Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika: Athmani Matenga Mwanachama wa TANU 1954 tawi la Ali Msham Magomeni apipa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,083
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: ATHMANI MATENGA MWANACHAMA WA TANU YA 1954 TAWI LA ALI MSHAM

Athmani Matenga ni mmoja wa wanachama wa TANU ya 1954 aliye hai hivi leo.

Mzee Athmani Matenga alijiunga na TANU katika tawi aliloanzisha Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu, Magomeni Mapipa mwaka wa 1954.

Wakazi wengi wa Magomeni ya miaka ile ya kupigania uhuru wa Tanganyika walikata kadi zao za TANU kutoka tawi hili.

Athmani Matenga alikuwa akiishi jirani ya makaburi ya Mwinyimkuu na hadi sasa bado anaishi hapo na si mbali na iliyokuwa nyumba ya Ali Msham na tawi la TANU.

Mzee Athmani Matenga anasema yeye alikwenda kumpokea Julius Nyerere alipotoka safari ya kwanza UNO mwaka wa 1955 akiendesha pikipiki miaka hiyo akiwa kijana mbichi.

May be an image of 2 people and people sitting
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom