Miaka 50 ya Uhuru:Tanzania tufanye nini ili tupige hatua zaidi ya Maendeleo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya Uhuru:Tanzania tufanye nini ili tupige hatua zaidi ya Maendeleo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by saggy, Jun 28, 2011.

 1. s

  saggy Senior Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Salamu sana wanajamii wenzangu,

  Wakati Taifa letu la Tanzania linasherekea miaka 50 ya UHURU wake sisi kama wanajumuia ya wa Tanzania ni vema tukatumia nafasi hii kujadili mambo ya msingi yanayolikabili Taifa letu la Tanzania.
  Wote tunafahamu wazi kwamba ili nchi yoyote iendelee yahitaji mambo makubwa manne(4) ya msingi hayo ni:-

  1.SIASA SAFI
  2.UONGOZI BORA
  3.WATU
  4.ARDHI

  Hebu tuchukue nafasi hii kujadali namna ambavyo mambo hayo niliyotaja hapo juu yametusaidia sisi kama Tanzania kupiga hatua moja zaidi katika maendeleo ya Taifa letu baada ya Nusu Karne nzima tangu Taifa letu lipate Uhuru.
  Katika kufanikisha maendeleo ya Taifa letu,tunahutaji Pato letu la Taifa (GDP) likue kwa kasi zaidi kama ilivyo katika mataifa yanayoibukia kwa sasa kama China,Brazil na mengineyo.Wote tunafahamu kwamba kasi ya kuongezeka kwa shughuli za Uzalishaji mali kutapanua upatikanaji wa Ajira hivyo kuongeza vipato vya wanachi na mapato ya Serikali.
  Uzalishaji wowote ule unahitaji mambo yafuatayo:-

  a.MTAJI
  b.ARDHI
  c.NGUVU KAZI
  Pamoja na hayo yote,Nishati pia ni swala muhimu sana katika kufanikisha uzalishaji,so ukosefu wa Nishati ya uhakika kwa mfano Umeme wa Uhakika ni moja ya changamoto kubwa inayorudisha nyuma maendeleo ya uzalishaji katika Taifa letu wakati tukisherekea Miaka 50 ya Uhuru wa Taifa letu.Kwa mfano mataifa makubwa kama USA na CHINA yanahaha kutafuta Nishati ya uhakika kote Duniani,Marekani na Washirika wake wamevamia Libya ili kupata Mafuta zaidi na China nayo wako katika kukamilisha mradi mkubwa wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kupita Bahari ya Atlantiki kutoka moja ya Taifa mzalishaji mkubwa wa Mafuta Duniani,Nigeria!

  Mambo mengine muhimu ni haya hapa chini katika orodha hii kwa mtizamo wango,napenda kuwakaribisha wanajamii wote kujitokeza kuushibisha mjadala huu ili tuwasaidie wadogo zetu ufahamu na sisi wenyewe wakati tukijiandaa kusherekea mika 50 ya Uhuru wa Tanzania.  1.ELIMU
  2.AFYA
  3.MAJI
  4.MIUNDOMBINU
  5.VIWANDA NA BIASHARA
  6.MALIASILI
  7.ONGEZEKO KUBWA LA WATU
  8.UTAWALA BORA
  9.ARDHI NA MAKAZI
  10.HAKI ZA BINADAMU

  Namwomba mwezeshaji wa Forum hii asihamishe Thread hii muhimu kwa Maendeleo ya Taifa letu.

  Nawasilisha kwenu.
   
 2. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
   
 3. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tutoke ndani ya chupa tufikirie kama taifa na kila mtu atimize wajibu wake basi
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Tuipige chini CCM kwani ndiyo kikwazo cha maendeleo. Imefanya kwa ujana wake sasa imekwisha kuzeeka haitufai na haiwezi kwenda na kasi ya mabadiliko ya kimaendeleo sambamba na dunia ya leo. CCM IMEKUWA KAMA BABU FATAKI, INAJUA HAIPENDWI KWA KUPITWA KWAKE NA WAKATI HIVYO INATUMIA PESA KUJARIBU KUPATANA NA WAKATI. Tuiondoeni CCM ni kikwazo tuendako!!
   
