Miaka 60 ya uhuru maji bado shida tuwakabidhini nchi wazungu tu tuendelee

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,614
2,000
Mtakuja na nyuzi zenu za kusifu serikali na kupiga matarumbeta but ukweli ni kuwa hii nchi under ccm ni good for nothing

Hebu imagine miaka 60 ya uhuru hadi leo maji tu bado ni shida.

Miaka 60 ni mtu anazaliwa hadi mzee hivi CCM mna jipya gani?

Ni aibu kwa taifa hili hadi leo kuna kero ya maji miaka 60 hii.

Miaka 60 ukiwauliza wamefanya nini hawana majibu.

Ifike mahali tu watanzania tukubaliane kwamba ccm nchi imewashinda suala la kumaliza tatizo la maji ni suala la miaka 5 tu sio suala la miaka 60 hadi leo ni aibu tupu.

Amini nawaambia tutasheherekea miaka 100 ya uhuru tukiwa na shida hizi hizi tu na wimbo huu huu ya utegemezi na shida za maji

Ni aibu aibu aibu kwa nchi.

Ifike mahali miaka 60 tuone imetosha tuwape hii nchi mabeberu yote tu kwa mkataba kwamba wataleta maji, umeme, elimu, afya na barabara jumla kwa asilimia 100 tujue mchezo umekwisha kuliko kuendelea na mambo ya ajabu ajabu tu huku tukiwa palepale tu wakati kiyama kinakaribia mnataka kiama kije kikute nchi zetu na wimbo huu huu?

Bora tuwape wageni hii nchi tu kwa mkataba wa pasu kwa pasu ili hata tufike mbali kama kina korea ya kusini, singapore etc walau tufurahie kwa vichache huku kwa muda unavyokwenda nisemeje sasa?maana hakuna tumaini chini ya maccm ni bora hii nchi kuwapa wageni tu maana waafrica wa CCM wameshindwa na kutoka madarakani hawataki.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,297
2,000
Miaka 60 ya uhuru wa mdanganyika MIFUMO yote ya kutoa haki IPO KAPUTI...

Taasisi ya Tume ya Uchaguzi - MOCHWAREE

Taasisi ya kimahakama...ICU inapumulia machine ka mgonjwa wa Corona...

Taasisi ya Bunge...IPO kwenye GENEZA safari ya mazishini...niagieni niagieni..

Taasisi ya kutoa haki Mashitaka - ICU

Afu mtanzania unajidai eti una Uhuru...ambao uliupata mwaka 1961..maajabu.

Key indicators ya maendeleo ya nchi huru ni hiyo mifumo kufanya kazi kwa weredi na usawa..

Sasa kwetu mifumo hii inafanya chini ya 30%..Sisi si nchi HURU.
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
13,748
2,000
Upo sahihi mkuu.
Tuendeshe nchi kama kampuni. Wannchi ndiyo wenye nchi. Tuajiri watu kutoka mataifa mbalimbali wenye utaalamu watusaidie kutoka kwenye umaskini.

Tuajiri Rais, na mawaziri na sekta zote zinazohitaji wataalamu. Tuwe na rais kutoka Marekani, waziri mkuu ujerumani, waziri wa viwanda kutoka japan nk. Uzalendo na utaifa ni viini macho tu.
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,607
2,000
Hawatokubali hata mkiwapa bure, ni nani alikudanganya Muzungu anataka kuishi kwenye tropics Afrika ukiondoa AK ?
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,765
2,000
Waafrika tumeshindwa kujiongoza tumeshindwa kujitawala. Pana umuhimu wa kubinafsisha nafasi za juu za uongozi, mfano badala ya kuweka wanasiasa tuajiri watu toka nje bila kujali mataifa yao au rangi zao hata kwa contract ya miaka 5 mitano Ili watusaidie wananchi kutuletea maendeleo.

Mfano waziri mkuu ajiri toka India, waziri wa kilimo toka israel, waziri wa uchumi toka ulaya, wa ujenzi na miundombinu weka mchina, wa nn weka Mkenya , Wa nn weka Msauzi Afrika hata Kama watalipwa pesa ndefu lkn tupate top cream watuleteee maendeleo tunayo taka wananchi na sio wayatakayo watawala.
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,765
2,000
Miaka 60 ya uhuru wa mdanganyika MIFUMO yote ya kutoa haki IPO KAPUTI...

Taasisi ya Tume ya Uchaguzi - MOCHWAREE....
Kusema upo huru au Uhuru then upati basic needs hali unalipa Kodi huo Uhuru umekusaidia nini una maana gani kwako,si heri ya mkoloni alikupa basic needs,leo ni aibu hata kujenga tu vyoo vya shule hatuwezi Hali tunatunua ndege na mav8 cash.
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,765
2,000
Upo sahihi mkuu.
Tuendeshe nchi kama kampuni. Wannchi ndiyo wenye nchi. Tuajiri watu kutoka mataifa mbalimbali wenye utaalamu watusaidie kutoka kwenye umaskini.

