Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,853
- 30,196
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA: MABAIBUI YALIYOMPOKEA MWALIMU NA MAMA MARIA NYERERE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Katika mazungumzo na BBC Swahili jana Mama Maria Nyerere amewasifia mama zetu kwa ushujaa wao wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Dada yangu Ummie Alley aliniomba nimtafutie hawa akina mama na nililiweka hapa historia fupi ya kina mama hawa wa TANU waliomuunga mkono Mwalimu Nyerere kuanzia siku ya kwanza alipopanda jukwaani Mnazi Mmoja kuidai Tanganyika.
Akina mama hawa Mama Maria anawajua vizuri sana - Bi. Chiku bint Said Kisusa, maarufu akifahamika kama Mama Sakina, Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu Mama Daisy, Bi. Hawa bint Maftah kwa kuwataja wachache.
Hawa ndiyo walikuwa mashoga zake waliompokea yeye na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950.
Nilimuahidi Da Ummie kuwa nitamwekea picha ya hawa akina mama wakiwa katika mkutano wa TANU Mnazi Mmoja picha iliyopigwa na Mohamed Shebe.
Angalieni picha hiyo hapo chini ambayo Shebe ameipiga kutoka juu.
Utaona kuna sehemu imejitenga kuna nyeusi tupu.
Huo weusi ni mabaibui ya mama zetu ambao miaka hiyo katika mikutano yote ya TANU wanawake walikuwa na sehemu yao maalum wakikaa.
Hapo ndipo zilipokuwa kunatoka vigelegele na nyimbo za lelemama Julius Nyerere alipokuwa anapanda jukwaani kaongozana na Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
Sheikh Suleiman Takadir yeye kazi yake ilikuwa kupiga fatha kuomba dua kisha kumtambuisha Julius Nyerere kwa wenyeji wa Dar es Salaam.
Kumtia hamasa Mwalimu, Bi. Titi Mohamed na Hawa bint Maftah wataanzisha nyimbo maarufu ya lelemama na uwanja mzima utaimba:
''Mheshimiwa nakupenda sana,
Wallahi sina mwinginewe,
In Shaa Allah Mungu yupo,
Tanganyika tutajitawala.''