Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Status
Not open for further replies.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Wanabodi,

Zanzibar inajiandaa kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 1964 yalioufuta ule uhuru bandia wa mwaka 1963 chini ya serikali ya vibaraka ya Sultani Jamseed. Hizi ni series za mada zangu zenye maswali yasiyo na majibu.

Hii ni Hotuba ya Waziri Mkuu Kibaraka Shamte kwenye Umoja wa Mataifa akiitambulisha rasmi Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hivyo kuuingiza rasmi Zanzibar ndani ya UN kama taifa huru.
Accession of the Sultanate of Zanzibar to the United Nations in 1963
and
The speech given by Prime Minister of the Sultanate of Zanzibar in the United Nations in 1963


Footage hii ni hisani ya mwana jf aitwae Badir

Nchi kuingizwa ndani ya UN na kupata kiti cha UN is a process inafuata taratibu fulani.

Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuunda Tanzania, kuna utaratibu pia uliopaswa kufanywa na SMZ na Jamhuri ya Tanganyika kwenda UN ili kuviunganisha viti vya iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika ili kuvifuta rasmi na badala yake kuwekwa kiti kipya cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nani anajua ni nini kilichofanyika hapa hadi kukifuta kiti cha Zanzibar kule UN?!.

Utaratibu ni kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kumuandikia rasmi Katibu Mkuu wa UN Note Verbale, kumtaarifu kuhusu muungano na kueleza lile taifa huru lililojiunga hivi karibuni, ceased to exist anymore hivyo kiti chake kifutwe! na kupewa taifa jipya laTaifa la Zanzibar halipo tena!. Hili halikufanyika!.

Na Tanganyika pia ilipaswa kumuandikia Katibu Mkuu wa UN, Note Verbale kumtaarifu kuwa lile taifa la Tanganyika has seased to exist kufuatia muungano na Zanzibar hivyo kiti chake kifutwe na kukabidhiwa Taifa jipya la JMT. Hili pia halikufanyika!.

Kwa barua hizo mbili, viti vya Tanganyika na Zanzibar ndipo vingefutwa rasmi, na kisha kupelekwa Note Verbale ya 3 toka serikali ya JMT ikilitambulisha Taifa jipya la Tanzania na kupewa kiti cha taifa jipya!.

Kilichotokea ni kule UN ilipelekwa Note Verbale moja tuu toka serikali ya JMT kumtaarifu Katibu Mkuu kuwa Tanganyika na Zanzibar zimeungana kuunda JMT, hivyo kiti cha iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kile cha iliyokuwa Tanzanyika, sasa vitakaliwa na nchi moja ya Tanzania wakati utaratibu wa submition ya union documentations zikiwemo zile Articles of Union ungefuatia, kitu ambacho hakikutekelezwa mpaka leo!.

Jee kiti halali cha nchi moja huru ndani ya UN kinawezwa kufutwa kirahisi rahisi hivyo with just a Note Verbale kutoka taifa jingine?!.

Mfano ikitokea Tanzania tukaungana na Kenya, hivi kweli mwenye jukumu la kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa UN ni Kenya tuu kumtaarifu kuwa tumeungana na Tanzania hivyo kuanzia sasa kiti cha Tanzania kifutwe?.

Nikiwa mwandishi nilibahatika kuutembelea ubalozi wetu wa UN pale NY, nikapokelewa na shemeji yetu (Mke wa mwana jf mwenzetu ndie alikuwa receptionist wakati huo), nikapeleka maswali yangu haya kwa balozi we enzi hiyo, sikupata majibu.

Pia nilitembelea jengo la UN ili angalau kuziona zile docu za muungano, kilichopo kule ni ile Note Verbale tuu, nothing more, nothing less!.

Wenye majibu naombeni msaada wenu!.

Pasco.
Update 1.
Note Verbale ilitoka kwa Balozi wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa, Chief Arasto Mang'enya na kuitambulisha United Republic of Tanganyika and Zanzibar, wakati huo jina la Tanzania halijaanza. Mwezi June aliteuliwa rasmi kuwa balozi wa kudumu wa Jamuhuri ya Tanganyika na Zanzibar, na mwezi September ndipo akawasilisha rasmi hati zake za utambulisho. Jina la Tanzania lilikuja kupelekwa Mwezi Septemba.

