Miaka hii minne na ushei ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli

Nancyjoa13

Senior Member
May 18, 2018
167
97
1588141709697.png


KATIKA miaka hii minne na ushei ya uongozi wa Rais Dk John Magufuli, kuna mambo mengi yamejiri ikiwamo dhana kwamba kiongozi huyo anafanana kwa kiasi kikubwa na rais wa awamu ya kwanza, hayati Mwalimu Julius Nyerere
Uzoefu unaonesha kuwa, viongozi wenye sifa zinazofanana hata kama wangepishana kwa kipindi cha miaka 100, vikwazo ambavyo hupitia katika kutoa uongozi hufanana kwa kiasi kikubwa kulingana na nyakati za wakati huo

Si jambo la ajabu kusikia ama kuona wananchi wakimfanananisha Magufuli na Mwalimu Nyerere katika nyanja za kiuchumi hasa ndoto za ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere (zamani Stiegler’s Gorge) uliokuwa moja ya ndoto za Mwalimu Nyerere ambao sasa unatekelezwa na serikali ya awamu ya tano

Sambamba na hilo, ndoto mbalimbali za Mwalimu zimeendelea kutekelezwa katika awamu hii, ikiwemo mpango wa kuhamia Dodoma ulioanza kupangwa tangu mwaka 1973. Hata kaulimbiu ya sasa ya Hapa Kazi Tu inakwenda sambamba na hotuba za Mwalimu Nurere ikiwemo ya Uhuru ni Kazi aliyoitoa Mei 01, 1974 kwenye sikukuu ya wafanyakazi.

Mwalimu pia alipata kusema Kila Mtu Afanye Kazi katika hotuba aliyoitoa katika ukumbi wa Diamond Jubilee Juni 25, 1976 kwa viongozi wa chama na serikali mkoa wa Dar es Salaam na pia alipata kusema ‘Heshima ya Mtu ni Kazi’ kupitia hotuba ya Julai 27, 1967, kwenye mkutano mkuu wa NUTA

Katika hotuba aliyoitoa kwenye mkutano maalumu wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mkoani Mwanza Desemba 12, 2019, Magufuli anasema: Kumekuwa na changamoto ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo kama Serikali katika jitihada zetu za kuleta mageuzi ya kijamii na kiuchumi

Kusema kweli, mimi huwa sipendi sana kuzungumzia changamoto; huwa napenda kuzikabili moja moja. Lakini kwa minajili ya hadhara hii, nitazitaja mbili tu

Watu hawa kamwe hawataki kuona tunadhibiti rasilimali zetu ambazo walikuwa wakizivuna na kusafirisha wanavyotaka bila kuulizwa na mtu. Zaidi ya hapo, watu hawa hawatakubali tutekeleze miradi mikubwa ya kimapinduzi itakayoharakisha maendeleo nchini, ikiwemo Bwawa la Nyerere, SGR au Kufufua Shirika la ATCL

Wangependa tuendelee kuwategemea wao, ilihali wao wanaishi kwa kwa kutegemea rasilimali zetu.” Kupitia hotuba hiyo unaweza kuona nia njema ya Rais ambayo inalenga kuipelekea Tanzania kwenye uchumi bora zaidi lakini anakumbana na vikwazo kama ambavyo alikuwa akikabiliana navyo Mwalimu; Ni jambo jema, lakini.


Chanzo: Habari leo
 
Back
Top Bottom