Miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika: Ujinga, Maradhi na Umasikini Unatoweka ama Unaongezeka?

ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Wakati Tanganyika inapata uhuru wake, Mwl JKN alibainisha kuwa maadui wetu wakuu watanzania ni UJINGA, MARADHI na UMASIKINI. katika kipindi cha utawala wake alipigana vilivyo kutokome hawa maadui wa taifa hili, Mathalan:- Kufikia mwaka 1980 Tanzania ilikuwa na wataalam wa kila aina, idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ilikuwa ndogo sana, elimu ya watu wazima ilitolewa kwa wote bila ya malipo! Alikataa katakata kusaini mikataba ya kinyonyaji, alisema kuwa siku watanzania wakiwa na uwezo watachimba madini yao kwa faida ya watanzania wote!... Afya ya jamii ilipewa kipaumbele Enzi za mwalimu, kila kijiji kilikuwa na zahanati yenye madawa na vifaa, Huduma ya maji safi na salama ilipatikana. Nyerere alijitahidi sana kutokomeza umasikini, vyama vya ushirika vilikuwa imara, viwanda vingi alivianzisha na kuvisimamia, kilimo kilishika hatamu kwa Tanzania kuongoza export ya kahawa, tumbaku, mkonge, korosho, karafuu, pamba...uchumi wa Tanzania ulisua sua baada ya kuwekewa vikwazo baridi na kupiganishwa vita na Idd amin! vyote hivi vilikuwa ni mpango mkakati wa mabeberu wa dunia hii... Miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika chini ya serikali ya CCM hali ikoje? figure za CPI na GDP vinaendana na uhalisia wa maisha ya wananchi wa kawaida? UJINGA, MARADHI na UMASIKINI status yake ikoje?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom