Miaka michache ijayo Arusha inaenda kuwa na kizazi cha tofauti nchi nzima

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,847
15,252
Kumekuwa na idadi kubwa ya kila aina ya vilevi, ugoro, gundi, pombe, nyingine wanzalishia majumbani. Na wala hata hazina vibali vyovyote.

Hali hii nayo inachangiwa na ongezeko kubwa la vijana wa kike na wakiume wanaotumia pombe kali yoyote waionayo. Waliopo mkoa huu nafikiri wanajionea wenyewe hali halisi ya wakazi wake, wake kwa waume.

Idadi ya Matomboy inazidi kuongezeka Yan mabinti nao wanaojifanya wanaume hii ni hatari maana kuna kitu kinajizalisha hapa, na hii imechangiwa na kuchanganya vitu vingi huko vichwani kama ugoro, mirungi, sigara kubwa. hapa siandiki zaidi kila mtu mwenye kufahamu na anafahamu.

Hata kwenye maongezi yao unashindwa elewa wanaongea nini maana maneno yao hayapo kwenye lugha yoyote ile.

Unakuta binti au mwanamama anakatia majani tena siku hizi wanaita nyama ya stake (inatoka Kenya) wanakuambia bila hili goma hailali halafu huku anashushia na mabapa kadhaa hadi mtu unafumba macho.

Na kawaida sana hapa ndani ya familia kuibiana yani baba anamuibia mama hela au vitu vya thamani ndani na kwenda kuviuza ili akanywe na kutengeneza mazingira kuwa ni wezi na hivyo hivyo kwa upande wa Wakina mama kuibia waume zao Watoto ndo hivyo hivyo.

Vijana na wenyewe wameishia kwenye pombe kali hawasikii konyagi wala Kvant wanasema hayo ni maji ya kunywa wanaona bora gongo kwa madai eti ndo inastimulate haraka na yale majani mengine.

Sigara imebaki kwa wazee tu na wamama. Vijana wao wanadili na sigara kubwa tena wanakuambia hiyo ni dawa ya maisha ukipiga hiyo hakuna kufa.

Vijana hawa wanaona maisha ni kutumia vilevi vya aina yote tena huku wakiwafundisha watoto wadogo kunywa pombe wengine wakiamini hakuna kufa.
 
Vijana wa Dar na Arusha sio taifa la kesho.
Ukute kasokota dreads, boda/toyo haina side mirror, haina Number plate, Imekunjwa usukani. Kaa nao mbali hao machalii.

Meno meusi tii ajili ya ugoro na Mirungi
FB_IMG_16496941492540540.jpg
 
Hapa tunakupinga boss, vijana wa chuga wagumu kinoma noma
Na ndio hapo mnapo zugiwa na kujifanya wao wagumu, njoo ujionee ktk kumbi za starehe... Na ukiona kijana wa kiume yupo na mgeni observe utaona... Arusha ilikua enzi hizo hawa vijana wa sikuhiz ni 🏳️‍🌈🏳️‍🌈🏳️‍🌈 hadi sio poa
 
Back
Top Bottom