Miaka 50 ya Uhuru: abiria akutwa na bastola ndani ya ndege ya Emirates! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya Uhuru: abiria akutwa na bastola ndani ya ndege ya Emirates!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumba-Wanga, Dec 9, 2011.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wana JF;

  Hongereni kwa miaka 50 ya uhuru! Ni kitu cha kujivunia sana, lakini, jamani, pamoja na mazuri yote (sina hakika kama yanazidia mabaya) shame on us Tanzanias!!!! How is this possible???

  Bofya hapo chini uksome kituko cha Karne!!!!

  Abiria akutwa na bastola kwenye ndege
   
 2. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Abiria akutwa na bastola kwenye ndege [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 08 December 2011 21:01 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Ramadhan Semtawa
  KATIKA hali ambayo si ya kawaida, Zainab Kaswaka aliyekuwa anasafiri kwa ndege kutoka jijini Dar es Salaam kwenda London, amekutwa na bastola kwenye ndege ya Shirika la Emirates na kuzua tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Viwanja vya Ndege nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei, zimeeleza kuwa tukio hilo lilisababisha ndege hiyo iliyokuwa tayari imeanza kuruka, kutua tena kwa ajili ya kuitoa bastola hiyo na kuikabidhi kwa walinzi uwanjani hapo kabla ya kuendelea na safari.

  Kwa mujibu wa habari hizo, tukio hilo ambalo limekuwa likiumiza vichwa vigogo wa usalama wa viwanja vya ndege nchini, limetokea Desemba 2 saa 11:45 na tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Insepekta Jenerali (IGP) Said Mwema ametaka maelezo ya tukio hilo.

  Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwananchi umebaini kwamba, Kaswaka alipanda na kukutwa na bastola hiyo aina ya Bareta yenye namba BAA197059 ikiwa na risasi nne na magazini moja ambayo alilazimika kuikabidhi kwa wahudumu wa ndege hiyo.

  Abiria huyo alikuwa na hati ya kusafiria namba AB00828, alipita na kukaguliwa katika mashine mbili za usalama (X-ray machines), lakini walinzi hao ambao wanatajwa walichukuliwa kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga Ukonga (Air wing), hawakuweza kubaini kama katika mizigo ya abiria huyo kulikuwa na pochi yenye bastola hiyo.

  Sehemu ya uchunguzi huo ilibaini zaidi kwamba, wakati abiria huyo akiwa tayari amekwishapanda ndege hiyo, ndipo mumewe alimwarifu kwa simu kuwa ndani ya mkoba wake mdogo uliokuwa katika begi kubwa, mlikuwa na bastola.

  Mwananchi ilibaini zaidi kwamba baada ya kuarifiwa bastola hiyo ingemsumbua mbele ya safari, abiria huyo aliangalia mfuko huo na kuikuta, kisha kuikabidhi kwa mmoja wa wahudumu wa ndege ambaye naye aliikabdihi kwa rubani.

  "Baada ya rubani kukabidhiwa bastola hiyo, alifanya mawasiliano na mamlaka za usalama uwanjani kisha akageuza ndege hiyo hadi uwanjani hapo, takribani dakika kumi tangu ilipoanza kuruka kuelekea nchini Dubai,"alisema.

  Hata hivyo, uchunguzi huo ulibaini kuwa badala ya abiria huyo kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo maalumu, aliruhusiwa kuendelea na safari hiyo na sasa anasubiriwa arejee nchini ndipo atoe maelezo.

  Kufuatia tukio hilo la abiria kupenya na bastola, tayari kumeibuka mvutano miongoni mwa mamlaka za usalama uwanjani hapo huku polisi wakianza kutuhumiwa kwa kushindwa kumpekua abiria huyo na kubaini bastola hiyo.

  Lakini, polisi nao wamekuwa wakirusha mpira huo kwa walinzi waliokuwa wakifanya ukaguzi kwa kutumia mashine hizo maalumu za kubaini mizigo isiyostahili kupita na abiria kuingia nayo ndani ya ndege.

  IGP awaka

  Vyanzo vilivyo karibu na IGP Mwema, vimesema tayari mkuu huyo wa jeshi la polisi lenye ametaka maelezo ya tukio hilo kutoka kwa Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo karibu na IGP, tukio hilo limemstua na kuacha maswali mengi kutokana na kwamba kama abiria huyo angekuwa ni mhalifu angeweza kuitumia bastola hiyo kufanya mauaji na hata kujeruhi watu ndani ya ndege.Hata hivyo, IGP Mwema alilishauri gazeti hili limwulize msemaji wa jeshi hilo, Adivera Senso ambaye baada ya kuulizwa, naye akataka kamanda Matei.

