Miaka 50 ya uhuru-serikali ya ccm imeshindwa kutoa huduma bora kwa jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya uhuru-serikali ya ccm imeshindwa kutoa huduma bora kwa jamii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwakalinga Y. R, Oct 3, 2011.

 1. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kinachonisikitisha ni miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kuna shule kama Shule ya msingi Mvomero-Morogoro haina madawati na madarasa.Kweli watu wakiwa wanaikosoa serikali ya CCM wanafanya makosa/dhambi?.
  Inasikitisha kuona shule hazina madawati wala madarasa halafu viongozi wachache wanatembelea magari ya kifahari na misafara mirefu ambapo kiukweli gharama wanazotumia zingetosha kununua madawati na kujenga madarasa.
  Ukweli unapotoshwa kuhusu amani.Tunadanganywa kuwa tuna amani wakati watu wanakufa kwa maradhi kutokana na umasikini unaosababishwa na mipango mibovu ya maendeleo-isiyotekelezeka.Huduma za afya duni ili hali watawala wanafuja fedha za walipa kodi bila huruma.
  kama watu wachache wanatumia madaraka yao kuwanyonya wengine,kuna amani kweli hapo?.
  Kweli ni haki watu wachache wafanye uzembe halafu serikali itumie hela za walipa kodi kufidia hasara hiyo ili hali watu hao wapo wanatembea kifua mbele.Gharama za kuwalipa Dowans bil 111 zingejenga madarasa mangapi na kununua madawati mangapi?.Kuna amani kweli hapo?.
  Yapo mengi sana yanasikitisha na kustaabisha.
   
Loading...