 5. M

  MKWELIMAN Senior Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwanza tuboreshe maisha ya watu waliowepo huko vijijini ikiwa pamoja na afya zao , elimu, miundombinu na utaaluma ambayo itawawezesha maisha yao kama sisi tunavyoishi hapa mikoani maana wao pia wanahaki na wanastahili kuwa na maisha ya kisasa na sio duni kwa ufupi waondowe umaskini kwa ukina kuendeleza eneo zao.................. Mungu atupe viongozi walio na upendo kwa watanzania wote na taifa kwa jumla..... Ameen
   
 6. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Dawa ni moja tu KUING'OA CCM
   
 7. M

  MKWELIMAN Senior Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Tatizo sio chama mkuu ila viongozi ni matatizo sugu hawa walio kuwa kwenye madaraka ndiyo mafisadi wenyewe na wanakula nchi kama nyama choma ya mbuzi!!! Maana chama yoyote ikiletwa kuendesha serikali yetu wasiwe na wazembe kama hawa !!!
   
 8. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uhuru upi tunaozungumzia?

  Ni miaka 50 ya mateso.
   
 9. s

  saggy Senior Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ahsanteni kwa maoni yenu wanajamii at least kidogo na mimi nimepata kitu.Kwakweli Pale kwenye SIASA SAFI sina wasiwasi napo kabisa kwakuwa tulikuwa tunafuata Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na hii ilisisitiza zaidi Kazi,Haki na Usawa mimi nina mashaka na UONGOZI BORA kama kweli upo Tanzania na Hapa ndio maana panatakiwa kuangalia ni nani na ni kina nani wanafaa kutuongoza,Hapa kwa mtizamo wangu mimi naona tuache Itikadi za Vyama kabisaa kwa mfano tuseme kwamba:-

  Hapa kwenye Uongozi bora,tatizo sio Chama bali kwa mtizamo wangu Tatizo ni Mfumo wenyewe wa Uongozi ,it means kwamba hata kama Kiongozi anaweza kuwa Bora kiasi gani but mfumo umefungana sana,ni wa Kihafidhina hapo ndipo tujiulize,ni mfumo upi unaweza kuwapa nafasi Viongozi bora wakafanya kazi yao vizuri?Hapo ndipo tungejiuliza.

  -Je tuna mfumo mzuri wa kulea Vijana kuwaandaa kuwa Viongozi wa Baadaye au tunawatumia kwa maslahi yetu kwa sasa?
  -Je maadili ya Uongozi yapo?na yanazingatiwa?yapo kwenye Katiba yetu?

  Hili la UONGOZI BORA tumakwama kwa miaka ya Mwl Nyerere hapo sina neno,but hizi awamu zilizofuata kidogo tumeteteleka,sasa tufanye nini?
   
 10. s

  saggy Senior Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani JAMII FORUM tunashindwa kujadili mada muhimu kama hizi kwa maendeleo ya Taifa yetu tunajadili maisha binafsi ya watu na majungu?inasikitisha sana na inaniuma sanaaaa1
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tatizo mkuu haya mambo tumeadili sana na tunajua kuwa viongozi ndo wanaotudondosha, tatizo hata tukirudia mara 100 kujadili haya bila serikali kusikia haina maana na ndo maana tunasisitizk kujadili na kutengeneza katoba mpya, kama tatizo ni mfumo ndo huo tunataka tuubadilishe, tatizo magamba bado nitatizo kubwa sababu hata hiyo katiba mpya hawaitaki,
  usione watu hawachangii hapa wamechoka na MAGAMBA ndo maana tunasema wacha MAGAMBA ife!
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  <br>Tatizo mkuu haya mambo tumeadili sana na tunajua kuwa viongozi ndo wanaotudondosha, tatizo hata tukirudia mara 100 kujadili haya bila serikali kusikia haina maana na ndo maana tunasisitizk kujadili na kutengeneza katoba mpya, kama tatizo ni mfumo ndo huo tunataka tuubadilishe, tatizo magamba bado nitatizo kubwa sababu hata hiyo katiba mpya hawaitaki,<br>usione watu hawachangii hapa wamechoka na MAGAMBA&nbsp; ndo maana tunasema wacha MAGAMBA ife!
   
Loading...