Miaka 500 yatimia tangu Kanisa Katoliki kumtenga Martin Luther, mwanzilishi wa Kanisa la Kilutheri

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Leo tunatimiza miaka 500 tangu Kanisa Katoliki lilipotoa waraka wa Kipapa wa kumfukuza aliyekuwa padre wake Martin Luther Januari 3, 1521. Papa alifikia uamuzi huo baada ya miaka minne ya minyukano kati ya kanisa na Luther. Luther alikuwa padre na mtawa wa kanisa katoliki kupitia shirika la Waagustino aliyepadrishwa mwaka 1507.

Alikuwa msomi na mhadhiri wa Taalimungu. Mwandishi mahiri. Mtunzi wa muziki na mtu maarufu wa mabadiliko. Amri hiyo iliyotolewa na papa hujulikana kwa lugha ya kilatin kama “Decet Romanum Pontificem” (It Pleases the Roman Pontiff) ndiyo iliyomfukuzisha Martin.

Chanzo cha kutengwa kwake
Kanisa katoliki katika kupitia kipindi kigumu cha uchumi wake, kilimfanya kiongozi wa wakati huo Papa Leo X kuendelea kutafuta vyanzo vipya vya kuongeza mapato ya kanisa. Kulikuwa na mambo kadhaa yaliyopelekea kuhitajika kwa fedha katika utawala wa papa huyu, mojawapo ikiwa ni hitaji kubwa la kuendelea kujenga kanisa la Mt Petro pale Roma achilia mbali hoja ya Wafaransa kuitawala Italia. Chanzo kimojawapo muhimu kilikuwa ni kulipia ondoleo la dhambi.

Wakati wa utawala wa papa Julius wa Pili, dhambi zilikuwa zinaondolewa kwa kulipia malipizi ya fedha zilizosaidia kujenga kanisa la Mt Petro. Papa Leo X ambaye alikuwa na haja kubwa ya kuendelea kwa ujenzi wa kanisa hilo, nae aliendeleza kile kilichoanzishwa na mtangulizi wake,ili kukusanya fedha zaidi za kujenga kanisa hilo. Kwa sababu za kutokufahamika sana ulaya magharibi kwa jambo hilo, iliyotokana na hoja za kiuchumi, hadi ilipofikia mwaka 1517 ndipo mhubiri aliyefahamika kama Johann Tetzel, mtawa wa shirika la Kidominikani alipoanza kuhubiri kuhusu malipizi hayo katika Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mainz na Magdeburg nchini Ujerumani mwaka 1516.

Tayari alikuwa na uzoefu mkubwa katika kupigia chapuo la kuuzwa kwa malipizi kama ondoleo la dhambi kwenye kiti cha kitubio kati ya miaka 1503 hadi 1510 katika miji mingine ya Ujerumani. Wengi waliona ni matumizi mabaya ya sakramenti ya Kitubio. Hii ndio hasa iliamsha hasira za Martin Luther, akiwa ameyasikia mahubiri hayo ya Tetzel akiwa Juterbog, karibu na mji wake wa Wittenberg mwaka 1517. Johann Tetzel hakuwa mtaalamu wa kutosha kuhusu Taalimungu (Theology) kama ilivyokuwa kwa Dr Martin Luther.

Katika kujibu mahubiri hayo, ndipo padre Martin Luther alipopinga vikali kwa kuandika hoja 95 zinazojulikana sana kama hoja 95 (95 Theses). Hoja hizo zilibandikwa mlangoni mwa kanisa alilokuwa anahudumu, huko Wittenberg Ujerumani tarehe 31 October 1517 akishutumu na kupinga mtindo mpya wa kuuza malipizi. Watu wengi walisoma na kukukubaliana na hoja zake na hoja hizo zilisambaa kwa kasi nchini Ujerumani kama moto wa kifuu. Mwaka 1518 hoja za Luther zilimfikia Papa Leo mjini Roma, na papa alitoa amri kwa mkuu wa shirika la Waagustino, ambako Martin alikuwa ndilo shirika lake, kumnyamazisha. Baada ya kushindikana kupitia mkuu wake wa shirika, Papa alifanya kile kilichoshindwa pia kumnyamazisha kupitia kwa Frederick wa Saxony, huyu alikwa Mfalme wakati huo.

Hatimaye ilipofika June 15 1518, papa alitoa amri kwenye (Exsurge Domini) kwa Martin kuzikana hadharani, akiorodhesha sentensi 41 alizoonyesha kuwa Martin alikuwa anapindisha mafundisho ya kanisa na utaratibu wake, hivyo akimtaka ndani ya siku sitini kukana au akabiliane na adhabu ya kutengwa na kanisa.