Game ilichezwa hivi
MERGER OF MEMBER STATES
29. During the period under review the issue of the merger of Member States arose in the United Nations in connexion with the formation of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, later called the United Republic of Tanzania. Tanganyika and Zanzibar, which had been admitted which in the United Nations since 14 December 1961 and 16 December 1963 respectively, informed the Secretary-General by a note verbale dated 6 May 1964 of the following:

" . . . the Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar were united as one Sovereign State on 26 April 1964, under the name of the United Republic of Tanganyika and Zanzi- bar and under the presidency of Mwalimu Julius K. Nyerere. A copy of the said Articles of Union is enclosed herewith.
"The Secretary-General is asked to note that the United Republic of Tanganyika and Zanzibar declares that it is now a single Member of the United Nations bound by the provisions of the Charter, and that all international treaties and agreements in force between the Republic of Tanganyika or the People's Republic of Zanzibar and other States or international organizations will, to the extent that their implementation is con- sistent with the constitutional position established by the Articles of Union, remain in force within the regional limits prescribed on their conclusion and in accordance with the principles of interna- tional law."
On 14 M a y , the Secretary-General, at the request of the Government of the United Republic of Tan- ganyika and Zanzibar, communicated the note to all States Members of the United Nations, to the principal organs of the United Nations and to the subsiding organs of the United Nations to which Tanganyika or Zanzibar had been appointed or admitted, and to the specialized agencies and to the International Atomic Energy Agency, by a note verbale which included the following statement:
"The Secretary-General is taking action, within the limits of his administrative responsibilities, to give effect to the declaration in the attached note that the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, is now a single Member of the United Na- tions bound by the provisions of the Charter. This action is undertaken without prejudice to and pending such action as other organs of the United Nations may take on the basis of the notification of the establishment of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar."
Source ni UN.
NB. Kwa vile nilipokwenda UN, nilikwenda kwa mengine, hili nikafanya kuliulizia tuu, kuna uwezekano kuwa ni kweli ile NV ilikwenda na Mkataba wa muungano kama ilivyosema!, ila pia inawezekana kabisa kilichokwenda ni hiyo NV peke yake bila mkataba wowote, hivyo Tanzania japo ni nchi halali, imekalia kiti chake cha UN mpaka kesho with a lie!.

Kwa vile mwakani nitakuwa na safari ya huko, this time nitafanya juhudi za makusudi kupita tena Ubalozi wetu pale UN na kutembelea tena Maktaba ya UN kuziona hizo "Hati za Muungano!"

Mjadala umehitimishwa rasmi na facts zote.

Asanteni sana!.

Pasco.


 
Last edited by a moderator:

Abdillahjr

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
694
0
Muungano huu una abracadabra kwa wingi tu,Zanzibar wanataka uhuru wao wakati Tanganyika haipo ila Tanzania ndio haitaki??

Ni yapi manufaa ya muungano kwa wananchi wa bara hadi watawala wautetee??!! Kwangu majibu yao ni abracadabra tupu!!
 

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,750
2,000
kweli ni mapinduzi.....lakini tofauti ya haya na mapinduzi mengine duniani haya yalii pindua nchi na kuifunika...na leo znz si nchi maana walopindua walikabidhi nchi 'yao' kwa Tanzganyika.
nchi ilipinduliwa kila kitu kuanzia
elimu
afya
ustaarabu
mila na utamaduni..( school wakiimbishwa kwaya za kanisani badala ya wanafunzi kusoma kasida)
nk nk
 

vngenge

JF-Expert Member
Apr 19, 2011
524
250
Akili ndogo inatafuta kujitenga akili kubwa inatafuta kuungana. Akili ndogo inafikiria udogo na madogo akili kubwa inafikiria ukubwa na makubwa. TUPIME WENYEWE TUPO UPANDE GANI
 

Khawarizm

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
205
0
Pasco

Nijuze kiduchu ukibaraka wa Shamte ni upi.

Na kwa nini mapinduzi haya unayaita matukufu.

Kamaa kuuwa Kimbari ni Utukufu wake then Kina Kagame na Wenzake kule Rwanda, Khmer Rouge ma Hitler walikuwa Watakatifu wanafaa kupewa Sainthood!
Binaadamu mwenye akili timamu hawezi kuita umwagaji wa damu uliotokea kokote duniani owe Zanzibar, au Burundi.

