Miaka 60 bado tunajenga madarasa! Serikali ibadilike ianze kujenga shule za ufundi na killimo tokea ngazi ya Kata

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,800
8,781
Juzi tumefikisha miaka 60 ya Uhuru lakini hali bado inasikitisha sana. Serikali inaendelea na ujenzi wa madarasa ya shule za awali na sekondari. Nadhani ni kipindi sasa serikali inabidi igeukia elimu za ufundi kilimo na ufugaji.

Kila mwaka nchi inalia na upungufu wa madarasa sasa unajiuliza hao wanaomaliza hawatoi nafasi kwa wengine kuingia kwa kutumia madarasa hayo hayo.

Hizi pesa za UVIKO bora zingeelekezwa kutoa elimu ya ufundi kilimo na ufugaji kuliko haya madarasa ya awali ambayo kwa elimu ya sasa yanatoa fursa chache kwa Watanzania kujiajiri.
 
Ona akili za Watanzania! Badala ya kusema kuwa Serikali imeshindwa kudeliver kwa hiyo inapaswa kukaa pembeni na kupisha wenye uwezo na vision, wewe unadai kuwa ibadilike ianze kutengeneza shule za ufundi na Kilimo?

Serikali ambayo imeshindwa kutengeneza hizo shule za ufundi na kilimo ndani ya miaka 60 ya uhuru ije kuweza leo?!

Tanzania haiwezi kamwe kuendelea kwa sababu ya mindset kama hizi.Watu ni mbumbumbu kupindukia.Linapokuja suala la akili ni kama Taifa lina laana.
 
Juzi tumefikisha miaka 60 ya Uhuru lakini hali bado inasikitisha sana. Serikali inaendelea na ujenzi wa madarasa ya shule za awali na sekondari. Nadhani ni kipindi sasa serikali inabidi igeukia elimu za ufundi kilimo na ufugaji. Kila mwaka nchi inalia na upungufu wa madarasa sasa unajiuliza hao wanaomaliza hawatoi nafasi kwa wengine kuingia kwa kutumia madarasa hayo hayo.. hizi pesa za UVIKO bora zingeelekezwa kutoa elimu ya ufundi kilimo na ufugaji kuliko haya madarasa ya awali ambayo kwa elimu ya sasa yanatoa fursa chache kwa Watanzania kujiajiri.
Kwa hiyo shule za fundi na Kilimo hazina madarasa?
 
Ona akili za Watanzania!Badala ya kusema kuwa Serikali imeshindwa kudeliver kwa hiyo inapaswa kukaa pembeni na kupisha wenye uwezo na vision,wewe unadai kuwa ibadilike ianze kutengeneza shule za ufundi na Kilimo?

Serikali ambayo imeshindwa kutengeneza hizo shule za ufundi na kilimo ndani ya miaka 60 ya uhuru ije kuweza leo?!

Tanzania haiwezi kamwe kuendelea kwa sababu ya mindset kama hizi.Watu ni mbumbumbu kupindukia.Linapokuja suala la akili ni kama Taifa lina laana.
Sawa wewe na baba yako na mama yako ni wakongo hivyo sio wajinga
 
Juzi tumefikisha miaka 60 ya Uhuru lakini hali bado inasikitisha sana. Serikali inaendelea na ujenzi wa madarasa ya shule za awali na sekondari. Nadhani ni kipindi sasa serikali inabidi igeukia elimu za ufundi kilimo na ufugaji. Kila mwaka nchi inalia na upungufu wa madarasa sasa unajiuliza hao wanaomaliza hawatoi nafasi kwa wengine kuingia kwa kutumia madarasa hayo hayo.. hizi pesa za UVIKO bora zingeelekezwa kutoa elimu ya ufundi kilimo na ufugaji kuliko haya madarasa ya awali ambayo kwa elimu ya sasa yanatoa fursa chache kwa Watanzania kujiajiri.
Ufundi si tuna VETA?

Kilimo si tuna hadi SUA?

Twakwama wapi sisi watu weusi?
 
Ufundi si tuna VETA?

Kilimo si tuna hadi SUA?

Twakwama wapi sisi watu weusi?
Kwa akili zako lazima tukwame aisee. VETA na SUA zinajengwa kila mwaka!? Cha muhimu serikali isitishe ngojera za kujenga madarasa kila mwaka. Ijikite kwenye kujenga shule za ufundi na kilimo ambazo mtu hata akimaliza la saba hana haja ya kwenda VETA na SUA anaanza kujitegemea hao STD 7 na Form 4 wanaweza kujitegemea?
 
