Rogojin The Idiot
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 2,704
- 3,035
Tuliosoma chuo hiki tulipata tabu sana. Kwa kiwango kikubwa tulisoma madesa. kwa kiwango kikubwa ilikuwa lazima tuhakikishe tunafaulu yale maswali ya madesa ili tusishindwe kupata degree.Chuo hiki kikongwe nchini kinatimiza miaka 60 toka kuanzisha Nini changamoto,mafanikio na mafunzo kwa watawala, maprofesa na wanafunzi?
**Cha ajabu chuo hiki pendwa hii. Hakuna midahalo, Wala kumbukizi
**RIP Prof Luhanga.
Kama tulielimika kiasi gani, hilo ni swali kila mmoja wetu anajiuliza kule aliko. Nategemea sasa hivi, wanafunzi watafundishwa kujiandaa kupambana na changamoto zinazozunguka mazingira yao na kuzipatia ufumbuzi. Zile Ego za kupambana kuhakikisha ufaulu unakuwa mdogo au watu wanakariri madesa halafu wanasema ndio wasomi, zitakuwa zimeisha sasa.
Kusema kweli, usomi uambatane na vitendo sio vyeti vikubwa na maneno mengi mengi kama madebe matupu