Utapomwita Shamte kibaraka basi uwaite na Marehem Mzee Karume, Mzee Idris Abdul Wakil na wenziwao waliokuwa katika ile Serikali ya Mseto nao Vibaraka washiriki kwani ile no serikali waliyo afikian kule Lancaster House Conference in London.
 
Last edited by a moderator:

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,309
2,000
Kamaa kuuwa Kimbari ni Utukufu wake then Kina Kagame na Wenzake kule Rwanda, Khmer Rouge ma Hitler walikuwa Watakatifu wanafaa kupewa Sainthood!
Binaadamu mwenye akili timamu hawezi kuita umwagaji wa damu uliotokea kokote duniani owe Zanzibar, au Burundi.

Utapomwita Shamte kibaraka basi uwaite na Marehem Mzee Karume, Mzee Idris Abdul Wakil na wenziwao waliokuwa katika ile Serikali ya Mseto nao Vibaraka washiriki kwani ile no serikali waliyo afikian kule Lancaster House Conference in London.
Mkuu,

Nashukuru kwa mchango wako umenifungua sana kuna vitu nilikuwa nijiuliza sana leo nimefahamu.

Cc; gombesugu, JokaKuu
 
Last edited by a moderator:

Khawarizm

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
205
0
Hawa jamaa fikira zao ziko katika migongo yao. The whole East Afrucan History imekuwa distorted since colonial times. Na hawa wenzetu wanaojiita wasomi wachambuzi wanafanya tafiti zao based om distorted history.
Kuna kitabu cha John Okelo kuhusu Mapinduzi kimenadikwa na nani na hali Okelo hakusoma ni illetrate!! Kimenadikwa na mzungu mmoja hafahamiki!! Hebu watu na wasome kitabu kinachoitwa Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru watawasikia wanamapinduzi halisi waliopnga na walioshiriki.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Pasco

Nijuze kiduchu ukibaraka wa Shamte ni upi.

Na kwa nini mapinduzi haya unayaita matukufu.
Mkuu Ritz, unamjua Shamte au unamsikia tuu?!.

Jee unajuwa kuwa Shamte alikuwa ASP!, unazijua sababu zilizomfanya kujiengua ASP na kuunda ZPPP?!.

Baada ya ASP kushinda uchaguzi wa mwanzo, Shante aliutamani Uwaziri Mkuu, kwa vile Karume ndio alikuwa Kinara wa ASP, Mohamed Shante akijiengua kutoka ASP na kuunda chama cha ZPPP ili kujiunga na wabaya wa ASP kuunda serikali ya mseto

Katika uchaguzi wa Julai 1961, ASP kilipata asilimia 49.9 ya kura zote, ZNP kilipata asilimia 35 na ZPPP asilimia 13.7. Hata hivyo, pamoja na ushindi wa kura ASP, kilishindwa kutamba katika viti vya bunge (LEGCO) kilipopata viti 10, ZNP 10 na ZPPP vitatu.

Uchaguzi huo ambao haukupata mshindi na ilibidi urudiwe Julai, 1963, matokeo ni muungano wa ZNP/ZPPP viti 18 na ASP viti 13. Shamte alishauriwa aunde Serikali ya mseto kati ya ZNP/ZPPP na ASP ili kulinda umoja wa kitaifa, lakini aligoma kata kata kwa kiburi na jeuri ya kuogopa ASP isije kumoutshine!. Kitendo cha Shamte aliyekuwa ASP na kujitoa kwa tamaa ya uiongozi, kisha kukataa kata kata kushirikiana na ASP ambao ndio Waswahili wenzake na badala yake kujiunga na ZNP ambacho ni cha Waarabu, hapa ndipo ukibaraka wake ulipolalia!.

