Miaka inaenda sioni Future yangu. Nimekata tamaa!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,032
50,940
MIAKA IMEENDA SIONI FUTURE YANGU; NIMEKATA TAMAA!

Kwa Mkono wa Robert Heriel.

"Nina miaka 33, sina mke, sina mtoto, sina kiwanja, Kodi inanishinda, wala sio Kodi nyingi haifiki hata elfu 50 Kwa mwezi lakini inanitoa jasho kuilipa, chakula nakula Kwa mbinde Kama mvuta upinde. Mavazi yangu ni duni, sikutegemea mambo yawe hivi, tangu nikiwa Chuo nilifikiri ningefanikiwa mapema mara tuu nitakapomaliza shule. Lakini mambo yamekuwa mbali mno na matarajio yangu. Nikikuambia naendelea na mapambano ninakudanganya, nimekata matumaini.

Ona Mimi sio WA kukosa hata hela ya kununulia Dawa ya Meno, ona! Mimi sio WA kukosa sabuni ya kuogea na kufulia hata marapurapu ninayoyavaa! Ona! Mimi sio huyu! Labda Mimi wamenibadilishia. Mimi wakula mlo mmoja kweli!

Hapa sina pakwenda! Kodi nadaiwa miezi mitatu sasa. Mwenye nyumba kanipa notisi kesho kutwa nafurumushwa hapa. Loooh!!

Labda ungefikiri nilimuasi Mungu Kwa kutokwenda kwenye nyumba zake za ibada, lakini sivyo. Nilikuwa Muumini mwaminifu hapo awali kabla sijageuka muasi, uasi uliosababishwa na mambo yangu mengi kwenda mrama huku watumishi wakinitoza kila nifikapo kwenye nyumba za Ibada. Nikaasi nikasema kumbe kuabudu Napo ni mpaka ulipie. Nikaacha kwenda huu mwaka wa Saba sasa.

Nataka kuoa lakini Nani akubali Hali yangu dhalili na fukara. Wanawake wote wa mjini hutaka maisha ya magari, urembo na majumba ya kifahari. Nitawawezea wapi.

Usifikiri kuwa nilizembea kwenda huko vijijini, nilifika mpaka Makanya huko, nikateremkia Saidong mpaka Hanang huko ndani ndani, nikapandisha mpaka vijiji vya Singida mpaka nilipojikuta Kibati huko Turiani Morogoro, kote huko kutafuta mwanamke wa kijijini, lakini niliambulia patupu.

Si ungenilaumu Kama sikufika kule kwenu Handeni, nilifika kote huko mpaka Lushoto nikapandisha milima ya shambalai kote huko licha ya kuwa na wasichana wazuri lakini kote walikatalia. Ati walihitaji mwanaume kwenye wadhifa na Mali walau Mbuzi wawili tuu. Nikawaza Mimi haya kuku mmoja sina sembuse Mbuzi. Loooh! Nikamkumbuka Paka wangu mzuri wa madoa doa niliyemfuga anikamatie panya na mende waliokuwa wakinisumbua humu ndani lakini Paka Yule Kwa hila akanikimbia akaenda Kwa jirani yangu huyo hapo nje mwenye Geti la rangi ya kijivu.

Paka Yule huenda alichoka Kula Mlo mmoja, kila siku Panya tuu na hata akikosa panya angekula Mende. Nani angekubali mlo mmoja miaka nenda Kula Milo mmoja. Hata Mimi huenda nisingekubali Kama kuna nafasi ya Kula minofu.

Siku hizi Paka wangu namuona juu ya kuta za jumba la jirani yangu. Hunitazama Kwa jicho la Dharau na mara huachia mlio wa dhihaka. Basi hasira hunipandaga sana, naokotaga jiwe ili nimpige lakini Paka Yule hata hashtuki kunikimbia. Aaargrrrrrrrhii! Sitaki Kueleza haya.

Ningetaka niwe mganga wa jadi, nipige Ramli chonganishi nijipatie kipato. Wazo hilo likanipeleka mpaka Pangani huko nikajifunze elimu ya uganga na uganguzi. Niliishia kutapeliwa na hata nilipohitaji Utajiri wakaishia kuugeuza mwili wangu uwanja wa viwembe, ninachale Mimi mpaka sehemu nyeti.
Nafikiri hata siku Mungu akinijalia mara paap nikatusua maisha na kuoa, huyo mwanamke ataniona Mimi ni mlozi niliyebobea haswa. Tena angeniona Mali zangu niza ndagu.

Haya tuachane na hayo!

Embu niambie Rafiki yangu utanisaidia nini maana mambo yangu yameniendea mrama. Macho haya ni mapambo tuu hayaoni mbele.
"

Akasema akinitazama!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Makanya, Kilimanjaro
 
Tatizo lako unapoteza muda mwingi kutafuta umaarufu hapa JF kwa kuandika makala zisizo na kichwa wala miguu. Jikite katika kutafuta hela, Achana kushindana na watu kama Erythrocyte au akina brazaj etc , wenzako wanalipwa na chadema!
 
Hahaha😁😁😁😁,Ile stor yako ya kula tunda kimasikhara ni very interesting 😁😁😁
 
badilisha reference yako ya mafanikio...je mafanikio yako unayapima kwa kuangalia kitu gani..ma padri awaoi ila wanaonekana poa wakiendesha ibada..watoto wa mitaani awana pa kulala ila goal yake apate msosi kwa siku..Pia tafuta purpose ya maisha yako unawezekana sio vyote unavyotamani au unavyotafuta..punguza speed ya maisha na kama mambo unayo yapa kipaumbele yanakuumiza yapunguze pia..ongea na waty ujue ni jinsi gani wanakabiliana na mamb yanayowasibu..sio ww tu unapitia mambo unayoyaita magumu...deal with your emotion and spiritual issues sababu yanajenga humanity
 
Tatizo lako unapoteza muda mwingi kutafuta umaarufu hapa JF kwa kuandika makala zisizo na kichwa wala miguu. Jikite katika kutafuta hela, Achana kushindana na watu kama Erythrocyte au akina brazaj etc , wenzako wanalipwa na chadema!

KAZI yangu ni kuandika Boss.

Unanifananishaje na watu usiowajua hata wewe wanaotumia Fake ID?
 
images - 2021-12-31T091229.995.jpeg
images - 2021-12-31T091244.183.jpeg
images (2).png
images - 2021-12-31T091115.593.jpeg
 
Tatizo lako unapoteza muda mwingi kutafuta umaarufu hapa JF kwa kuandika makala zisizo na kichwa wala miguu. Jikite katika kutafuta hela, Achana kushindana na watu kama Erythrocyte au akina brazaj etc , wenzako wanalipwa na chadema!
Nchi hii watu wana shida sana.
1. Unamjua hadi umwambie ajikite kutafuta pesa?
2. Huwa anaomba msaada hapa?
....Watu hufanya mambo kwa kujifurahisha nafsi. Huenda anapotoa ujumbe flani katika jamii moyo wake hufurahi, tuache mambo ya kuona mtu anapoteza muda badala ya kutafuta pesa.
Pesa sio kila kitu.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom