Miaka 60 ya uhuru; vijiji vingi havina maji, umeme, na barabara hazipitiki.

Surveillance

Member
Dec 2, 2018
25
22
Kwanza nimpongeze rais kwa kuzindua mradi mkubwa wa maji Arumeru wenye thamani ya bilioni 500. Kama walivyosikika wabunge wengine wa Arusha, nchi nzima mijini na vijijini kuna shida kubwa ya upatikanaji wa maji tangu dunia iumbwe. Hali kadhalika umeme umekuwa ni ndoto kwa asilimia kubwa ya watanzania. Barabara zinazounganisha vijiji na miji nazo nyingi hazipitiki kwa misimu yote. Ninamuomba rais wangu ajizatiti zaidi kwenye miradi ya maendeleo kwa wanyonge wa vijijini. Amefanya mambo mengi mazuri, ila wasiwasi wangu miradi hiyo haina 'impact' ya moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida kama mkulima, mfugaji, na wafanyabiashara wadogo. Anaweza akapunguza bajeti za flyovers na bombadier ili atekeleze miradi ya huduma za jamii zaidi kwa ajili ya wananchi wanyonge hasa wa vijijini
 
Kabisa,ukipata muda katembelee kagera kyerwa ndani ndani huko yani kulala tu siku moja km mwaka.
 
Kwanza nimpongeze rais kwa kuzindua mradi mkubwa wa maji Arumeru wenye thamani ya bilioni 500. Kama walivyowasikika wabunge wengine wa Arusha, nchi nzima mijini na vijijini kuna shida kubwa ya upatikanaji wa maji tangu dunia iumbwe. Hali kadhalika umeme umekuwa ni ndoto kwa asilimia kubwa ya watanzania. Barabara zinazounganisha vijiji na miji nazo nyingi hazipitiki misimu yote. Ninamuomba rais wangu ajizatiti zaidi kwenye miradi ya maendeleo kwa wanyonge wa vijijini. Amefanya mambo mengi mazuri, ila wasiwasi wangu miradi hiyo haina 'impact' ya moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida kama mkulima, mfugaji, na wafanyabiashara wadogo. Anaweza akapunguza bajeti za flyovers na bombadier ili atekeleze miradi ya huduma za jamii zaidi kwa ajili ya wananchi wanyonge.
Mhh vijiji vya ufipa mkijengewa miundo mbinu mnagoma mnasema hamli miundombinu...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom