Miaka 60 ya uhuru! Tuambizane ukweli tusiwafurahishe watawala!!!

haha

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
1,400
1,628
Miaka 60 ya Uhuru hiyooo!!! Hakina ni safari ndefu na mengi yamefanyika ila tusemezane ukweli bado,bado tupo mbali ( nyuma).Tambo za wanasiasa hazisadifu hali halisi!?

"Tukitaka kujifananisha tujue tumekimbia kiasi gani ,tutazame walifanikiwa " je !?? Wao wametumia njia zipi!?

Nikweli tuna barabara za kutuunganisha ,tumejitahidi katika baadhi ya mambo mfano umeme umefika maeneo mengi ya nchi (/japo familia nyingi tuna umeme ambao hatuwezi kuutumia kwa baadhi ya shughuli zetu za ndan kama vile kupikia kutokana na garama kubwa per unit)
Tumebakiza miaka 40 ilitutimize miaka 100 ya uhuru!

Kuna maeneo ambayo nadhan yapaswa kutazwamwa kwa jicha LA tatu!

Najaribu kijiuliza nchi kama malesia,China,Taiwan ,Singapore nk ambazo kuna ushahidi wa data kuwa miaka ya 1960 zilikuwa sawa na sisi mbona zimetuacha kiasi hicho!?

Tuna kila kitu cha kutufanya tuwe kama wao tatizo letu ni lipi!??

Nimesoma mahali duniani kuna maziwa makuu kumi ( ten great lakes) kilichoniumiza zaid matatu yapo Tanzania!!!!!!! Dahhhh hii ni bahati ya namna gani!?

Achilia mbali rasilimali nyingine!! Sasa tatizo ni nini hasa!

Mwalim JK Nyerere aliwahi kusema ili tuendelee twahitaji
1)/watu ( ambao tunao)
2)ardhi (IPO ya kutosha)
3) siasa safi ( hapa sina hakika)

Sasa tufanyaje!?
Elimu yetu baada ya miaka 60 imekuwa hoi!!! Ubora wa wahitimu wa miaka ya 70s,80s,90s ni tofauti mno na 2000s !!! Yani kadiri tunapokua mbali na uhuru ndio hali yazidi kuwa hoi kielimu katika ubora tunakwama wapi!?Leo miaka 60 ya uhuru hakuna waziri anadhubutu kupeleka mtoto shule ya uma!??? Halafu ukiwaona kwenye TV wanasifia mafanikio ya uhuru!!!

2) viwanda !!!yani 60 miaka ya uhuru tunaagiza mafuta ya kula wakati tulikuwa na viwanda vya kutosha baada ya uhuru !!! Alizet IPO ,mbegu za pamba zipo tatizo nn!?

3) ajira !!! Wanasiasa wanatumbia tujiajiri bila kuwana skills!!!!!!!MTU kama hajaandaliwa anajiajiri vipi!?? Kama sio kuzalisha wazururaji "wamachinga!??

Hali ya ajira ni janga kubwa watu vijana wasomi na wasio wasomi wanazurura mitaani mbaya zaid vyuo vinazid kudahili na serikali inazidi kulipia watu fedha!!!

Hakuna mkakati wowote na kutatua hilo tatizo zaid ya siasa nyepesi!?? Nini hatima ya hilo!??watoto wa viongiz hawana shida kwani Ukuu wa wilaya,U-das ,ukurugenzi achilia mbali vimemo kwenye mashirika ya umma!??

Vipi sisi wengine!?daaah! Hakika hali ni ngumu tuseme ukweli watawala waelewe!?

Kwa kifupi bado safari ni ndefu sana sana
 
Ndo hivyo tayari miaka 60 imefika Mkuu lakini tulikitoka na tulipo huwezi kuamini,,

nchi yenye ziwa Victoria inahudumia misri kwa kiasi cha maji alaf watu wake wa dodoma wapo jangwani hawana maji,,

Umeme sio wa uhakika kabisa kiasi kwamba unakata tu ovyo ovyo lakini kuna mabwawa makubwa na mito pia,,, alafu wanahimiza uwekezaji wakat umeme amna uhakika nani anapenda apate hasara.

Madini yapo yakutosha na yanachimbwa lakini mikataba yake inahuzunisha sana, upumbavu mwengine viongozi wenyew ndio wapigaji wakuu wakishirikiana na watu wengine,

Na bado kuna mengi mengiii sana hiyo ndio miaka 60 ya Uhuru Tz hatuna cha kujivunia zaidi ya amani ya kubumba na wazalendo wachache wa mchongo.
 
Tatizo moja nchi yetu ukiongea ukweli wewe ni adui mkubwa sana
Ukiosoa mabaya ya serikali wewe ni kama jambazi au mwizi

Tumekosa viongozi wenye maono tunaviongozi wanao jijali wenyewe tu na familia zao na kama wapo basi wachache sana
 
Ile heshima tuliyokuwa tumeirudisha chini ya JPM, imetoeka kama ukungu, baada ya kuwa "incapacitated" na kuzimwa kama mshumaa kwenye kimbunga! Ama kweli, adui hatoki mbali.
 
Back
Top Bottom