busara kwanza
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 239
- 109
Kwanza tayar unamafanikio bro usilinganishe wewe na mwingine kuwa weweKiukweli kadri siku zinavyozidi kwenda nakata tamaa
Naona mambo yangu hayaendi sawa kabisa japo nimesoma na najishughulisha ila hali ngumu sana
Mi ni kijana mwenye miaka 31 Nina elimu ngazi ya PGDE ambayo ipo mbele ya Bachelor
Tangu nimalize bachelor na hiyo PGDE ni mwaka wa 6 sasa sina dili la kueleweka la kupata fedha za kutosha kuendesha Maisha
Najishughulisha na kazi katika private sector flani inayotoa elimu lakini salary ndogo,nimejaribu kuomba kazi Maeneo mbalimbali kuanzia serikali na taasisi binafsi but sijafanikiwa
Hela ninayopata ni ya kuunga unga sana
Nikiwaangalia baadhi ya wenzangu wengi niliosoma nao wamefanikiwa kimaisha na sasa najiuliza mi nafail wapi mbona najishighulisha sana ingawa kipato ninachopata ni kidogo
Sina mtaji labda ningeweza kufanya biashara
Nifanyaje wakuu nitoboe naona umri unazidi kwenda na Nina watoto wawili wanalelewa na mama yao ambaye ni mwajiriwa ,nikiwaza kuhusu watoto wangu na sioni mwanga wa mafanikio hadi sasa najiuliza wataishi vipi wanangu,hata kama mama yao ana hela za kuwahudumia ila najiskia vibaya kutowapa msaada mkubwa kama baba,niliwapata kipindi nasoma hela ilikiwepo ya boom na bahati nzuri mama mtoto nae alipata kazi mapema ,nifanyaje wakuu nitoboe??
Sent using Jamii Forums mobile app