Miaka ijayo Rais Samia atakumbukwa kama 'Iron Lady', tumpe muda ya kuendeleza vita vya uhujumu uchumi na ugaidi

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Tukiachana na unafiki, hakika nikiri kusema Serikali ya Rais Samia ni imara na madhubuti kwenye kusimamia amani na usalama wa nchi yetu.

Jukumu la Rais kama amri jeshi mkuu ni kuhakikisha usalama na amani vinalindwa kwa nguvu zote na yeyote anayeonesha viashiria vyovyote vya kuvunja amani anadhibitiwa na kushtakiwa.

Katika mambo yanayohatarisha uchumi na uwekezaji ni uwepo wa vitendo vya ugaidi unaoratibiwa kwa mgongo wa siasa na wahusika waonekane wanaonewa vinavyodhibiwa.

Utawala wa Rais Samia Suluhu umesema hapana na kama mtanzania mwenye uchungu na Taifa lake anapigana kufa na kupona kuhakikisha usalama upo kwa ajili ya wawekezaji na watanzania kwa ujumla.

Tusiwe wepesi wa kulaumu pale wanaoenda kinyume na sheria zetu wanapoadhibiwa na badala yake tupongeze kwa maamuzi mazuri yanayofanywa na Serikali.

Serikali ya Rais Samia imeonyesha mfano wa Serikali makini inavyopaswa kuwa linapotea kundi la watu linapochochea uhalifu kwa mgongo wa siasa.

Ni muda muafaka sasa watanzania kuamini vita vya ugaidi na uhujumu uchumi vilivyopiganwa na Serikali ya awamu ya tano vimepata mpambanji mwingine hodari wa kuviendeleza.

MIMI NINAAHIDI KUWA NA RAIS SAMIA KWENYE VITA YA UGAIDI
 
Na aliposema nasimamisha uchumi we ulielewa nini na sasa hivi unaona uchumi umesimama au haujasimama unaenda mbele.
 
Iron Lady ni mtu jasiri asiyeogopa kivuli cha mtangulizi wake na hao wanaomzunguka - bado hajafikia viwango.
 
Kama kweli jasiri asiache asili......Gwaji na slow slow wazibwe midomo
 
Tuendelee kumuweka kwenye maombi Mungu wa Mbinguni amuongoze huyu kiongozi wetu. Matokeo ya uongozi wake tunaoumia ni wananchi. Angalia kuhusu tozo za simu. Nikasikia 'tetesi' Mbeya watu wanafuata mafuta ya Petrol/Diezel Zambia. Eti huko yako rahisi ukilinganisha na hapa kwetu. Kumbuka Zambia wanatumia kwa sehemu bandari na ardhi yetu kufikiwa na hayo mafuta.

Ukishakuta yuko Kiongozi/Viongozi wa watu wanaoshindwa kupata ufumbuzi wa mambo ya msingi kama haya ili kuwasaidia walio wapa jukumu la kuwaongoza jua kuna tatizo kubwa mahali. Neema ya Mungu wa Mbinguni isitupungukie ili itusaidie kuepukana na janga hili.
 
Uzuri sijawahi kusema lolote juu yake. Namuona kama binadamu aliyepitiwa na Zali la mentali tu kufika alipofika. Hata yeye anajishangaa kwa nini yuko hapo na Jana kathibitisha kwa kumwambia Salim Kikeke kuwa hakuwa na hana maandalizi yoyote ya kuwa kwenye nafasi hiyo. Yaani kocha msaidizi asiyejiandaa kuwa kocha mkuu siku moja!!
 
Tumia hekima na busara, kiongozi chini Rais be it Makamu wa Rais akisema alijiandaa kuwa Rais kuwa maana yake ni uhaini na unaweza kufikirika vibaya kwamba ulipanga njama fulani. Ni kweli hakujiandaa kwa sababu maandalizi ya Urais ni mpaka 2025 na sio kipindi nchi ina Rais
 
Hapa nilipo tu Mimi nimejiandaa kuwa Rais, iweje kwake aliyekuwa VP? Kwani kuna chuo watu wanajiandaa kuwa marais?
 
Wewe haina shida hata ukijianda kuwa Katibu Mkuu wa UN kwa sababu upo mbali na hiyo nafasi, mimi nazungumzia VP ambaye yupo karibu kabisa na u-rais
 
Kazi yake kwani ni kuzibsla midomo watu? Au ni kuwasikiliza wote wenye kumpinga na wanaomuunga mkono Kama wewe, na kufanya maamuzi sahihi?.
Kama kweli jasiri asiache asili......Gwaji na slow slow wazibwe midomo
 
Tukiachana na unafiki, hakika nikiri kusema Serikali ya Rais Samia ni imara na madhubuti kwenye kusimamia amani na usalama wa nchi yetu.

Jukumu la Rais kama amri jeshi mkuu ni kuhakikisha usalama na amani vinalindwa kwa nguvu zote na yeyote anayeonesha viashiria vyovyote vya kuvunja amani anadhibitiwa na kushtakiwa.

Katika mambo yanayohatarisha uchumi na uwekezaji ni uwepo wa vitendo vya ugaidi unaoratibiwa kwa mgongo wa siasa na wahusika waonekane wanaonewa vinavyodhibiwa.

Utawala wa Rais Samia Suluhu umesema hapana na kama mtanzania mwenye uchungu na Taifa lake anapigana kufa na kupona kuhakikisha usalama upo kwa ajili ya wawekezaji na watanzania kwa ujumla.

Tusiwe wepesi wa kulaumu pale wanaoenda kinyume na sheria zetu wanapoadhibiwa na badala yake tupongeze kwa maamuzi mazuri yanayofanywa na Serikali.

Serikali ya Rais Samia imeonyesha mfano wa Serikali makini inavyopaswa kuwa linapotea kundi la watu linapochochea uhalifu kwa mgongo wa siasa.

Ni muda muafaka sasa watanzania kuamini vita vya ugaidi na uhujumu uchumi vilivyopiganwa na Serikali ya awamu ya tano vimepata mpambanji mwingine hodari wa kuviendeleza.

MIMI NINAAHIDI KUWA NA RAIS SAMIA KWENYE VITA YA UGAIDI

CCM hawawezi kutaka katiba mpya, katiba hii imewezesha wana CCM kutengeneza utawala wa kurithiana wao na vizazi vyao, fuatilia wabunge , Ma DC, Ma RC, RAS, DAS, DED huko wamejazana watoto wa viongozi wa zamani, au ndugu zao, usitegemee watu wanaonufaika na katiba hii kukubali katiba mpya.
 
Interview ya Salim Kikeke na Samia jana imefanya mambo makuu manne yafuatayo:

1.Imemfunua Samia ni nani,anataka nini na ana mpango wa kuifanyia nini Tanzania.Imemfunua kuwa ni dikteta muoga na asiejiamini.

2.Imemshusha Salim Kikeke kupindukia.

3.Imeumiza image ya BBC.

4.Imedhalilisha waandishi wa habari.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Back
Top Bottom