Tuajiri Rais, na mawaziri na sekta zote zinazohitaji wataalamu. Tuwe na rais kutoka Marekani, waziri mkuu ujerumani, waziri wa viwanda kutoka japan nk. Uzalendo na utaifa ni viini macho tu.
Hili ndilo sahihi kwa afrika na sio hili la kuweka wezi madarakani,
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
13,748
2,000
Waafrika tumeshindwa kujiongoza tumeshindwa kujitawala. Pana umuhimu wa kubinafsisha nafasi za juu za uongozi, mfano badala ya kuweka wanasiasa tuajiri watu toka nje bila kujali mataifa yao au rangi zao hata kwa contact ya miaka 5 mitano Ili watusaidie wananchi kutuletea maendeleo...
Wakati visiwa vya Comoro vinapata uhuru kisiwa cha Mayote kilikataa kujiunga na umoja wa visiwa vya Comoro. Kikasema kinabaki kuwa chini ya Ufaransa. Leo hii wacomoro wanaenda kutafuta kazi Mayote.

Mi huwa nahisi utamaduni wetu wabantu hauturuhusu kuendelea kwa mazingira ya uchumi wa dunia yalivyo.
 

Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
1,982
2,000
Sisi tunajenga viwanda 100 kila mkoa na wapinzani ndio walituchelewesha...sukari tunazalisha hadi tunauzia majirani! 5 tena
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,208
2,000
Kwa kweli maji ni shida kubwa sana !

Sijui kwa wengine siyo kipaombele?

Mashuleni maji ni shida
Hospitali maji ni shida
Majumbani maji ni shida
Viwandani
Mama lishe

N.k
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,765
2,000
JE HOTUBA ALIYOITOA RAISI TRUMP SEPTEMBER 2018 JUU YA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA NI MATUSI AU NDO UKWELI?

Kumbuka wakati huu karibu nchi 133 za dunia zimekutanika ikiwemo na Tanzania ambayo imewakilishwa na waziri wa mambo ya nchi za nje.
Haya ni mambo yaliyonukuliwa katika hotuba ya Raisi Trump akiongelea bara la Afrika. Naomba usome na utoe maoni yako. Akiwa anawasuta viongozi wa Afrika, Trump anahoji kwamba:
  • lkiwa sasa imefika miaka 50 ya uhuru na bado viongozi wengi wa Afrika wameshindwa kuwa na miundo mbinu thatbiti kwa ajili ya watu wao, je hao viongozi ni binadamu kweli?
  • Anaendelea kusema kuwa ikiwa ninyi viongozi mnakalia dhahabu, almasi, mafuta na uranium na watu wenu wanakosa chakula, je ninyi viongozi wa afrika ni watu kweli?
  • Kama mnakaa kwenye madaraka na kununua silaha kutoka kwa wageni na kuua watu wenu, je ninyi ni binadamu kweli?
  • Kama mnawaza kukaa madarakani mpaka mwisho wa maisha yetu, je ninyi ni binadamu kweli?
  • Ikiwa mnatumia maliasili ya nchi zenu kwa maendeleo ya familia zenu, je ninyi ni watu kweli?
  • lwapo hamjali kuweka miundo mbinu ya afya za watu wenu na badala yake mkiugua mnaenda kutibiwa nchi za nje, Je ninyi ni binadanu kweli?
  • Mtaheshimikaje katika mataifa yenu wakati mnapiga risasi raia wenu kama vile ni mchezo?
*Amemalizia kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika wataendelea kuwa kama wanyama hadi watakapo badili mtazamo wao na kuheshimu watu wanaowaongoza.

NB: Hadi kufikia hapo, unadhani Raisi Trump inatakiwa alaumie kutokana na tabia zake za kutukana waafrika, au labda anachosema ni kweli tukubaliane na yeye?
Una maoni gani kutokana na hotuba aliyoitoa huko kwenye kikao cha umoja wa mataifa? Hizi ni dharau za wazungu au kuna ukweli ndani yake?


Screenshot_20200518_071225.jpg
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,084
2,000
Waafrika tumeshindwa kujiongoza tumeshindwa kujitawala. Pana umuhimu wa kubinafsisha nafasi za juu za uongozi, mfano badala ya kuweka wanasiasa tuajiri watu toka nje bila kujali mataifa yao au rangi zao hata kwa contact ya miaka 5 mitano Ili watusaidie wananchi kutuletea maendeleo. Mfano waziri mkuu ajiri toka India, waziri wa kilimo toka israel, waziri wa uchumi toka ulaya, wa ujenzi na miundombinu weka mchina, wa nn weka Mkenya , Wa nn weka Msauzi Afrika hata Kama watalipwa pesa ndefu lkn tupate top cream watuleteee maendeleo tunayo taka wananchi na sio wayatakayo watawala.
Mtu anayeandika contact badala ya Contract ,

Ushauri wake sio wa kuzingatia , na the rest of the gang from Chadema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom