Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
Zitto Kabwe
Tarehe 9 Desemba 1961 Tanganyika iliingia katika Jumuiya ya Mataifa huru duniani baada ya kupata Uhuru wake kutoka Himaya ya Uingereza. Muda mfupi baadaye Tanganyika ikawa mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Safari ya kwanza ya nje ya Nchi ya Mwalimu Julius Nyerere kama Mkuu wa Serikali ilikuwa tarehe 14 Desemba 1961 kwenda New York kwa ajili ya kupokea uanachama wa Tanganyika katika Umoja wa Mataifa.Siku ya Uhuru Mwalimu Nyerere alitoa hotuba fupi sana ya kupokea ‘instruments of independence’ kutoka kwa mwakilishi wa Malkia wa Uingereza. Kabla ya hapo, akiwa Rais wa TANU, alitoa salamu za Uhuru ambapo pamoja na mambo mengine alieleza maana ya Uhuru ambao Watanganyika waliupigania. Aliwakumbusha wanachama wa TANU kuwa “ muda wote ambao tumekuwa tukipambana kupana Uhuru wa Nchi yetu, tuliweka msingi kuwa Imani yetu ni usawa na heshima ya utu kwa watu wote na kuheshimu tangazo la haki za binaadam”. Alisisitiza kwa wana TANU kuwa, “hakuna rangi, dini, kabila, au kingine chochote kile kinachoweza kumwondolea mtu haki yake ya kuwa sawa mbele ya Jamii yake”. Aliwaambia wana TANU kuwa ni lazima kuendelea kupambana na “ umasikini, ujinga na maradhi” ili kujenga Jamii ya watu waliosawa na huru. Katika mazingira ya sasa unaweza kusema kuwa hata kuwa mwanachama wa chama cha Siasa tofauti na kilichopo madarakani hakuwezi kukuondolea haki yako kama Mtanzania mwengine yeyote. Hii ndio maana ya Uhuru ambao waasisi wan chi yetu waliamini.
Hata hivyo, utapata maana ya Uhuru kwa Wazee wetu kwa mapana Zaidi katika Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya Desemba 10, 1962 wakati Mwalimu Nyerere anahutubia Taifa kama Rais wa Jamhuri ya Tanganyika. Ikumbukwe Mwalimu alijiuzulu Uwaziri Mkuu na kutumia mwaka mzima kujenga TANU kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanganyika. Katika Hotuba hii ambayo inapaswa kusomwa na kila Mtanzania kuanzia Rais wa Tanzania mpaka mwanachi wa kawaida, Mwalimu Nyerere anaeleza maana ya Uhuru ambao waliupigania yeye pamoja na wenzake akiwemo Hamza Mwapachu, AbdulWahid Sykes na wadogo zake, Denis Phombeah, Oscar Kambona, Rashidi Kawawa, Dossa Aziz, John Rupia, Titi Mohammed, Andrew Tibandebage, Vedastus Kyaruzi, Steven Mhando na wengine wengi ambao kwa hakika hawathaminiwi wala kuenziwa. Sina hakika kama Nchi hii hata kuna Mtaa au Barabara iliyopewa jina la Mtu kama Hamza Mwapachu au Vedastus Kyaruzi kuenzi uasisi wao wa Taifa letu.
Katika Hotuba hii ya 10/12/1962 Mwalimu Nyerere anasema “Uhuru tulioupigania sio tu uhuru dhidi ya mkoloni; tulitaka uhuru wa watu wetu binafsi kufanya mambo yao na kujitafutia kipato chao kwa ajili ya maisha yao yenye Utu”. Aliendelea kusema “ tunataka kila raia awe sawa na mwengine na hakuna ubaguzi wowote”. Maneno haya ya Mwalimu yanaweza kutafsiri maana ya Uhuru kwa uendelevu kwani ni rahisi kupima kama kila mwananchi ana haki sawa mbele ya Jamii, haswa bila kujali itikadi za kisiasa. Lakini tafsiri hii ya Uhuru ina maana hivi sasa? Watanzania wa leo, ( baada ya Nchi mbili zenye hadhi sawa mbele ya sharia ya kimataifa kuungana – Tanganyika na Zanzibar ), wana tafsiri Uhuru sawa na Watanzania wa miaka ya 1960?
Takwimu rasmi za Serikali zinaonyesha kuwa ni 3% tu ya Watanzania wanaoishi walikuwepo mwaka 1961 wakati Tanganyika inapata Uhuru. Watanzania wengi, 71%, hawakuwa wamezaliwa mwaka 1995 wakati wa Uchaguzi wa kwanza chini ya Demokrasia ya Vyama vingi. Asilimia 65 ya Watanzania wanaoishi sasa wala hawakuwahi kumwona Mwalimu Nyerere akiwa hai. Kwa Watanzania hawa, Uhuru wa Tanganyika una maana gani kwao? Ni Uhuru wa kumtoa Mkoloni na kupandisha Bendera ya Tanganyika tu au ni Uhuru wa kuondokana na Umasikini, Ujinga na maradhi?
