Miaka kumi ijayo ni michache sana utajivunia nini?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
MIAKA KUMI IJAYO
NI MICHACHE SANA UTAJIVUNIA NINI?

Miaka kumi ijayo hutajivunia ni kwa haraka kiasi gani ulikuwa unajibu jumbe za simu unazotumiwa, au kupokea kila simu iliyokuwa inapigwa.

Miaka kumi ijayo hutajivunia ulikuwa kwenye makundi mangapi ya whatsaap, huenda hata kipindi hiko isiwepo kabisa...

Miaka kumi ijayo hutajivunia ni mitandao mingapi ya kijamii umetumia, na ipi mipya uliwahi kuingia haraka...

Miaka kumi ijayo hutajivunia ni habari kiasi gani umefuatilia, umejua kila kinachotokea, nani kamuua nani, au kambaka nani...

Miaka kumi ijayo hutajivunia kujua maisha ya wasanii yameendaje, nani anatembea na nani, na msanii gani analipwa sana.

Miaka kumi ijayo hutajivunia round za bia ulizozungusha, ulipokuwa na marafiki kwenye baa.

Miaka kumi ijayo hutajivunia kuwa shabiki namba moja wa timu fulani, au kwa jinsi gani kocha wa timu unayoshabikia alivyokuudhi...

Miaka kumi ijayo utajivunia ni kitu gani kikubwa umefanya kwenye maisha yako, kinachokunufaisha wewe na wanaokuzunguka pia.

Miaka kumi ijayo utajivunia biashara uliyoanza, na wengi wakasema huwezi, lakini ukapambana na hatimaye kusimamisha biashara imara.

Miaka kumi ijayo utajivunia kufanyia kazi kipaji chako, iwe ni mchezo, uandishi, kuigiza au chochote na ukafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.

Miaka kumi ijayo utajivunia kwa kuona maisha yako yamekuwa bora zaidi, umeondoka kwenye utegemezi wa chanzo kimoja na madeni na umeweza kutengeneza vyanzo vingi vya kipato.

Sikukatazi kwamba usifanye mambo ambayo yanakupa starehe, bali nakukumbusha kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwako, ambayo yatafanya maisha yako na ya wanaokuzunguka kuwa bora zaidi.

Na pia nikukumbushe miaka kumi ijayo siyo mingi kama unavyofikiri, kumbuka Raisi Kikwete aliingia madarakani lini na sasa ameshatoka,
Je unaweza kujilinganisha hali yako ya maisha wakati anaingia na wakati anatoka?

Miaka kumi ni michache sana,
AMKA sasa na weka juhudi kuboresha maisha yako.
 
Well said
 
Mkuu huwezi kupumzika kuandika mada, kila siku mada zaidi ya 10, pata muda wa kupumzika basi usome na za wenzako.
 
Umenigusa sanaa kwa ujumbe huu, wazembe lazima wapite kuponda
 
Kizazi cha Instagram na WhatsApp hawataelewa hili let alone kusoma hili bandiko
 
Back
Top Bottom