Miaka 82 ya penzi la Malkia Elizabeth II na Mwanamfalme Philip

MWAKA 1939, Elizabeth alikuwa binti mwenye umri wa miaka 13. Urembo wake haukuwa na kificho. Mwaka huo, Philip alikuwa kijana barubaru, umri wake tayari ulishatimia miaka 18. Ndipo wakakutana. Binti wa miaka 13 akaangukia kwenye penzi la kijana mwenye miaka 18.

Elizabeth na Philip wakawa wanaandikiana barua za urafiki. Kutoka urafiki, ukawadia uchumba kisha ndoa. Ilipofika Aprili 9, mwaka huu, Philip akaitikia wito wa Mungu. Ukihesabu kutoka mwaka 1939 mpaka 2021 ni miaka 82 iliyotimia. Elizabeth ameachwa peke yake na rafiki waliyedumu kwa upendo na uaminifu mkubwa kwa miaka 82.

Hapo sasa utaelewa pale Elizabeth anaposema kuwa amejihisi mpweke mno kuliko wakati wowote ule kwenye maisha yake. Philip na Elizabeth, mapenzi yao hayakuwa na kishawishi chochote kile cha pembeni. Walipendana wakiwa wadogo, mioyo yao ikiwa bado salama kabisa dhidi ya visa vya dunia. Walipofunga ndoa, wakaishi pamoja kwa takriban miongo nane.

Elizabeth ndiye Malkia Elizabeth II wa United Kingdom (UK) au kwa jina linguine Great Britain, dola inayounganisha visiwa vya Uingereza (England), Scotland na Northern Ireland. Moja ya dola imara ambazo zimekuwa zikitafsiriwa kama viranja wa dunia. Hapohapo, Malkia Elizabeth II ndiye binadamu anayetajwa kuwa na mamlaka makubwa ya moja kwa moja kuliko yeyote duniani.

Malkia Elizabeth II, mbali na UK, mpaka sasa ni Malkia wa Canada, New Zealand, Australia, Jamaica, Barbados, The Bahamas, Grenada, Papua New Guinea, Visiwa vya Solomon, Tuvalu, St Lucia, St Vincent na Grenadines, Belize, Antigua na Barbuda, St Kitts na Nevis.

Malkia Elizabeth II, alishakuwa Malkia wa Tanganyika (Tanzania Bara) kabla haijajitangaza kuwa jamhuri Desemba 9, 1962, vilevile Pakistan, Afrika Kusini, Ghana, Nigeria, Kenya, Malawi, Gambia, Trinidad na Tobago, Ceylon, Sierra Leone, Uganda, Mauritius, Malta, Guyana na Fiji.

Philip akawa ndiye mume wa mwanamke huyo mwenye mamlaka hayo makubwa duniani. Unaweza kujiuliza maisha ya ndani yalikuwaje? Philip anapewa sifa kubwa muhimu kwamba pamoja na kuwa mume wa Malkia, alitambua nafasi yake na alijua kucheza nayo. Kamwe hakufanya jambo la kumuaibisha Malkia katika kipindi chote cha ndoa yao, iliyodumu kwa miaka 74.

Philip, siku zote alipoamua kuzungumza kwenye uso wa jamii, kilichotoka kwenye kinywa chake kililenga moja kwa moja kumuunga mkono Malkia. Hakuna wakati wowote amewahi kutumia nafasi yake kama mume kuwa mwavuli wa kufunika hadhi, cheo na heshima ya Malkia. Philip hakuwahi kumtweza wala kumkwaza Malkia katika uso wa jamii.

Hata pale Philip alipoonekana kutoa kauli kali hadharani, mara nyingi ilikuwa kwa ajili ya kumtetea Malkia na koo ya kifalme. Na kwa sababu kwake aliingia kwenye uhusiano na Elizabeth miaka zaidi ya 80 iliyopita, akitambua ni mwanamke wa aina gani, kwa hiyo siku zote alihakikisha anaiweka mbele heshima na hadhi ya Malkia, badala ya kuinua mabega kuwa mume wa Malkia.

MIAKA 82 ILIYOPITA

Aliyekuwa Mfalme wa UK, George VI, alimuoa Elizabeth. Katika ndoa yao, wakapata watoto wawili, wote mabinti; Elizabeth (mkubwa) na mdogo wake, Margaret. Huyo Elizabeth (mtoto mkubwa), ndiye Malkia Elizabeth II. Hivyo, Malkia Elizabeth, mama yake naye anaitwa Elizabeth. Kuna Elizabeth Malkia ma Elizabeth mama wa Malkia (Queen Mother) ambaye alikuwa mwenzi wa Mfalme (Queen Consort).

