Miaka 58 ya Muungano, nafasi ya Rais Samia kuzimaliza kero.

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,239
Happy Muungano day naomba nitumie fursa hii kuwa kumbusha ndugu Ndugu Zangu Wanzanzibar kwa kipindi chote cha miaka 58 ya Muungano imekuwa ngumu kwao ukweli ulio wazi ni km wamekuwa mateka ndani ya Muungano ila Wakati ni Huu wa kuweka mambo Sawa wote tunajua Fursa iliyopatikana naweza kusema bahati ya mtende wote tunajua kama sio kifo Mh Magufuli kulikuwa hakuna Dalili siku yeyote Mzanzibar atakuja kuongoza Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Narudia tena kuwaomba na kuwa kumbusha ndugu zangu Wazanzibar Kero za Muungano wakati ndio huu wa kuweka mambo Sawa mkipoteza nafasi hii itabidi msubiri tena kwa miaka 58 mingine nami Kijana wa Leo Hamidu Bin Rubawa Cape Town South Africa...
IMG_20220426_092839.jpg
 
Miaka 58 ya Muungano, nafasi ya Rais Samia kuzimaliza kero.
Viongozi waliomfuatia Sheikh Karume walikuwa na udhaifu wa kupigania marekebisho ya Muungano na kuondoa kero zilizokuweko na ambazo zikiongezwa kwa makusudi na upande wa pili.
Sababu inaweza kuwa ni kuyojiamini au kuhofia yaliomfika Mzee Aboud Jumbe Mwinyi 1985 yasiwafike na wao. Kwao uongozi ulikuwa ni Kulinda masilahi binafsi.
Wakirudi nyuma pia wakiangalia msukosuko wa Dr Salim Amour alipoambiwa alipotaka Zanzibar ijiunge na Jumuiya ya nchi za Kiislamu OIC.
Lakini Salmin pamoja na kuzidiwa nguvu alikuwa na ujasiri wa kusema "msitikise kibiriti. "
Bahati mbaya aifikiri ataungwa mkono na Wazanzibari lakini walimuangusha. Tukumbuke Rais wa Muungano wakati huo alikuwa Ali Hassan Mwinyi aliyevaa Joho lenye luvalika pande zote mbili.
Mzee Mwinyi hakuzaliwa Zanzibar bali Mkuranga. Alipokelewa Zanzibar kusomeshwa na kuelewa bila chuki. Alikubalika kama wengine. Alipewa nafasi mpaka kwenda Uingereza kwa masomo ya juu. Lakini slipopata Urais wa Muungano akakiuka haki na usawa wa dola mbili huru. Akawa na uwoga na kulinda masilahi yake, masilahi ambayo leo yamempa pia Urais mwanawe Dr Hussein kuwa Rais visiwani. Mwinyi Baba amekiri katika kitabu juu ya maisha yake kuwa kwao ni Mkuranga na mwanawe Dr Hussein aliwahi kwa mara ya kwanza kugombea ubunge wa Mkuranga na akashinda.
Muungano bado una matatizo na kuondoa kero hizo kunahitajika ujasiri wa Wazanzibari wenyewe.
Rais aliyetangulia Maguli aliwadhalilisha alipounda baraza la mawaziri bila hata waziri mmoja kutoka Zanzibar, kwa mara ya kwanza katika historia ya Muungano. Inawezekana akijaribu kujenga msingi wa ile dhana inayozungumzwa kujaribu kuimeza Zanzibar na kuwa na serikali moja nayo ikiwa mkoa.
Mama Samia ameifuta dhana hiyo kwa kuunda Baraza ambalo takriban lina uwakilishi sawa wa pande zote mbili za Muungano. Nakukumbusha hadharani kwamba Tanzania imetoka ana Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wazanzibari na Watanzania bara wapenda haki wana kila sababu kumuunga mkono Rais Samia katika azma yake ya kuudumisha Muungano huu kwa njia ya haki na usawa. Mpaka sasa amefanya mengi kiasi ili lakini kufanya zaidi anahitaji uungaji mkono wa Wazanzibari kwani ni mwanasiasa wao tena mzaliwa wa Zanzibar mwenye kuiongoza taifa la Tanzania.
Wahafidhina wa chama tawala wa pande zote mbili, alau kwa sasa wamevunjwa nguvu lakini bado wapo. Nafasi ya kujaribu kumuweka Muungano huu kuwa rehani watakuwa nayo pindi Mama Samia atalega lega. Ajenda yao ilikuwa ni pamoja na kuwa na mtu kama Dr Mwinyi visiwani ambapo mpaka sasa kuna hoja kwamba hakuzaliwa Zanzibar.
Muungano huu ni wa aina yake lakini utastahiki kutukuzwa tu kikamilifu zitakapoondoshwa kero kwa manufaa ya Zanzibar na Tanganyika. Mama Samia ni Rais hadi 2025 na panapo uhai ana nafasi ya kuiongoza Tanzania hadi 2030.Suala la kuondoa kero zilizobaki ni muhimu katika muda wake wa uongozi. Kama sivyo kama nilivyosema awali Zanzibar Isubiri miaka mengine 58 kupata haki inayostahili.
View attachment 2201179
 
Kero kamaliza kwa kuwa raisi wa kwanza kutohudhuria sherehe za muungano,mama anaupiga mwingi
 
Back
Top Bottom