Inasikitisha sana

20211213_170355.jpg
 
Juzi tumefikisha miaka 60 ya Uhuru lakini hali bado inasikitisha sana. Serikali inaendelea na ujenzi wa madarasa ya shule za awali na sekondari. Nadhani ni kipindi sasa serikali inabidi igeukia elimu za ufundi kilimo na ufugaji. Kila mwaka nchi inalia na upungufu wa madarasa sasa unajiuliza hao wanaomaliza hawatoi nafasi kwa wengine kuingia kwa kutumia madarasa hayo hayo.. hizi pesa za UVIKO bora zingeelekezwa kutoa elimu ya ufundi kilimo na ufugaji kuliko haya madarasa ya awali ambayo kwa elimu ya sasa yanatoa fursa chache kwa Watanzania kujiajiri.
Chama Cha Mazuzu sio wasikivu. Wanataka kujenga makorokoro yao wyasioyo na tija kila mtaa
 
Kwa akili zako lazima tukwame aisee. VETA na SUA zinajengwa kila mwaka!? Cha muhimu serikali isitishe ngojera za kujenga madarasa kila mwaka. Ijikite kwenye kujenga shule za ufundi na kilimo ambazo mtu hata akimaliza la saba hana haja ya kwenda VETA na SUA anaanza kujitegemea hao STD 7 na Form 4 wanaweza kujitegemea?
Ili waimarike kinadharia na kivitendo std 7 na form 4 ni lazima waende angalau VETA au vyuo vya kilimo ambavyo tunavyo kama cha Uyole Mbeya.

Si kwa akili zangu ila kwa mawazo yangu.

Wahitimu wa VETA wapaswa kuwezeshwa kwa kuwa na access na mikopo nafuu kutoka kwenye mabenki ili waanzishe shughuli zao kihalali na watambulike na wawe na access na soko la ndani.

Wahitimu wa SUA vivyohivyo wanahitaji access ya mikopo ili kuanzisha kwa mfano hospitali ya wanyama na madawa ya mifugo.

Nitajie mhitimu hata mmoja mwenye veteriary Clinic ya maana ili nimpeleke chihuahua wangu.
 
Serikali niyakulaumiwa daily ila kwa hili wacha niitete lakini nitailaumu tena.
Ishu iliopo hapo ni population kuongezeka rapidly, raia mnazaliana sana yani sana, mpaka mwenda zake alishapiga promo ya kuatufyatuane alafu tatizo linakuja kua hili. Yani mwisho wa siku kila kitu kinakuja kuwa mzigo kwa Serikali madarasa kama Hivi pia kusahau walimu gap kubwa linazidi kuwepo, pia Kwenye matibabu kila leo hata dawa za Msaada uwa hazitoshi.
Wazungu kupiga promo ya ishu ya uzazi wa mpango si mashetani kama tunavyo aminishwa.
 
Sawa ww na baba yako na mama yako ni wakongo hivyo sio wajinga
Mimi,Mama yangu pamoja na Baba yangu kuwa Watanzania haiwezi kuzuia ukweli kusemwa.

Sasa unataka nisifie watanzania kinafiki kuwa ni watu smart sana kisa mimi pamoja na wazazi wangu ni Watanzania?
 
Juzi tumefikisha miaka 60 ya Uhuru lakini hali bado inasikitisha sana. Serikali inaendelea na ujenzi wa madarasa ya shule za awali na sekondari. Nadhani ni kipindi sasa serikali inabidi igeukia elimu za ufundi kilimo na ufugaji. Kila mwaka nchi inalia na upungufu wa madarasa sasa unajiuliza hao wanaomaliza hawatoi nafasi kwa wengine kuingia kwa kutumia madarasa hayo hayo.. hizi pesa za UVIKO bora zingeelekezwa kutoa elimu ya ufundi kilimo na ufugaji kuliko haya madarasa ya awali ambayo kwa elimu ya sasa yanatoa fursa chache kwa Watanzania kujiajiri.
Mjomba Tanzania hii haiwezi kubadilika we tuombe uzima tutafika miaka 70 ya uhuru bado vumbi litakua la kuzidi mjini!!
 
Back
Top Bottom