Miaka 54 ya uhuru haki ya matokeo ya urais haihojiwi mahakamani! Huu ni ukoloni!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Tanzania sasa ina umri mkubwa sana! Ni umri wa kiutu uzima kabisa na ni umri wa kung'amua ni lipi jema na ni lipi baya katika nchi yetu bila kusaidiwa! Tanzania sasa ni mtu mzima!

Ni ajabu sana kuona Tanzania mtu akishatangazwa ra rais na tume ya uchaguzi na mambo yanaisha! Hakuna kuhoji mahali popote pale! Kulikuwa na haja gani kudai uhuru kama hatujapevuka kiasi cha kusuluhisha vijitatizo vidogo kama hivyo? Hivi kweli tunathubutu kusubiri demokrasia Tanzania? Anayasema kuwa Tanzania ina demokrasia huyo ni mjinga!

Tanzania kama tumeshindwa kuelewa jambo muhimu kama hilo na kulitilia maana ni, hakika tupo kwenye mfumo halisi wa kikoloni! CCM inaikandamiza Tanzania kikoloni na ina sifa zote za kuwa hivyo!

Sasa ni dhahiri kuwa tuishiwe uvumilivu na tudai mambo muhimu kama hayo kwa nguvu! Tuonyeshe kuchoshwa na ujinga huu wa CCM!
 
Back
Top Bottom