  Kauli ya kamanda Matei
  Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei alithibitisha tukio hilo na kusema tayari hatua kadhaa zimechukuliwa kwa watu waliokuwa kwenye mashine hizo za ukaguzi.

  Kwa mujibu wa kamanda Matei, wanajeshi wote waliokuwapo zamu kwenye mashine hizo siku ya tukio, wamerejeshwa kambini kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.

  Kamanda Matei alisema, baada ya tukio hilo na ndege kurejea tena uwanjani hapo, vyombo vya ulinzi na usalama vikiwamo polisi na usalama wa taifa, walikutana na kujadili hilo ikiwamo kuangalia picha za abiria walivyokuwa wakipita kwenye mashine hizo.

  Alifafanua kwamba baada ya kuangalia picha hizo, ilibainika tukio zima lilitawaliwa na uzembe kwa walinzi hao kutoka JWTZ ambao walikuwa katika mashine hizo, kwani hawakuwa makini kuona namna abiria huyo alivyokuwa akipita na bastola iliyokuwa katika pochi hiyo.

  Matei ambaye alifafanua tukio zima kwa uwazi, alisema ndege hiyo ilipaa katika njia maalumu iitwayo 'runway five' na kuongeza kwamba hadi sasa tayari kumechukuliwa hatua mbalimbali za maboresho ya udhibiti wa mfumo wa ukaguzi na usalama unaofahamika kama 'quality control.'

  Kwa mujibu wa Kamanda Matei, baada ya tukio hilo, pia wameamua walinzi wanaofanya ukaguzi kwenye mashine hizo, wasiwe na simu za mkononi kwani imebainika kuwa simu ni moja ya sababu zinazowafanya kukosa umakini katika kazi uwajibikaji wao.

  Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu hatma ya abiria huyo, alisema imebainika hakuwa na kosa lolote kwani alipita tu na bastola yake pasipokufahamu wala hakuwa na nia mbaya. Silaha hiyo inashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege.

  Kamanda Matei alieleza kuwa abiria huyo ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam eneo la Jangwani Mtaa wa Swahili na alikuwa akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea London, kwa shughuli zake binafsi.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Usalama wa taifa kazini, thanks God ubovu wao umeanza kujidhihirisha.
   
 4. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni fundisho kubwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi na kwamba tusitambe sana kwamba tunaweza ziba mianya yote kuzuia ugaidi. huyu mama katoa fundisho na kutubumbulusha. inanikumbusha miaka kadhaa iliyopita (1989/90) jamaa uingereza alipenya njia za panya akipita vihunzi vyote vya ulinzi na kuambaa akipanda mabomba ya maji taka na safi hadi kuingia chumba cha Malikia - ilikuwa patashika lakini pia ikawa ni fundisho kwa namna walivyotoa ulinzi kwa mfalme wao.
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tulishauona waliposhindwa kuzuia Twiga Kule KILI airport, itakuwa bastola? This leaves a lot to be desired. Imagine abiria waliokwua kwenye ndege hiyo walituonaje sisi watanzania? At this age, 50 years and we have failed to detect even a gun?

  This is Tanzania: business as usual....
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Shame!!!
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  JWTZ wamelala usingizi mzito baada ya ile vita sasa wanaenda kazini na mazoea na kurudi home wamezoea dezo dezo..kila kitu!!hawajawahi kuwa serious wakiwa nje ya kambi zao maana wamezoea kupokea amri ndio watekeleze sio waanzishe wao...never!
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  They have failled us, they should be punished, demoted and nothing else.
  Who gonna pay for all these costs?
  The Emirates watalipwa na nani, gharama za kutua na kuondoka tena DSM? Imagine, ndege inakwneda Dubai, kule abiria wana connection ya ndege mbali mbali, ..... imagine hiyo chaos iliyokuwepo huko Dubai? Simply because few stupid Tanzanians did not do their jobs....
  Imagine the image of Tanzaniana nje, nchi isiyoweza hata ku search mtu aliyeingia na pistol kwenye ndege...
  Shame on us.....
   
Loading...