Mwaka 1939, Mfalme George VI, akiongozana na mkewe, Elizabeth, vilevile mabinti zake, Elizabeth na Margaret, walitembelea chuo cha kifalme cha mafunzo ya jeshi la majini, Royal Naval College, kilichopo Dartmouth, Devon, England.

Louis Mountbatten ni mjomba wake Philip. Aliuawa mwaka 1979. Mwaka 1939, Mountbatten alikuwa ofisa mkuu wa Chuo cha Royal Navy. Kipindi hicho, Philip pia alikuwa akipokea mafunzo ya kijeshi Royal Navy College.

Sasa, Mfalme George VI na mkewe, Elizabeth, wakawa wanazungumza na Mountbatten. Kuacha mazungumzo ya watu wazima yaendelee, Elizabeth (Queen Mother), akamuomba Philip awazungushe kwenye maeneo ya chuo mabinti zake, Elizabeth (Malkia Elizabeth) na Margaret.

Huo ukawa mwanzo wa Elizabeth (Malkia Elizabeth) kufahamiana na kijana mzuri, aliyemvutia, Philip. Urafiki wao ukawa wa kuandikiana barua. Mwaka 1946, Philip akagonga hodi kwenye kasri la Mfalme wa Uingereza kuomba mkono wa ndoa kwa binti yake wa kwanza, Elizabeth II.

Mwaka huo, 1946, Elizabeth alikuwa na umri wa miaka 20. Mfalme George VI alikubali posa ya Philip, lakini sharti likawa kusubiri Elizabeth II afikishe umri wa miaka 21 ndipo aolewe. Ndio maana, mwaka 1947, Elizabeth alipokuwa na umri wa miaka 21, akafunga ndoa na Philip.

Baada ya miaka sita ya ndoa, Elizabeth II alitawazwa kuwa Malkia wa UK, kufuatia kifo cha baba yake, Mfalme George VI. Aprili 21, mwaka huu, Malkia Elizabeth II atatimiza umri wa miaka 95 ya kuzaliwa. Kimahesabu, Malkia Elizabeth II amekuwa mtawala kwa miaka 68, huku Philip akiwa pembeni yake.

PHILIP ALIPOTOKA

Philip alikuwa mwanamfalme wa Ugiriki na Denmark. Philip ni mtoto wa mwanamfame wa Ugiriki na Denmark, Prince Andrew na Princess Alice wa Battenberg. Kwa kifupi hao ndio wakwe wa Malkia Elizabeth.

Mwaka 1947, Philip ilibidi ajitoe kwenye mnyororo wa kuwa Mfalme wa Ugiriki na Denmark ili atambulike kuwa raia wa UK aweze kumuoa Elizabeth II. Hivyo, safari ya Philip kumuoa Elizabeth II iliambatana na sadaka kubwa. Kuyaacha masilahi yote ya kuwa mwanamfalme wa Ugiriki na Denmark, pamoja na utaifa wa asili yake.

Lingine ambalo lilimjengea sifa kubwa Philip kufikia kuaminika na kukabidhiwa mke, Malkia wa UK aliyekuwa akisubiri (crown queen), ni historia yake ya kupigana upande wa Uingereza katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Kwa kutumikia kwake jeshi la UK, Philip alijikuta vitani dhidi ya shemeji zake wawili, Prince Christopher wa Hesse na Berthold, Margrave wa Baden, waliokuwa vitani kwa upande wa Ujerumani. Kwa kuchukua sifa hiyo kuwa aliitumikia Uingereza katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, jumlisha kwamba ni mpwa wa Mountbatten, Mfalme George VI hakuona sababu ya kumnyima Philip binti yake. Zingatia, Elizabeth II alikuwa ameshampenda Philip.

Juni 2, 1953, Malkia Elizabeth II alitawazwa rasmi kuwa Malkia wa UK na dola nyingine nyingi zilizokuwa chini ya taifa hilo. Kuanzia hapo, Philip akapewa cheo cha Duke wa Edinburg (unaweza kuita Mtukufu wa Edinburg). Duke ni cheo cha heshima kubwa ambacho hupewa mwanaume kwenye ukoo wa mfalme. Mwanamke huitwa Duchess.

Philip alirithi cheo hicho kutoka kwa mama mkwe wake, Elizabeth (mama wa malkia). Kipindi Mfalme George VI alipokuwa hai na akiwa ndio mtawala wa UK, mke wake, Elizabeth, ndiye alikuwa Mtukufu wa Edinburg (Duchess of Edinburg). Kwa sasa, Price Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Philip na Malkia Elizabeth II, ndiye kapewa cheo cha Duke of Edinburg.

