Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
JUMAPILI ya Aprili 26, 1964, saa 4.00 asubuhi ilileta mabadiliko makubwa kwa mataifa mawili – Tanganyika na Zanzibar – kwani ndiyo siku nchi hizo ziliunganishwa na kuzaa Muungano wa aina yake ambao leo umetimiza miaka 52.
Ni siku ambayo Mwenyekiti wa TANU Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mwenyekiti wa Afro-Shiraz Party (ASP) Sheikh Abeid Amani Karume walikutana mjini Dar es Salaam na kusaini hati ya makubaliano ya kuziunganisha nchi zao.
Muungano huo ulifikiriwa kwa takribani miezi mitatu na siku 24 tu tangu yalipofanyika Mapinduzi ya kuung'oa utawala dhalimu wa Kisultani Visiwani Zanzibar Januari 12, 1964. Kabla ya kutiwa saini, wakuu hao wa nchi mbili walikuwa wamefanya mazungumzo ...http://www.fikrapevu.com/miaka-52-ya-muungano-katiba-mpya-katika-nuru-mpya-ya-uongozi/