Miaka 52 ya Uhuru: Maadui wetu wamerudi nyuma kiasi gani?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,176
25,446
Kesho tarehe 9/12/2013, Tanzania Bara-iliyokuwa Tanganyika itasherehekea miaka 52 ya Uhuru wae.Tanganyika ilipata Uhuru wake mnamo tarehe 9/12/1961 kutoka kwa Waingereza waliokuwa wakiikalia nchi yetu hii pendwa kwa uangalizi ulioidhinishwa na Umoja wa Mataifa.

Rais wa kwanza wa Tanganyika huru alikuwa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Akiiongoza Serikali mpya huru,Hayati Mwalimu Nyerere alitangaza maadui wa Taifa hili: umaskini,ujinga na maradhi. Mwalimu Nyerere na Serikali yote waliamini kuwa kama nchi itapambana na maadui hawa,basi nchi itakuwa salama.

Umaskini ni kipato na hadhi ya maisha ya mtanganyika(sasa mtanzania) kuhusu mavazi,chakula na malazi. Na hata umaskini wa kiakili. Umaskini ulikuwa ni ajenda ya tangu Nyerere kutokomezwa. Kama nchi ambayo tayari imeshakuwa na marais wanne,tumefikia wapi? Vifaru vyetu vya kinchi vimemvurumisha adui huyu kwa umbali gani kurudi nyuma kuelekea kumtokomeza?

Ujinga ni kukosa maarifa;kukosa elimu. Kuhusu elimu, Serikali zote tangu uhuru zimekuwa zikipambana na adui huyu. Pamoja na kujenga shule,kufunza waalimu,wakufunzi na wahadhiri na kuandikisha wanafunzi wengi,tumefanmikiwa kwa kiasi gani? Elimu yetu imeboreka au imeporomoka? Nini kifanyike? Adui huyu tunamzidi au anatuzidi nguvu?

Maradhi ni adui mwingine. Ni ukosefu wa huduma bora za kiafya kupitia Hospitali,Zahanati na Vituo vya Afya. Na pia, maradhi husababishwa na kukosekana kwa chakula bora kwa wananchi na mazingira safi. Maradhi yaweza pia kuwa ya kiakili. MARADHI NI MARADHI TU. Adui huyu vipi? Mabomu yetu kama nchi yamemuangamiza adui huyu kwa kiasi gani?

Kama nchi, tunapaswa kutafakari suala hili ili tusherehekee mafanikio. Sherehe hunoga kwenye furaha! Karibuni kwa mjadala Wakuu...
 
Ndugu yangu Petro Mselewa tulikuwa tunaenda vizuri kama taifa lakini kuna mahali tulijikwaa na kuanza kuporomoka. Tunahitaji mdahalo mpana usiokuwa wa kiitikadi ambako tutajadili objectively tulikotoka tulipo na kule tunakotaka kwenda kama taifa.

Yapo mambo mengi tuliyoyakosea lazima kama taifa tukubali tulikosea na hii iwe bi-partisan na turekebishe sasa ili hasara isiwe kubwa zaidi!

Sera yetu ya madini haiko sawa na sijui kwanini hatuangalii uwezekano wa kuwa na win win policy kwenye eneo hili! either tunachimba sasa au tunaacha hizo raslimali ardhini mpaka tutakapokuwa na uhakika wa kufaidika nazo.

Suala la elimu ni jambo ambalo tumelichezea sana tunapaswa kuliweka sawa kwa kuangalia tulipojikwaa ili makosa tuliyoyafanya yasijirudie tena.

Kuhusu kama tusherehekee nafikiri ni muhimu kusherehekea lakini pia ku-reflect kama taifa kama hapa tulipofika panafanana na muda tuliochukua wa miaka 52! Je,kasi yetu ni nzuri?
 
Ni kweli Mkuu.Lakini kasi yetu ya mapigano dhidi ya maadui wetu si nzuri.
 
Hivi ni uhuru gani unao sherehekewa wakati kila kukicha pande zote za tz tuna kimbizana na mabomu inge kuwa amri yangu hizo gharama zhngesambazwa kwa wasio jiweza
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom