Miaka Ishirini tangu Kutungwa Sheria ya Kuruhusu Vyama Vingi: Bado Upinzani ni sawa na Uadui! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka Ishirini tangu Kutungwa Sheria ya Kuruhusu Vyama Vingi: Bado Upinzani ni sawa na Uadui!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jul 2, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Tarehe kama ya leo miaka 20 iliyopita, yaani tarehe 2 Julai, 1992, Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya kuruhusu kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

  Miaka 20 imetimu, tumepiga hatua, lakini, mpaka hii leo, bado upinzani kwa wengine unatafsiriwa kama ni uadui, na wakati mwingine ni uhaini.

  Na katika Tanzania yetu, wenye fikra za kukipinga Chama tawala, CCM na Serikali wamekuwa wakitengwa na hata kupewa majina mabaya. Nimeshawahi kumsikia mtu akiambiwa;

  "Alaa, unaongea na Lipinzani hilo!" Kana kwamba aliyeitwa ' Lipinzani' hakuwa Mtanzania na binadamu kama wengine.

  Na hakika, katika kujadili hili la Katiba Mpya, tuna kila sababu ya kuipitia historia yetu. Maana, naamini, kuwa historia ni mwalimu mzuri.

  Itakumbukwa, katikati ya vuguvugu lile la mageuzi ya kisiasa miaka ya 90 mwanzoni, Watanzania zikatufikia habari; kuwa Oscar Kambona, aliyekosana na Nyerere na aliyekimbila uhamishoni Uingereza, alikuwa njiani kurudi nyumbani. Ujio wa Oscar Kambona ukawa gumzo la mjini na nje ya jiji. Kuna waliojiandaa kwenda uwanjani kumpokea.

  Usiku mmoja ikasikika sauti ya Bw. Mrema redioni. Sauti ya Waziri wa Mambo ya Ndani. Mrema alitamka, kuwa kama Kambona angekanyaga mguu wake Dar es Salaam, basi, angekamatwa kujibu mashtaka ya uhaini.

  Ni hofu ile ile ya Serikali hata wakati huo. Hofu ya kuimarika kwa fikra za upinzani na kukua kwa upinzani. Mrema akatumika au akajituma kuwatisha na kuwakatisha tamaa Watanzania. Kambona alikanyaga Dar, hakuwa na mashtaka ya kujibu. Ulikuwa ' mkwara' tu, kama wanavyosema mitaani.

  Na Mrema, akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, aliifanya kweli kazi ya kuwa ' Mbwa wa Serikali'. Alibwaka kweli kweli. Nakumbuka usiku mmoja mwanzoni mwa miaka ya tisini nilimsikia Mrema akiongea redioni kutishia maandamano ya CUF. Maandamano yale yalikuwa yahitimishwe kwa mkutano viwanja vya Mnazi Mmoja. Mwenyekiti wa CUF, Bw. James Mapalala ndiye alikuwa aongoze maandamano hayo na kuhutubia.

  Augustino Lyatonga Mrema akaaunguruma redioni usiku ule. Alishusha ' mkwara' mzito. Kuwa maandamano hayo si halali na yangekutana na nguvu za dola. Kesho yake, CUF waliingia mitaani. Ndio, Ungangari wa CUF ulianza siku nyingi.

  Pale Mnazi mmoja FFU wakamwagwa, na farasi wao pia. Virungu vilitembea. James Mapalala, Mwenyekiti wa CUF, hakuonekana. Kukawa na taarifa, kuwa anatafutwa na polisi.

  Dar ilikuwa ndogo wakati huo, lakini James Mapalala hakupatikana .
  Ninazo taarifa za kuaminika za Kibalozi, kuwa James Mapalala alikuwa amejificha kwenye moja ya makazi ya rafiki yake, balozi wa nchi moja ya Kimagharibi. Ni balozi gani huyo? Na nini hasa kilitokea miaka 20 iliyopita?

  James Mapalala yungali hai. Huu ni wakati kwa waandishi vijana kuwatafuta wazee veterani wa harakati za mageuzi ya kisiasa hapa nchini. Wazee kama akina James Mapalala.

  Hawa ni watu muhimu sana watakaotusaidia kupokea simulizi zao. Kisha ziwekwe kwenye maandishi, na iwe kumbukumbu za kihistoria. Ni historia yetu, tusiionee aibu. Ni urithi tutakaowaachia wajukuu zetu ili nao waweze kujifunza. Waweze kujitambua na kujenga mioyo ya uzalendo.

  Maggid Mjengwa,
  Barcelona, Spain
  Mjengwa Blog
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakupa hongera kwa kuwa na mapumziko katika nchi ambayo jana tu imetwaa ubingwa wa kombe la Ulaya-Soka! Umekumbusha jambo muhimu na ni jukumu la wanataaluma wetu kuingia kazini ili kuto wigo wa vijana wa sasa kujua magumu ambayo siasa yetu imepitia.
   
 3. T

  TUMY JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu uliyosema ni kweli kabisa huku kwetu upinzani ni uadui jambo ambalo hata mimi linanishangaza sana, wenye dola wameshindwa kuelewa kwamba lengo la upinzani ni kuwapa changamoto na kuwafanya wawe amini zaidi katika utendaji kazi upinzani ni kama watchdog na si uadui kama ilivyo sasa, tumeshuhudia positive criticism kutoka kwa wabunge wa upinzani ila kwa kuwa tu ni wa upinzani basi wamekuwa wakipuuzwa na kutukanwa na kwa namna hii nchi hii haiwezi kuendelea watu wameweka mbele tamaa binafsi na si kutaka leta maendeleo.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sisi tulikurupuka tu na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kujiandaa. Ilitakiwa tuingie kwenye huo mfumo tukiwa tayari tuna katiba mpya kabisa lakini hatukufanya hivyo.

  Tulichofanya ni kuwekea viraka katiba ambayo kwa ujumla wake haiendani na mazingira ya vyama vingi. Sasa miaka 20 baadaye ndiyo tunaona kumbe kuna ulazima wa katiba mpya.

  Ina maana kweli hatulijua hilo wakati tunaingia kwenye huo mfumo? Hatujitambui kabisa sisi.
   
 5. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa hali inavyoendelea Bungeni ni dhairi kabisa CCM hawajakubali kwa nia ya dhati uwepo wa vyama vingi.
  Si ajabu Kiongozi wa Bunge kuchukua muda mrefu kumtetea mbunge wa CCM hata kama anatukana na kutoa kashfa kwa sababu tu wapo chama kimoja. Ni aibu sana kwa Taifa hili. "No Separation of Power !!". Serikali = Chama = Mahakama = Bunge.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Umeonekana na sasa utakomaa japo kunakuwa na hujuma kibao za hawa waioko madarakani
   
Loading...