Philip na Malkia Elizabeth, wamefanikiwa kupata watoto wanne katika ndoa yao. Wa kwaza ni Prince Charles, ambaye pamoja na kuwa Duke of Edinburg, vilevile cheo chake kingine ni kuwa Mwanamfalme wa Wales. Anne, ambaye cheo chake ni Princess Royal ni wa pili. Anafuata Prince Andrew (Duke of York) na Prince Edward (Earl of Wesse). Prince Charles ndiye Mfalme ajaye (a crown prince), endapo Malkia Elizabeth II atapokea faradhi ya kifo.

AMEZIKWA JANA KAWAIDA

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kasri la Malkia, Philip aliomba akifa asipewe mazishi yenye hadhi ya kitaifa, aliomba azikwe kawaida. Hivyo, jana, April 17, amepumzishwa kwenye nyumba yake ya dawamu, mazishi yake hayakutikisa.

Mwili wake haukubebwa kwenye gari la kijeshi lenye bunduki mbele na ibada ya mazishi ilifanyika kwenye kanisa la watu wachache. Wosia huo ambao aliuacha unaonesha kuwa Philip alikuwa mtu asiyependa makuu. Dhahiri, alipenda kuishi kawaida, akiruhusu kivuli cha Malkia kimfunike.

Jeneza lake halikufunikwa na Bendera ya Taifa la UK, badala yake, lilipambwa na bendera maalum yenye kuonesha asili ya utaifa wake (Ugiriki), vilevile vyeo vyake vya kijeshi alivyovipata alipokuwa anatumikia jeshi la UK.

Tangu alipoitikia wito wa kifo, mwili wa Philip ulilazwa kwenye kanisa la Windsor Castle, lililopo katika eneo maalum la makazi ya kifalme. Ujumbe tofauti ulitumwa kutoka ndani ya ukoo wa Malkia. Kutoka Prince Charles hadi Princess Royal walioeleza mguso wa kifo cha baba yao.

Kinachovutia zaidi, kifo cha Philip kimemrudisha nyumbani, Prince Harry, aliyeondoka kwenye makazi ya Malkia, akiwa na mkewe, Meghan Markle na mtoto wao, Archie Mountbatten-Windsor, wakidai kubaguliwa. Meghan ni nyota wa zamani wa filamu mwenye asili ya Afrika.

Prince Harry amerudi UK kumzika babu yake, lakini Meghan na Archie wamebaki Marekani, wanapoishi kwa sasa. Hta hivyo, swali kubwa kwa sasa ni kwa nini Prince Harry amerejea peke yake bila Meghan na Archie?

View attachment 1755126View attachment 1755127View attachment 1755128
Huu uhusiano thabiti umetufumba midomo wengi.

Hali ya mahusiano ni tete a tata
 
Hao huwa hawatafuti waume/wake wa kuoa au kuolewa bali wanatafutiwa wa kuoa au kuolewa nao kwahyo Philip na Elizabeth walishapangiwa kuwa wataoana
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa ni kwamba huyu mama aliwahi kuchumbiwa na bwana David Williamson mmiliki na mwanzilishi wa mgodi wa Mwadui mwanzani mwa miaka ya 50, mama huyu huyu ndiye aliyefungua jengo la kuchambulia Almasi pale Mwadui na ndiye alizindua kanisa la Anglican pale pale Mwadui; uchumba haukwenda mbali sana cause washauri wa familia ya Malikia walimkataa Dr. David Williamson kwamba anatokea familia masikini na nadhani ndio ilipelekea kifo chake huyu mwamba! Narudia, Nimesema, "kama kumbukumbu zangu zipo sahihi"
Aliuliwa au?
 
Sidhani kama uko sahihi.

Elizabeth alianza kumtamani kijana Phillip akiwa bado mdogo sana kama miaka 13 na kijana akiwa na miaka 18 na walikutana kwenye moja ya harusi za kifalme.

Baadae baada ya miaka mitano yaani mwaka 1939 wakaanza mahusiano.

Baada ya vita wakawa wanakutana jamaa akiwa chuo cha mafunzo ya kijeshi.

Walichumbiana rasmi mapema mwaka 1947na wakaoana mwishoni mwa mwaka huohuo.

Hivyo utaona bwana David Williamson kwenye hiyo miaka ya 50 alikwishachelewa.
Hii story bibi yangu ananipa mkanda now ......nadhani ina kaukweli flani
 
Prince Phillip alijitoa Sana, pia ni fundisho kumbe ndoa kudumu Hadi uzeeni inawezekana kabisa
Dia hawa walizaliwa kwenye asali wakakulia kwenye maziwa.

Take note that, hata kukutana kwao walikutanishwa shule maalumu shule za hivyo walipa tozo hawawezi peleka watoto wao.
 
