Miaka michache ijayo (kama 5 hadi 10) hakutakuwa na wakala wa M-Pesa tena

Wakuu dunia inaenda kasi ile mbaya mno, na teknolojia ya sasa inaenda kwa speed ya kutisha na watu hawalali wakiwaza jinsi ya kuleta mambo ya teknolojia.

Back to the Point, miaka kama 15 nyuma hakukuwa na hii kitu inaitwa M-Pesa na ukisoma taarifa za Safaricom ambao ndio wamiliki wa M-Pesa wanakuambia walipata shida mno siku za mwanzo kuendesha biashara ya M-Pesa.

Tanzania mtakumbuka wakati inaaza M-Pesa pia hakuna aliyekuwa anaimini na wengi waliona kama utapeli fulani au watapoteza pesa zao.

Leo hii M-Pesa inafanya transaction za trilion kwa siku tu. M-Pesa kwa sasa sio ishu tena.

Ishu ni nini?

Kwa sasa M-Pesa inahama kutoka mambo ya tuma pesa katoe kwa wakala na tumia na kwa sasa inaenda kwenye kutumia Mpesa kwa manunuzi.

Kwamba hutahitajika kutoa pesa kwa wakala ili ukanunue kitu, hutahitajika kwenda kutafuta wakala yuko wapi ili utoe pesa na uzitumie.

Rejeeni MPESA Mastercard.

Tunaelekea kwenye cashless kwa sasa mambo ya kutembea na waleti imetuna pesa yatapotea.

Dunia inaenda speed sana.

So hawa mawakala ni suala la muda tu kabla hawajawa outdated kabisa. Mambo yanaenda speed sana na ukizembea unaachwa nyuma.
Hata ikipotea Mimi nimeshazoea kutembea na pochi iliotuna unaweza ukadhani Nina ulemavu wa tako
 
Kuna Mabadiliko mengine, sio wote watafikiwa mkuu , kina wengine hupitwa na baadhi ya stage, Zamani kulikuwa na Typewriter, Zilikuwa sehemu chache sana, Ila leo hii Computer ziko sehemu ambazo hizo typewriter hazikuwahi kufika, mifano ni mingi, so sio lazima Benki ziwe nchi nzima au kila kijiji, hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah mkuu nalielewa hilo ujue mabadiliko hayo mpaka yafikue kuiafect jamii yanatakiwa ya take place in majority,.. sasa point yangu narud kua mpka majority iwe hvo inahitaji muda ukizingatia sisi ni "ELEMENTARY COUNTRY" kama alivosema magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii
Hii kitu nimeiona kwa I&M bank...Kuna kitu wanaita SPENN account! Lengo ni kuhamasisha cashless transactions inakuwa kama M Lipa, ni kama Mpesa tu ila yenyewe pesa unatolea Bank bure kabisa ila kupitia kwa wakala utakatwa 1% ya pesa unayotoa.

Hii ipoje kwn app yao tyr nshaipakuw, tatizo linakuja kwny kuweka salio ili nifanue miamala na mm nipo kibaha
 
Atm nazo zitakufa
ATM wazungu wamezilinda, m pesa tu ingeweza kuzitoa ila serikali imegoma kutumua full m pesa teknology. Pesa ingegunduliwa ulaya ingekuwa next level ila kwa sababu in muafrika basis haina nafasi.

Safari com wanatakiwa waende next level vinginevyo watatolewa kwenye biashara..Safar com wanatakiwa wasisitize transaction za on line au gsm teknology wasisubiri kutolewa sokoni.
 
Ko hatakama mtu nimenunua vitumbua au mihogo kwa mama ntilie,mchicha soko mjinga ntalipa kwa njia ya mtandao?
Lakini pia Bado hujanishawishi kwenye kuweka hiyo float
Wewe wala hushawishiwi,ila mabadiliko yanakulazimisha utake usitake
 
Hakuna kutoa wala kudepost mkuu.
Kwaio kwa mfano nna watu wawili wa kuwalipa, katika akaunti kuna milioni moja, na kila mmoja ananidai milioni 1, nikimlipa mmoja manake akaunti itakuwa zero, sasa pesa nyengine nitaweka vipi kwenye M-pesa ili nimtumie na huyo mwenigne?
 
Sasa Kama hujaenda kwa wakala ili azibadilishe hizo hela zako katika mfumo wa kielectronic na kukuwekea kwenye simu yako hayo manunuzi utayafanya vipi? Au hayo malipo utayafanya vipi?
Na bado hatujazungumzia swala la maeneo ya vijijini na miji midogo ambazo hizi huduma za kibenki hazijafika bado
 
Muda si mrefu nilikuwa natumia simbanking app ya crdb nikakutana na kitu wanaita mVISA, kweli mambo yanabadilika kwa kasi sana.
Walikuwa wanaringa sana kipindi cha nyuma kuhusu malipo ya mtandaoni. Leo hii wanaanza kuchukua hatua baada ya kuona bank kama equity, exim, na wengineo wameanzisha huduma ya malipo ya mtandaoni kwa urahisi....
 
Sasa Kama hujaenda kwa wakala ili azibadilishe hizo hela zako katika mfumo wa kielectronic na kukuwekea kwenye simu yako hayo manunuzi utayafanya vipi? Au hayo malipo utayafanya vipi?
Huyu jamaa ni boya sana...amefikiria upande mmoja tu wa kutoa siyo kuweka
 
Hivi mnajua kuwa mpaka leo kuna watu wanarushiwa vifurushi vya simu?? achana na huko kwenye mpesa... hzo zote ztakuwa ni dar, na mijini tu na sio vijijini.
 
Hivi mnajua kuwa mpaka leo kuna watu wanarushiwa vifurushi vya simu?? achana na huko kwenye mpesa... hzo zote ztakuwa ni dar, na mijini tu na sio vijijini.
Mimi niliwahi kufikiri baada ya ujio wa MPESA na wenzake mauzo ya vocha yatapungua sana kama sio kwisha, hadi leo hii miaka zaidi ya 10 ya huduma hizi still vocha zinaenda sana. Dunia inaenda kasi ndio, ila waafrica tuko slow, sivyo kama anavyofikiri mtoa mada
 
Vocha zinapotea sana niliona Kenya Mitandao ina plan ya kusiisha kabisa Vocha, nchi kama Rwanda walisha sitisha vocha,
Hata Bongo wanao nunua vocha kwa mpesa wanaongezeka sana, itakuwepo ila inapotea.

Pia kununua vocha kwa mpesa kumeanza juzijuzi tu haikuwepo hii huduma
Mimi niliwahi kufikiri baada ya ujio wa MPESA na wenzake mauzo ya vocha yatapungua sana kama sio kwisha, hadi leo hii miaka zaidi ya 10 ya huduma hizi still vocha zinaenda sana. Dunia inaenda kasi ndio, ila waafrica tuko slow, sivyo kama anavyofikiri mtoa mada
 
Back
Top Bottom