Hofu ya papa ilikuwa hoja hizo zingewapotosha waamini. Martin Luther kwa wakati huo tayari alikwisha pata uungwaji mkono sana na watu maarufu nchini Ujerumani, alimjia juu papa na kugoma kukana hoja zake. Licha ya mikutano kadhaa kufanyika za kumtisha Martin azifute hoja hizo lakini alishikilia msimamo wake hadi mwisho. "Sumu" ya Luther ilianza kuenea nje ya Ujerumani, na kupata wafuasi wengi Ulaya Magharibi. Papa Leo X hakuwa na namna nyingine baada ya hapo zaidi ya kutoa amri ya kutengwa kwake Januari 3, 1521.

Papa Leo X kwa mtazamo wa wasomi wengi wa mambo ya kanisa, hakujua na hakupima madhara ya hoja za Martin namna zilivyoenea na kuleta mabadiliko makubwa nchini Ujerumani na duniani kote, kitu ambacho kilikuja kuonekana baadae. Yeye aliamini tu kuwa Martin alikuwa ni sehemu tu ya wapinga kanisa kama wengine waliokwisha tangulia, akijua kuwa kanisa la ukweli litapata ushindi tu. Papa Leo X alikufa ghafla Desemba 1521, akiacha mtanziko mkubwa wa kisiasa na kidini nchini Italia na kuenea kwa kasi Ulaya Magharibi.

Mabadiliko katika kanisa
Baada ya vuguvugu la mabadiliko kushika kasi, kanisa lilifanya mabadiliko kwenye yale yaliyoandikwa na Martin. Hadi leo kanisa linafuata kile kilichopingwa na Martin kutokuuza misamaha ya dhambi kama ilivyotokea nyakati hizo.

Kuzaliwa na Kifo
Martin Luther alizaliwa November 10, 1483 katika mji wa Eisleben, Ujerumani na na kufariki Februari 18, 1546. Katika kuishi kwake nje ya kanisa, alifanya kazi kubwa ya kutafsiri biblia katika lugha ya Kijerumani kutoka Kiebrania, Kigiriki na Kilatini kutokana na umahiri wake wa kuzijua vizuri lugha hizo, ingawa yeye hakuwa wa kwanza kufanya hivyo maana alitanguliwa na Mtakatifi Jerome.

Utofauti ni kuwa wakati wa kutafsiri na namna ya kutumia Biblia. Kwa kutumia wasaidizi kwenye kazi hii, alimaliza Agano zote mbili mwaka 1534. Lakini Martin alileta mapinduzi mapya kwenye kulimiliki neno la Mungu kwani ndiye aliyeleta mawazo mapya kuwa biblia imilikiwe kokote na watu wote iwe kanisani, shuleni au nyumbani. Sio suala la makuhani tu.
 
All road leads to Rome..
Kwa maneno na matendo yao yote ni kama waRome.. Soon they will back to their roots.
 
Kuna faida gani labda Kuamua Kumtenga Mtu kisha nae anaenda Kuanzisha Kitu kingine ambacho kinakuja Kufanikiwa Kiimani kwa Wengine pia?
 
Sahau huo ujinga wako
Badala yake nyie ndiyo mnawafuata protestant
Suala la kuoa mtakubalii tuu
Naona mnavoteseka na nyige zenu
Hadi mna.
Naona umepanic kama vile masirahi yako yameguswa..
Mengi manayofanya mme CTRL +V kutoka RC halafu mkaongezea mambo kidogo..ndio maana hadi kuimba mnaimba kama sisi..Ubarikiwa kama sisi.

RC ina miaka 2000+ sasa na itaendelea kuwepo milele na milele. Hoja ya kuoa au kutokuoa si hoja maana ni taratibu binafsi
 
Kuna faida gani labda Kuamua Kumtenga Mtu kisha nae anaenda Kuanzisha Kitu kingine ambacho kinakuja Kufanikiwa Kiimani kwa Wengine pia?
Ndiyo uone kuna watu wana wivu,chuki, unafiki kiburi
Ni kama mtu anakufukuza kazi halafu unapata kazi nzur zaid ya ile aliyokuajiri

Huwa nasema binadamu ni kiumbe mnafiki Sana
 
Naona umepanic kama vile masirahi yako yameguswa..
Mengi manayofanya mme CTRL +V kutoka RC halafu mkaongezea mambo kidogo..ndio maana hadi kuimba mnaimba kama sisi..Ubarikiwa kama sisi.

RC ina miaka 2000+ sasa na itaendelea kuwepo milele na milele. Hoja ya kuoa au kutokuoa si hoja maana ni taratibu binafsi
Na wewe ni wale wale tuu
Siku ukiacha unafiki utaelewa
 
Na wewe ni wale wale tuu
Siku ukiacha unafiki utaelewa
Bwana wax Jesuist tunasema Cum cruce et gradio.. kwa upanga na msalaba katoliki itaendelea kuwepo. Mpende msipende mtarudi kundini tu..
 
Hizo hoja 95 za Martin zilikua zipi!?
Na zile 41 zilizopingwa na Kanisa ni zipi!?
 
Back
Top Bottom