Huu utaratibu ndo mzuri na umeiletea uingereza heshima kubwa na iliweza kutawala dunia, utawala wao ni miiko ya kimila siku wakiacha watasambaratika hata huku Africa kinachotukwamisha ni kuiga democracy za nje wakati tulikuwa na watawala wetu wa asili tofauti na alivokuja mzungu na Berlin conference imagine Tanganyika imeinganishwa makabila mangapi wengine wavivu, wachapakazi wamekusamywa humo ndio maana watu hawana uchungu ni ufisadi, nepotism plus ukabila tu wakati wa chiefdom kila kabila lilikuwa ni chief wake na hyo ingerahisisha maendeleo ni ngumu kuibia ndugu mnao share language na vinasaba Kama Sasa.
Umenichekesha sana..kwamba Tanganyika iliunganishwa na makabila mengine ni wavivu!
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa ni kwamba huyu mama aliwahi kuchumbiwa na bwana David Williamson mmiliki na mwanzilishi wa mgodi wa Mwadui mwanzani mwa miaka ya 50, mama huyu huyu ndiye aliyefungua jengo la kuchambulia Almasi pale Mwadui na ndiye alizindua kanisa la Anglican pale pale Mwadui; uchumba haukwenda mbali sana cause washauri wa familia ya Malikia walimkataa Dr. David Williamson kwamba anatokea familia masikini na nadhani ndio ilipelekea kifo chake huyu mwamba! Narudia, Nimesema, "kama kumbukumbu zangu zipo sahihi"
Sidhani uko sahihi mkuu! Hata njia zo utoto hawajawahi kukutana...hebu turudie historia zao!
 
Huwa najiuliza ikiwa ikitokea kizazi kuna mgumba,au vyovyote vile asipatikane mtoto,huwa inakuaje kwenye kuchagua ufalme/malkia???

Mfano eliza na philip wasingefanikiwa kupata mtoto.
 
Huwa najiuliza ikiwa ikitokea kizazi kuna mgumba,au vyovyote vile asipatikane mtoto,huwa inakuaje kwenye kuchagua ufalme/malkia???

Mfano eliza na philip wasingefanikiwa kupata mtoto.
Elizabeth walizaliwa wawili tu,mdogo wake alikua anaitwa Princess Margreth, Kama asingekuwa na watoto mpaka kufa umalkia ungekwenda kwa Margreth
Margreth aliisha fariki 2002,aliiacha watoto wawili David na Sarah.
Kumbuka pia ilikuwa ni BAHATI kwa Elizabeth kuwa Malkia, aliyetakiwa kuwa mfalme alikuwa ni Edward,huyu alikukataa ufalme kwa mpenda mwanamke Marry Wills Walls Simphson ambaye nadhani alikuwa ametalikiwa na alikuwa Mmarekani, alipoukataa ufalme kwa ajili ya Mwanamke ukaenda kwa mdogo wake,akawa Mfalme George aliyemzaa Elizabeth, hivyo Baba Mkubwa wa Elizabeth aliukataa ufalme kwa ajili ya kupenda!
 
Elizabeth walizaliwa wawili tu,mdogo wake alikua anaitwa Princess Margreth, Kama asingekuwa na watoto mpaka kufa umalkia ungekwenda kwa Margreth
Margreth aliisha fariki 2002,aliiacha watoto wawili David na Sarah.
Kumbuka pia ilikuwa ni BAHATI kwa Elizabeth kuwa Malkia, aliyetakiwa kuwa mfalme alikuwa ni Edward,huyu alikukataa ufalme kwa mpenda mwanamke Marry Wills Walls Simphson ambaye nadhani alikuwa ametalikiwa na alikuwa Mmarekani, alipoukataa ufalme kwa ajili ya Mwanamke ukaenda kwa mdogo wake,akawa Mfalme George aliyemzaa Elizabeth, hivyo Baba Mkubwa wa Elizabeth aliukataa ufalme kwa ajili ya kupenda!
Yah king Edward alidumu kwenye ufalme miezi 11 baada ya inshu ya abdiction ndio George akachukua ufalme, kwa hyo queen Elizabeth kaupata ufalme kibahati Sana..
 
Yah king Edward alidumu kwenye ufalme miezi 11 baada ya inshu ya abdiction ndio George akachukua ufalme, kwa hyo queen Elizabeth kaupata ufalme kibahati Sana..
Alikuwa loyal kwa mwanamke wake,sijui Harry atafika wapi na Meghan,maana licha ya yote ndoa huwa zinawatatiza sana. ELizabeth alipata mwanaume cool.
 
Back
Top Bottom