Miaka 6 ya uanachama wa JF: Mafanikio mbalimbali niliyopata

kitalembwa

JF-Expert Member
Jul 12, 2014
2,867
7,168
Wana bodi salaam!

Ni takribani miaka sita imepita tangu nijiunge rasmi jamii forum mnamo mwaka 2014 July.

JF imenipa connection kadhaa, na imenikutanisha na watu smart sana ambao Leo hii tumekuwa kama ndugu!

JF niliifahamu mwaka 2009-2010 lakini nilikuja kujiunga 2014, nilikuwa nashangaa watu wanacomment vipi kumbe ilitakiwa niwe member kwanza,,,nakumbuka simu yangu ya kwanza ni Nokia flani zilitamba sana zinaitwa express music ndo nilikuwa navinjari nayo enzi hizo 2010 na kuendelea, kitu opera mini unafungua unajimwaga.

Kipindi chote hicho jf ilikuwa tofauti na ya Sasa , Kuna watu wanaleta hoja nzito zenye mashiko watu wanakuja wanatoa maoni, kulikuwa hamna matusi ya hapa na pale Wala mihemko isiyokuwa na maana, watu wanabishana kwa hoja. Baadhi ya members waliokuwa hot kipindi hicho ni Watu 8, masai dada, Kiranga, Mshana Jr, Mbu, baadae wakaja kina lara 1, The Boss , Mara kina ONTARIO na project zao na wengineo!

Watu ninaofahamiana nao JF
1. Kuna mwanadada mmoja ambaye tulikwaruzana kwenye Uzi mmoja hivi, nakumbuka tulikuwa na hoja kinzani, ikafika hatua tunatoleana maneno mazito, tukahamia PM, tukafahamiana. Kadri siku zinavyokwenda tukazidi kufahamiana na kubadilishana namba, baadae nikaja kugundua Ni mtu mzima kiasi, Ni mtu ana maisha Yake ana NI mtu wa idara ya afya, anafanya kwenye taasisi kubwa tu hapa nchini.

Tukaendelea kuzoeana hadi nikaifahamu family yake, akanitambulisha kwa husband wake (Ni mtu ana nafasi nyeti wizarani huko), nikawa kama family friend. Mind that hapa nipo chuo, Mambo ya chuo akawa ananitoa kidogo kidogo, hata connection ya field ni yeye alinifanyia office flani ambayo nilikuwa napewa posho kidogo.

Tukawa tunashauriana na kuonana Mara moja moja, mda mwingine ananialika kwao weekends. Nikamaliza chuo, nikasota kidogo. Nikiri wazi hata hii job niko nafanya ni mume wake huyu dada alinipa direction, zile unaambiwa nenda kaonane na flani sehemu flani mwambie flan ndio amekuagiza.

Nikiri wamekuwa zaidi ya family kwangu. Kuna siku mwaka jana niliwaalika dinner sehem nzuri kidogo kuwashukuru. Ni watu poa mno!
Ila ukimuona huku jukwaani hayupo serious kivile, then ni mtu wa masihara lakn in life ni mtu smart sana.

2. Kuna mshkaji flani nilikutana nae mkoani ambaye tulifahamiana hapa hapa JF. Ni mtu anafanya halmashauri fulani hivi. Kuna kipindi nilitembelea huo mkoa, nilishukia kwake, nilikaa kama wiki (nilikuwa na shughuli zangu) alinipokea vzr yeye na familia yake. Kuanzia malazi, kula kunywa matembezi, kwa kweli niliinjoy. From there tumekuwa brothers , akija huu mkoa nilipo ni full kampan na off course wote ni watu wa moja moto moja baridi, pia connection tunapeana hapa na pale.

3. Kuna bidada mmoja nilikutana nae jukwaa la JF Doctor, kuna ndugu yangu alikuwa anasumbuliwa na UTI sasa nilivyoweka ile mada akawa amenifuata pPM kunielekeza namna/mahali anapoweza kwenda kupata tiba sahihi. From there tukawa tunawasiliana hapa na pale kumbe ni mtu anaishi mkoa nilipo, tukabadilishana namba na tumekuwa washikaji sana yani, ni dada flani yupo charming, ni mtu ana maisha yake, kaajiriwa pia kawekeza. Tunapeana kampan za hapa na pale! Tunashauriana mengi na sapoti za hapa na pale. Ukimwona huku jukwaani sasa utadhan ni mjinga flani, ni mtu wa masihara mda wote.

Hao watatu naweza kusema ni watu ambao kwa sasa tumekuwa kama ndugu.

Pia kwa kipindi chote cha miaka sita, makwazo yapo, kuna watu mnakwaruzana, matusi pengine kwa ajili ya hoja flani n.k ! Nipende kusema kuwa sijawahi kulimwa ban.

Majukwaa nayopenda
MMU
Spots
JF doctor
Siasa kidogo

Nimalize kwa kusema huu Ni mtandao wa kijamii, watu hatutumii identity zetu. Ukiutumia vzr utaona matunda yake. Humu kuna wahuni, matapeli, watu smart sana, viongozi kadhaa tupo nao humu.

Ni namna unavyoutumia huu mtandao, miaka/siku za hivi karibuni kumekuwa na id mpya pengine ni watoto wanajiunga humu ni mada zisoeleweka na matusi kisa kitu kidogo tu.

Hio ndio safari yangu ya JF kwa miaka 6.

Long live JF
 
Back
Top Bottom