Kuna baadhi ya watu wanajenga hoja kuwa Uhuru wetu ni kujenga Barabara, Reli, vituo vya kufua Umeme, madaraja nk. Lakini Mkoloni alifanya haya. Mkoloni Mjerumani alijenga Reli ya Kati kutoka Pwani mpaka Bara ( Dar es Salaam – Kigoma ) na kutoka Tanga mpaka Dar es Salaam. Mkoloni mwingereza akamalizia Reli mpaka Mwanza na Mpaka Moshi na Arusha. Wakoloni walijenga mashule ambayo kina Mwalimu Nyerere walisoma n ahata barabara mbalimbali na Mahospitali. Lakini haya ‘maendeleo’ aliyoleta Mkoloni hayakuwafanya Wazee wetu waseme “ sasa Uhuru wa nini wakati barabara zimejengwa, Shule zipo n ahata Reli zimejengwa”. Wazee wetu walitaka Uhuru wa wananchi kujiamulia wenyewe mambo yao. Uhuru wa kuzungumza watakacho. Uhuru wa kuendesha maisha yao bila hofu ya kukamatwa, kuuwawa au kushtakiwa na kufungwa. Kina Nyerere na Hamza Mwapachu hawakujali miundombinu inayojengwa kwani wao walitaka kujenga Taifa.
Mwalimu Nyerere alisema hili vizuri wakati wa Hotuba ile ya 10 Desemba, 2019. Aliwaambia Watanganyika “kujenga nchi sio kujenga barabara za lami, majengo makubwa na mahoteli ya kifahari. Nchi inaweza kuwa na hayo yote lakini isiheshimike. Kujenga Taifa ni kujenga Watu”. Wazee wetu hawa walijaribu kweli kujenga Taifa kwa kujenga watu. Tanganyika na baadaye Tanzania ilikuwa inaheshimika duniani sio kwa sababu ya utajiri wake wa madini nk bali kwa Utu wa watu wake, tabia za watu wake na misingi imara ya kutetea haki za watu waliokuwa wanaonewa. Leo Tanzania bado ni Taifa lenye heshima hii?
Uhuru waweza kuwa na maana tofauti kabisa kwa 71% ya Watanzania ambao wamezaliwa baada ya mwaka 1995. Uhuru kwao ni Uhuru dhidi ya Umasikini, kulisha familia zao na kuepukana na njaa. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, 49% ya Watanzania wanaishi kwenye dimbwi la umasikini kwani hawana uwezo wa kutumia shilingi 5000 kwa siku. Iwapo kuna miaka 58 ya Uhuru lakini nusu ya Wananchi hawawezi kula mlo mmoja kwa siku Uhuru una maana gani? Wenzetu ambao tulipata Uhuru wakati mmoja, kama Malaysia, ni 3% tu ya watu wao wanaitwa masikini.
Uhuru kwa 71% ya Watanzania ni Uhuru wa usalama wao. Kwamba waweze kuishi bila kuogopa kuwa wanaweza kutekwa na kupotezwa. Matukio ya Utekaji na Mauaji ni miongoni mwa masuala makubwa manne ambayo Watanzania wanasema yanawaumiza mno. Utafiti uliofanywa twaweza unaonyesha kuwa 54% ya wananchi, pamoja na mambo mengine, wanaumizwa sana na 1) Ukosefu wa Ajira, 2) kuminywa kwa Uhuru wa watu na 3) Utekaji na Mauaji. Hii ina maana kuwa kwa Watanzania wa sasa Uhuru kwao maana yake ni kuwa na ajira, kuwa na haki ya Uhuru wa mawazo na kuwa na haki ya uhuru wa usalama wake.
Ni Dhahiri kuwa maana ya Uhuru kwa Watanganyika wa miaka ya sitini ni tofauti na ile ya Watanzania wa kizazi cha demokrasia. Hivyo kama watu hawana uhuru wa kutoa mawazo yao, kukosoa Serikali yao, kujipatia ajira atakayo, kupata na kutoa habari na Uhuru dhidi ya umasikini, kwanini washerehekee siku ya Uhuru? Kwa wale 3% siku hii inaweza kuwa na maana kubwa maana waliona mkoloni mzungu akitoka na mweusi akijitawala. Sio kwa Watanzania wengi.
Mtanzania aliyezaliwa mwaka 1995 ambaye anaona utawala wa chama kile kile, chaguzi zikiibwa kila wakati wa uchaguzi, magazeti yakifungiwa, waandishi wa habari wakipotea kwa miaka 2 na wengine kufungwa jela kwa makosa ya kubambikiwa, wabunge wakifunguliwa mashtaka ya uongo na wengine kutwangwa risasi, wavuvi wakichomewa nyavu na kufanywa masikini, wakulima wakichukuliwa mazao yao kwa nguvu na majeshi na kutolipwa kwa miaka 2, Wafanyabiashara kubambikiwa makesi na kuporwa fedha zao za marejesho ya kodi, Wafanyakazi hawaongezewi mishahara kwa miaka minne licha ya gharama za maisha kupanda kiasi cha debe la mahindi kuwa ghali kuliko mfuko wa saruji wa 50kg, Watanzania 2.7 milioni wamedumbukiwa kwenye umasikini kati ya 2016-2018, Wanasiasa wakizuiwa kufanya mikutano kuzungumza na wananchi kwa miaka minne na mengine lukuki, anajiuliza Uhuru huu maana yake nini?