Miaka 50 ya UHURU, Serikali za CCM bado hazina huruma kwa wajawazito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya UHURU, Serikali za CCM bado hazina huruma kwa wajawazito

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, Oct 18, 2011.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  JF habarini.
  Ninatoa thread hii kwa uchungu mkubwa, kwani linanigusa mimi mwenyewe kwa namna ya kipekee.
  Serikali ya Tanzania inayoundwa na CCM, miaka 50 sasa, bado haina huruma kwa wanawake wajawazito wanaopata taabu ya kupata huduma za kikunga kwa kuwa hospitali, vituo vya afya na zahanati viko mbali na wanavijiji wengi.

  Mke wangu ni mtumishi wa umma, anayefanyia kazi katika kata ya CHIGUNGA kijiji cha KABUGOZO, wilayani GEITA. Leo imemlazimu wife kutembea zaidi ya kilometa 7 kufuata huduma ya afya katani huku akiwa na ujauzito wa miezi nane. Amefika zahanati hakuna nesi hata mmoja, lakini kamkuta daktari mmoja aliyeajiriwa enzi za mwalimu ndiye anayeendelea kuwahudumia wanaofika na matatizo mbalimbali.

  Hofu yangu ni kwamba, serikali dhalimu ya CCM, inaweza kukatisha ndoto yangu kuwa baba kwa kuwa mke wangu yuko katika hali mbaya na uhakika wa kupata huduma nzuri ni mdogo.

  Ndugu wana JF, tuanze kuhamasishana hapa JF, tuhamie kwenye familia zetu tuwaelimishe ndugu waliondani ya himaya zetu, tuhamie kwa majirani nadhani ujumbe wa kutaka watawala watakaoshusha huduma za kijamii zilizo bora kwa wananchi tutaupata by 2015.

  Ikumbukwe tu kwamba, Barrack Obama, alipata kura za haja kwa kuwa kuna watu walijitolea hadi kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.

  CCM imedhihirisha kushindwa, tusiruhusu iendelee kuweka maisha ya wake zetu rehani na kutukosesha nafasi ya kuwa wazazi.

  Nawasilisha kwa uchungu mzito
   
Loading...