Miaka 60 na CCM Madarakani: Ujinga, umaskini na maradhi bado havijaondoka

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,480
35,363
Tangu tupate Uhuru 1961 sasa ni miaka 59 . Lakini wale maadui 3 ambao ni ujinga, umaskini na maradhi bado wanawatesa Watanzania.

Je, tuendelee kuwapa kura CCM ili waendeleze mapambano waliyoyashindwa kwa miaka 59?

Tuwanyang'anye mamlaka kwakuwa wameshindwa kutokomeza ujinga, umaskini na maradhi?

Nimefanya kazi mgodi wa GGM kama security officer, nimefanya kazi mgodi Mkubwa wa dhahabu Bulyanhulu as security officer.

Nimefanya kazi Hifadhi ya Serengeti FOUR SEASONS HOTEL kama security officer pia. Kote niliacha mwenyewe tu. Nilikuwa naangalia maslahi namwaga manyanga na CV yangu kwenye security issue iko poa, nikifanya interview na Wazungu wasiopenda udhalimu na rushwa wananikubali sana.

Wanalipa vizuri kuliko hata serikalini. Sasa niko serikalini nako nilitaka kuacha June - July 2020 ingawa nimeongeza muda mbele kwasababu ya kuondolewa kwa fao halali la kujitoa psssf

Turudi kwenye mada, utajiri ulioko huko kwenye Hifadhi za taifa ni mkubwa, utajiri ulioko huko kwenye migodi ya dhahabu na madini mingine ya madini ni mkubwa sana.

Maajabu ni kwamba umaskini, ufukara, ujinga na maradhi bado vinawatesa Watanzania.

Lakini bado CCM wanajisifu wamewatendea mema Watanzania. Kuendelea kuwapa mamlaka CCM ni kutokujitambua.
 
Tahadhari Sichangii kwa itikadi za kisiasa bali kama mwafrica.

Swali;
Nchi gani Africa ambayo haiongozwi na ccm imeendelea kuliko nchi yoyote Africa na ambayo inaweza kulinganishwa na nchi mojawapo nje ya Africa...?

Nchi gani ndani ya Africa ambayo haiongozwi na ccm imefanikiwa kuondoa Ujinga, maradhi na umasikini kuliko nchi nyingine yoyote ndani ya africa?

Nijibu tafadhali.
 
Hizo nchi zingine zinatawaliwa na CCM?... Jibu hoja.
Miaka 59 imetosha wapewe chama kingine tuone nao watafanya nn...
 
wapi nimesema wasipewe chama kingine?
Nimesema sijachangia kwa itikadi za kisiasa hivyo soma kwa makini uelewe swali kabla kujibu swali kwa hisia na mitazamo binafsi.
Hizo nchi zingine zinatawaliwa na CCM?... Jibu hoja.
Wapi nimesema zinatawaliwa na ccm?
Hebu soma tena kwa makini na uelewe nilichouliza.
 
Umasikini, maradhi na ujinga kuondoka ndani ya utawala wa CCM ni muujiza mkuu. CCM inategemea zaidi ujinga kama mtaji wake muhimu kisiasa. Bila ujinga ccm haiwezi kuwepo. Hivyo lazima iuendeleze ujinga kwa gharama zote.
 
Kufaidi keki ya taifa ni suala la serikali inayotawala kuhakikisha maendeleo yanakuwa diversified. Hii ni kuhakikisha kuwa kila sehemu ya nchi yetu inapata maendeleo kwa usawa na kwa uwiano unaotakiwa bila ubaguzi.

Leo hii Ccm baada ya kutawala kwa miaka 60 hali ya maisha ya wananchi wa kawaida ni mbaya na inatia huruma.

Ccm peke yao ndio wanafaidi matunda ya taifa letu, huku wananchi wa kawaida tukiteseka. Kila kitu ni kwa wanaCcm vigogo ambao wanakula keki ya taifa kama mali yao.

Ili kukabiliana na huu uonevu wa Ccm tunakiwa kama watanzania kufanya mapinduzi ndani ya mioyo yetu na kuikataa Ccm. Mapinduzi sio kushika bunduki na kuondoa madhalimu bali ni kubadilika na kuwakataa kwa kila namna.
 
Kufaidi keki ya taifa ni suala.ya serikali inayotawala kuhakikisha maendeleo yanakuwa diversified. Hii ni kuhakikisha kuwa kila sehemu ya nchi yetu inapata maendeleo kwa usawa na kwa uwiano unaotakiwa bila ubaguzi.

Leo hii Ccm baada ya kutawala kwa miaka 60 hali ya maisha ya wananchi wa kawaida ni mbaya na inatia huruma.

Ccm peke yao ndio wanafaidi matunda ya taifa letu, huku wananchi wa kawaida tukiteseka. Kila kitu ni kwa wanaCcm vigogo ambao wanakula keki ya taifa kama mali yao.

Ili kukabiliana na huu uonevu wa Ccm tunakiwq kama watanzania kufanya mapinduzi ndani ya mioyo yetu na kuikataa Ccm. Mapinduzi sio kushika bunduki na kuondoa madhalimu bali ni kubadilika na kuwakataa kwa kila namna.
Naunga mkono hoja
 
Tuna tatizo kubwa sana kama Taifa kwasasa nchi yetu zaidi ya 60 millions lkn ni kikundi kidogo sana cha watu ambao wanaweza kuzungumza mambo mapana na yenye maslahi mapana
 
Kufaidi keki ya taifa ni suala la serikali inayotawala kuhakikisha maendeleo yanakuwa diversified. Hii ni kuhakikisha kuwa kila sehemu ya nchi yetu inapata maendeleo kwa usawa na kwa uwiano unaotakiwa bila ubaguzi.

Leo hii Ccm baada ya kutawala kwa miaka 60 hali ya maisha ya wananchi wa kawaida ni mbaya na inatia huruma.

Ccm peke yao ndio wanafaidi matunda ya taifa letu, huku wananchi wa kawaida tukiteseka. Kila kitu ni kwa wanaCcm vigogo ambao wanakula keki ya taifa kama mali yao.

Ili kukabiliana na huu uonevu wa Ccm tunakiwa kama watanzania kufanya mapinduzi ndani ya mioyo yetu na kuikataa Ccm. Mapinduzi sio kushika bunduki na kuondoa madhalimu bali ni kubadilika na kuwakataa kwa kila namna.
Sukuma gang umepokonywa keki unabwabwaja miaka 5 ya nyuma full kumsifia hayati leo umepokonywa keki unalia?acha usen**** kama unabisha ntascreenshort jumbe zako nizitume humu kama hukuwa praise team
 
Kufaidi keki ya taifa ni suala la serikali inayotawala kuhakikisha maendeleo yanakuwa diversified. Hii ni kuhakikisha kuwa kila sehemu ya nchi yetu inapata maendeleo kwa usawa na kwa uwiano unaotakiwa bila ubaguzi.

Leo hii Ccm baada ya kutawala kwa miaka 60 hali ya maisha ya wananchi wa kawaida ni mbaya na inatia huruma.

Ccm peke yao ndio wanafaidi matunda ya taifa letu, huku wananchi wa kawaida tukiteseka. Kila kitu ni kwa wanaCcm vigogo ambao wanakula keki ya taifa kama mali yao.

Ili kukabiliana na huu uonevu wa Ccm tunakiwa kama watanzania kufanya mapinduzi ndani ya mioyo yetu na kuikataa Ccm. Mapinduzi sio kushika bunduki na kuondoa madhalimu bali ni kubadilika na kuwakataa kwa kila namna.
Ni kweli kabisa na .apinduzi yetu wala sio ya vita na mitutu. Katiba Bora na Mpya ndio mwarobaini.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom