Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika: Kisa cha Julius Nyerere na vilio vya akina mama

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,912
30,254
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA: KISA KILICHOWALIZA WANAWAKE WANNE PEMBENI YA JULIUS NYERERE WAKATI WA KUPIGANIA UHURU

''Kwa kuwa umependa kumbukumbu hizi za nyumbani kwetu Gerezani basi nataka nikupe kisa kilicholeta taharuki kubwa ambayo naelezwa haijapata kutokea katika historia ya TANU na Nyerere labda hadi Baba wa Taifa anaaga dunia.

Siku za mwanzo za TANU viongozi wake walikuwa wakiwa na jambo zito la kujadili walikuwa wakikutana nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Walikuwa wakimaliza shughuli basi inakuwa chakula na vinywaji kujipongeza.

Siku hiyo baada ya kikao wakala chakula cha mchana.

Baada ya kula ghafla Nyerere akaanza kulalamika kuwa tumbo linamkata.

Nyerere akawa anajipindua huku na huku kwa maumivu.

Siku zote TANU walikuwa wakiishi chini ya hofu ya Nyerere kudhuriwa na maadui wa TANU lakini katika chakula kile cha nyumbani kwake hapakuwa na hofu kwani chakula chake kilikuwa kinatoka Kariakoo na kwa watu maalum ambao Market Master, Abdul Sykes akiwafahamu na Mzee Mshume na ndiye akikinunua, mpelekaji wa chakula hicho kwa Mama Maria alikuwa dereva wa TANU, Said Kamtawa maarufu kwa jina Said TANU.

Nyerere kalala kwenye kochi anaugulia na taharuki ikazuka na minong'ono haikuweza kukwepeka.

Nyerere kalishwa sumu!

Sumu Nyerere alishwe nyumbani kwa Abdul Sykes?

Uani jikoni walikuwa mama yake Nyerere Bi. Mgaya, Mama Maria, mama yake Abdul Sykes Bi. Mruguru bint Mussa, mkewe Abdul Sykes, Mama Daisy.

Bi. Mgaya hakuweza kustahamili alipoona wanaume ingia toka kule ndani.

Aliposikia kuwa Nyerere anaumwa baada ya kula chakula kitu cha kwanza kilichomjia ni kuwa mwanae kalishwa sumu akawa sasa mikono kichwani analia na kutembea ua mzima.

Bi. Mgaya anasema Kizanaki na anachanganya na Kiswahili.
Ikawa patashika nguo kuchanika kumtuliza.

Wote waliokula chakula kile walikuwa salama na hawa ni watu waliokuwa wakijuana vizuri na wakiaminiana mwisho wa imani.

Nani anaweza kupenya nyumbani kwa Abdul akampa sumu Nyerere?

Nani?

Mama Daisy ndiye alikua akinihadithia alipomaliza aliinamisha kichwa akasema, ''Mwanangu Mohamed, Abdul na Nyerere wametoka mbali sana na walikuwa zaidi ya ndugu.''

Iko siku nitakileta hapa kisa cha sanduku la fedha la Abdul Sykes kama nilivyokipokea kutoka kwa Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Picha ya kwanza ni mama yake Julius Nyerere Bi. Mugaya Nyag'ombe, Bi. Mruguru bint Mussa Mohamed mama yake Abdul Sykes, Ally na Abbas, Mama Maria Nyerere na Bi. Mwamvua bint Mrisho.

Screenshot_20211201-234330_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom