Miaka 50 ya uhuru-serikali ya ccm imeshindwa kutoa huduma bora kwa jamii

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,719
1,440
Kinachonisikitisha ni miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kuna shule kama Shule ya msingi Mvomero-Morogoro haina madawati na madarasa.Kweli watu wakiwa wanaikosoa serikali ya CCM wanafanya makosa/dhambi?.
Inasikitisha kuona shule hazina madawati wala madarasa halafu viongozi wachache wanatembelea magari ya kifahari na misafara mirefu ambapo kiukweli gharama wanazotumia zingetosha kununua madawati na kujenga madarasa.
Ukweli unapotoshwa kuhusu amani.Tunadanganywa kuwa tuna amani wakati watu wanakufa kwa maradhi kutokana na umasikini unaosababishwa na mipango mibovu ya maendeleo-isiyotekelezeka.Huduma za afya duni ili hali watawala wanafuja fedha za walipa kodi bila huruma.
kama watu wachache wanatumia madaraka yao kuwanyonya wengine,kuna amani kweli hapo?.
Kweli ni haki watu wachache wafanye uzembe halafu serikali itumie hela za walipa kodi kufidia hasara hiyo ili hali watu hao wapo wanatembea kifua mbele.Gharama za kuwalipa Dowans bil 111 zingejenga madarasa mangapi na kununua madawati mangapi?.Kuna amani kweli hapo?.
Yapo mengi sana yanasikitisha na kustaabisha.
 
Nimekuwa najiuliza ni Kwa nini CCM IMESHINDWA kuwakomboa watanzania na wimbi la UMASKINI Kwa zaidi ya MIAKA 50?
 
Kwa sababu wanaoshindwa kuwakomboa Watanzania wakibadilisha Shati na kuvaa Kombati mnawadanganya Watanzania kuwa Hao ni Wakombozi,
 
Niambie ni chama gani Africa kiliwaondolea umaskini wananchi wake?,umaskini wako utauondoa wewe mwenyewe kwenye familia yako, wala ukoo wako huwezi kuuondolea umaskini. Sio CCM,CUF wala CHADEMA itakayoondolea wananchi umaskini.Umaskini ni fikra za kuzaliwa nazo, hata marekani na maendeleo iliyonayo ina watu wanaitwa BERGERS(ombaomba) zaidi ya million mbili pamoja na kuitwa Land OF Opportunity, hapo ndo vyama vya upinzani vinapolaghai wananchi,kinachotakiwa ni miundo mbinu ya kueleweka,barabara,hospitali,maji, umeme nk na ndo anachopigania Magufuli. Wananchi hawataki kusikia habari za CCM,CDM wala CUF wanachotaka ni maendeleo. Sasa nyie jikite kwenye uvyama uvyama msahau kuwasikiliza wananchi majimboni kwenu muone mtakavyopoteza majimbo karibu na yote 2020.
 
Back
Top Bottom