Miaka 52 baada ya uhuru: Tunahitaji mdahalo wa wazi kuhusu mgawanyo wa fursa na raslimali za taifa


N

ngika

Member
Joined
Oct 19, 2012
Messages
18
Likes
0
Points
3
N

ngika

Member
Joined Oct 19, 2012
18 0 3
Kwa haraka haraka hoja hii yaweza chukuliwa kama ukabila lakini kuna manung,uniko kwa baadhi ya watanzania kuwa raslimali za taifa tokea uhuru zimeendelea kuwa chini ya wachaga ,wahaya na wanyakyusa na huku jamii zingine kama maasai na wengineo wameendelea kuwa na thamani sawa na wanyama wa tarangile na ngorongoro. Wakati wa mwalimu nyerere kulikuwa na nia ya dhati ya kutokomeza matabaka na ukabila lakini kwa sasa hili limesahaulika.wakati mwingine waweza lisikia katika hotuba za mwalimu nyerere japo utekelezaji haupo. Ili kudumisha umoja na mshikamano wa taifa ipo haja ya kuhakikisha kuwa kila kabila nchi hii lina nafasi sawa katika mgawanyo wa fursa na raslimali za taifa.
 

Forum statistics

Threads 1,263,713
Members 486,018
Posts 30,161,077