Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania,kwanini bado Tanzania ni maskini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania,kwanini bado Tanzania ni maskini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NEW NOEL, May 21, 2011.

 1. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Leo katika chuo kikuu cha ushirika na biashara moshi(muccobs),kuna kongamano la kujadili tatizo la umaskini katika taifa letu.
  Kuna watoa mada mbalimbali,akiwemo samwel sitta,waziri wa ushirikiano wa a.mashariki,harrison mwakyembe naibu waziri wa miundombinu. Bila kuwasahau prof chambo mkuu wa chuo kikuu cha muccobs mstaafu. Na mwl mangasini.

  Samwel sitta ameanza kwa kuizungumzia historia ya taifa letu:
  Akasema yeye ni mwanasiasa anayefikiria kwa kichwa na sio tumbo. Na anakumbuka aliwahi kuwa mshindi wa shindano la kuandika insha akiwa kidato cha nne miaka hiyo kabla ya uhuru ''how tanganyika independence will look like''. Pia mnamo mwaka 1999 kabla nyerere ajafariki anakumbuka nyerere alimwambia neno moja''mkiichezea misingi ya nchi,misingi hiyo itawabomoa''
  pia amesema anatamani kuona tanzania inasonga mbele kutoka hapa ilipo.kufikia 2025 taifa la tz liwe ni taifa la kati kutoka pato la mwaka la mwananchi wa kawaida kutoka $560 hadi $3500


  pia mwl mangasini amezungumzia tatizo la umaskini wa tz kwa kutoa takwimu mbalimbali ikiwemo:
  -12.1% wanapata umeme tz
  -95.8% ya watu wanatumia vinyesi,mkaa na kuni
  -34% ya watu wanatumia vyoo vya kisasa wengine baharini na porini
  -2002 mwanza iliongoza kwa magonjwa ya mlipuko
  -kuibuka kwa dawa kama za semunge ishara za za huduma mbovu hospital
  -death rate imeongezeka
  na amesema kwanini tanzania ni maskini:
  1.tz inategemea kilimo cha mvua
  2.ari ya kufanya kazi imepungua
  3.tunategemea takwimu na miongozo kutoka world bank na imf
  4.ukosefu wa shule nzuri,walimu na vifaa vya kufundishia.
  5.watu kutokuwa na nguvu ya maamuzi.

  Na amezungumzia mambo ambayo ambayo tukifanya yatatuondoa katika tatizo la umaskini:
  -watu wenye hari ya kufanya kazi na uzalendo kwa taifa.
  -ardhi
  -uongozi ulio bora
  -katiba safi na bora.
   

  Attached Files:

 2. i411

  i411 JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Yale yale tunaandikaga maripoti mazuri kwenye makaratasi mpaka tunajaza mavitabu……. Utendaji wa kuondoa matatizo hakuna labda kurasa moja mistari miwili. Sasa umasikini tutauondoaje, badala hao wanaojiona wasomi waje na hoja ya kujadili kama kutwa nzima jinsi gani wanaweza kuwawezesha wakulima kutotegemea mvua za masika na kutengeneza mikondo ya maji kutoka ziwa viktoria, tanganyika na nyasa tunaongelea vile tunavyojua na kulaumiana. Simavyuo yetu yanatoa mainjinia kila mwaka kwanini wasitujengee mavitus ya maana badala ya kuongelea matatizo na maakili yetu sikuizi yamefunguka lakini tunaishia kuandamana sasa. Wakati umefika sasa watu waongelee masuluhisho siyo matatizo kujaza makaratasi tu na watu wapewe maposho hiyo ni kucopy paste sasa, matatizo yetu yote tunayajua tunataka masuluhishi!
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,065
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu sie wasomi tunapenda sana sifa,sasa kufaulu insha inasaidia nn?mbona hata leo vijana wanafaulu?

  Mie bnafsi naona matatizo yote yanatokana na viongozi wa CCM(Serikali),ni wanafiki,wabnafsi,wasaliti,walaghai,wezi.wabaguzi,n.k.

  Nasema hvi kwa maana ni viongozi chini ya Nyerere(TANU) waliweza kupunguza ujinga 90%,waliweza kujenga viwanda,mashirika mpaka Tanzania ikaheshimika duniani kote n.k,lakini ni viongozi chini ya Mwinyi,Mkapa,JK (CCM) walioharibu na kuwafanya watanzania kufika hapa walipo,huku ujinga ukizidi 40%,viwanda vikfa,mashirika yakiuzwa/kutekelezwa,na heshima ya Tanzania ikishuka ...POOR LEADERS!
   
 4. i411

  i411 JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  hapo kwenye red inamahanisha nyie wasomi wa bongo mnapenda sana kujisifia matatizo ya wabongo na kujaza mikurasa kibao bila masuluhishu. Nadhani hii kitu ya kujisifia matatizo kwa wasomi basi inapatikana Tanzania tuu. Mimi ningekuwa msomi, mwanasiasa ningefikiria masuluhisho siyo malawama……
   
Loading...