Miaka 52 baada ya uhuru tujadili kwa upana uwiano wa kugawana fursa na raslimali za nchi za nchi


N

ngika

Member
Joined
Oct 19, 2012
Messages
18
Points
20
N

ngika

Member
Joined Oct 19, 2012
18 20
Inaweza elezwa au kuonekana kama ni ukabila au hata ubaguzi lakini tayari kuna minong'ono na manung'uniko kwa watanzania kuwa tokea uhuru na hadi sasa raslimali na fursa za nchi hii zimeendelea kuwa chini ya makabila machache tu ya nchi hii, na hasa WACHAGA, WAHAYA na WANYAKYUSA.

Baadhi ya makabila kama wamasai hadi leo wanaonekana kuwa na hadhi sawa na wanyama walioko ngorongoro na tarangile na kwingineko na hata wakati mwingine kuchukuliwa kama vivutio vya watalii. Hali si tofauti sana na makabila mengine katika nchi hii. Mbaya zaidi hata ajira zinatolewa kwa mtindo uleule wa kikabila.

Ipo haja ya kuwa na mfumo ambao utaangalia namna ya kunufaisha makabila yote ya nchi hii, waasisi walijaribu kufanya hilo lakini kadri siku zinavyosonga ukabila na hata matabaka yameachwa kukua kwa kasi na hiyo kutishia umoja na mshikamano wa taifa.
Umoja na mshikamano utadumu pale tu amabapo kila mtanzania anaona ana nafasi sawa na pia hakuna ukabila au ukanda unaohodhi raslimali na fursa za nchi kuliko mwingine na mjadala kuhusu kuondoa tofauti kama hizi usichukuliwe kuwa ni ukabila.
 

Forum statistics

Threads 1,283,909
Members 493,869
Posts 30,805,755
Top