo, kama kawaida, akajenga uhusiano na mwanafunzi mwezake wa kiume mwanafunzi huku mhadhiro akiaminishwa kuwa huyo mvulana alikuwa na undugu wa damu na huyo mdada. Mnyarwanda wa watu akawa anaamini kuwa jamaa ni ndugu wa mchumbake.

Mwanamke alihudumiwa kwa kila jambo na wengi walimuonea gere kwa jinsi alivyompata mnyarwanda aliyejua kupenda kweli kweli. Masikini mdada aliandaliwa bonge la sherehe siku ya mahafali ambayo kweli ilifana sana, na siku hiyo Mnyarwanda wa watu aliweka mambo hadharani na kukiri kuwa amepata mtu wa kumtunza. Ikumbukwe jamaa wakati wa genocide, alipoteza mke na watoto wake wote kwa kuuwawa. Kifupi jamaa aliishi maisha ya upweke sana baada ya kuhamia bongo na kuja kufundisha SUA.

Ajabu baada ya graduation na kwenda kwao, msichana hakurudi tena morogoro kwa mchumbake, na akaolewa juu kwa juu bila Lecturer kujua. Masikini huyo mhadhiri alipokuja kujua kuwa huyo mchumake kaolewa, ilikuwa ni kama kapata pigo lingine. Tumjuao tulihisi huenda jamaa angefikwa na umauti maana alibadilika kabisa na kuwa kama dhaifu kiafya kama mgonjwa vile. Aliumia zaidi kujua kuwa aliyemuoa mke wake mtarajiwa ni yule kijana aliyekuwa akija nyumbani kwake huku yeye akijua kuwa ni kaka wa mchumba wake.

Mungu si Athumani, Kagame alimteua yule Mwalimu kwenda kuwa waziri kwao Rwanda na maisha yake yamebadilika na kuwa mazuri kwani baada ya kuoa jamaa akapata watoto na amesahau ubaya alofanyiwa na dada wa kibongo. Taabu sasa ni huku kwa huyu mdada, ambaye pamoja na kujua kuwa mtu alomfanyia unyama kafanikiwa kimaisha tena kawa Waziri-siku alipojua alijisikia vibaya-, yeye sasa yuko kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7, bado hajapata mtoto pamoja na juhudi a kuhangaika mahospitalini. Imefika mahali huyu dada anahisi kwamba pengine ni laana ya Mungu kutokana na ubaya alomfanyia mtu ambaye alikuwa na mapenzi ya dhati kwake.

Siku moja wakati naongea naye kimtego mtego nikamuuliza watoto wanasemaje. Ilikuwa kama nimemtonesha kidonda, kwani alikosa raha na kusema hajabahatika kupata mtoto na kwamba anahisi kama ana mkosi. Nilipomuuliza mkosi kivipi akasema anahisi yule mnyarwanda kamroga au ni adhabu ya Mungu kwa kumkosea sana Mnyarwanda. Na pia mumewe kisha zaa nje baada ya kuona hakuna matunda ktk ndoa yao. Nikaamua kumtania vp kama mnyarwanda akiamua kurudisha majeshi? Akajibu tuko radhi kumkubalia kwani ndoa yake ya sasa ni kero tupu, eti ni heri angeolewa na mnyarwanda hata kama angekosa mtoto angekuwa na furaha ya mapenzi na maisha pia.

My take: Jamani tusipende kuhusisha matukio mabaya tunayokumbana nayo maishani mwetu na watu ambao tumewafanyia ubaya. Inawezekana ikawa ni laana ya Mungu au ni mapito tu ya kawaida ktk maisha. Ila tukumbuke ubaya haulipi na wema hauozi kamwe.
 
na stres pia inachangia.......lakini imejionyesha wazi kuwa kakanyaga mavi. maana jamaa keshazaa (I mean zalisha) nje!

Pole Edson, naamini mungu alishayaponya majeraha yako!
 
na stres pia inachangia.......lakini imejionyesha wazi kuwa kakanyaga mavi. maana jamaa keshazaa (I mean zalisha) nje!

Pole Edson, naamini mungu alishayaponya majeraha yako!

Ndo hapo sasa
Atajikuta hana laana yoyote sana sana yeye ndo mwenye matatizo kama jamaaa yake kashapata mtoto nje
Mambo mengine tunajitafutia wenyewe halafu tunabaki tunasema laana sijui kulogwa
 
hamna noma naona unatupiga madongo wasabato

Mtumeeeeeeeeeee! Mkuu umemaliza lini aiseee, maana niliogopa kutaja religious denomination! Mhhhhhhh kweli hakuna unaloweza liongea humu ikapita bila kupata mtu anayelijua. Umesomeka mkuu ila hukupaswa kutamka imani husika
 
na stres pia inachangia.......lakini imejionyesha wazi kuwa kakanyaga mavi. maana jamaa keshazaa (I mean zalisha) nje!

Pole Edson, naamini mungu alishayaponya majeraha yako!
edson ndio huyo kaka aliempora mnyarwanda shori? aiseeee ila alifanya sio vema.....
 
Kuna watu hawajui kusimamia wanayotaka..wanasukumwa na upepo kushoto na kulia utadhani ni bendera. Mwisho wa siku mtu anayefanikiwa ni yule anayeweza kusema yes au no come rain, come sun.
 
Watafute tiba kwani kuna uwezekano mmoja wao akawa mgonjwa.
OTIS
 
Mtumeeeeeeeeeee! Mkuu umemaliza lini aiseee, maana niliogopa kutaja religious denomination! Mhhhhhhh kweli hakuna unaloweza liongea humu ikapita bila kupata mtu anayelijua. Umesomeka mkuu ila hukupaswa kutamka imani husika

wewe ndio hukupaswa kuandika sentensi hii " hadi wasabato wenziwe walimuonea gere" hapo juu !
 
Hili ni funzo linaloendelea usije kushangaa baada ya wiki anakuja mtu hapa kuomba ushauri kwa ujinga kama huu alioufanya huyo mdada
 
Amtafute Mnyirwanda amuombe msamaha ili aiweke roho yake huru. Uwezekano mkubwa ni laana kutoka kwa huyo aliyemfanyia huwo ubaya. Alitakiwa kutubu mapema sana ila kwa kuwa na roho ngumu ameacha mpaka Mume wake amezaa nje au tunaweza kusema ameoa mke wa kumzalia watoto. Asipotubu anaweza asizae kabisa mayai yake yamekuwa kama ya kuku wa mayai asiyekuwa na jogoo.
 
Back
Top Bottom