Pasco.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Swali zuri sana Ritz tunasubiri jibu Pasco.
Mkuu Bilal, natumaini umenisoma, na anayeyaita Mapinduzi Matukufu sio mimi, bali wale waliopata utukufu kutokana na mapinduzi hayo, huku waliopinduliwa wakiyalaani na kutaka kuurejesha usultani kwa mlango wa nyuma wa kisingizio cha Zanzibar yenye mamlaka kamili!.
Pasco.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Kwa Taarifa yako ASP katika mkutano wa Lancaster House walipendekeza Constitutional Mornachy copy ya UK na hata katiba na mfumo wa bunge la UK na Waliahidi kuwa watamlinda Sultan na Familia ya Kifalme yote milele!!! Fanya utafiti na ulipinge hilo kama uwongo.
Kwa hiyo unachotaka kusema ni kuwa hata ASP wanamhitaji sultani?. Jitoeni CCM, rudisheni ASP muiteni Sulani arejee awatawale!.
Pasco.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Matukufu maana yake nini?
Kuna watu wanadhani Mwarabu alipokuja Zanzibar, kuna wenyeji aliwakuta!, la hasha!. Hao wamatumbi mnao waona leo, na masalia ya watumwa walikosa soko!. Waarabu walikuwa ndio mabwana na Matumbi ni watwana, Mapinduzi yamewafanya watwana kugeuka ndio mabwana na waliokuwa mabwana wakawa watwana!. Leo hata wingi wa machotara na Mapinduzi kuwezesha mtwana kujitwalia binti wa Kiarabu na kumfanya mke!. Wabwana wa Mkongwe walichinjwa kwa jambia, leo Alhamdidulahi, watwana nao wanaishi ghorofani!, zamani wali wakiishi Kibanda Maiti, Mchambawima, Mchafukoge etc. Huu sii utukufu wa mapinduzi?!.

Pamoja na harakati zote, muungano utadumu, Mapinduzi Daima!.
Pasco
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Ulitaka nchi hizo zitume hiyo taarifa kabla au baada ya Muungano?
Muungano ni kama ndoa, na kwa upande wa UN ni kama ndoa ya ughaibuni. Baada ya kumtwaa binti wa watu huko ughaibuni, kuwa mkeo, ni binti ndiye kwanza hutoa taarifa kwao kuwa amepata mchumba na wanataka kuleta posa, kisha ndipo mshenga hutumwa na binti kuulizwa kama amekubali ndipo posa hupokelewa na mahari kupangwa na ndoa kufungwa, na sio muoaji kutoa taarifa kwa wazazi wa binti kuwa yeye ndie kamuoa binti yao!.

Hivyo tulipoungana, SMZ ndio ilipaswa ipeleke NV kule UN kuisurender seat yake kwa Tanganyika baada ya muungano!, kilichofanyika ni kwa Tanganyika kupeleka NV kule UN kuwa imeungana na Zanzibar hivyo Jamhuri wa Watu wa Zanzibar has ceased to exist na imebadili jina kutoka Tanganyika hadi Tanzania!.

Kama ilivyokuwa kwenye issue ya ratification, something was wrong, the same kwenye kufuta seat ya Zanzibar kule UN, something was wrong!. Its very unfortunately UN iko busy sana, bado sijaelewa mpaka leo, nchi imefutwa futwa vipi bila any international instruments kuwa deposited kule UN kuonyesha muungano!. Kiti kimefutwa kwa NV tuu!. Its very unusual ila hivyo ndivyo hali ilivyo till todate!.
Next year nafanya tena visit ya UN kwa mengine, ila hili pia litakuwa ni moja ya agenda zangu!. Nimeishamaliza ground work huku nyumbani, hizo articles of union, are no where to be seen!, sababu naijua!. Kumbe hata UN hazipo!.
Pasco.
Pasco
 

gombesugu

JF-Expert Member
Apr 4, 2013
1,485
0
Mkuu,

Nashukuru kwa mchango wako umenifungua sana kuna vitu nilikuwa nijiuliza sana leo nimefahamu.

Cc; gombesugu, JokaKuu


Mkuu Ritz,

Shukran na nimekusoma!

Naona huyo ajiitae Pasco anapotosha majambo mangi mno!...namstahi mno,lakini yanishinda kumstahamilia kwa jinsi ya mtiririko/pattern ya mazungumzo yake,naona pana mangi labda hayajui kiundani au ndo yale yale matatizo ya jamaa wengi wajiitao ndo "wasomi" wa huko Tanzania Bara kuendeleza ule upotoshaji wa historia na kuzidisha chuki na ubaguzi wa rangi huku wakiichafua Zanzibar na Wazanzibary!? Dah!

Sifahamu hii ni kwa lengo lipi au manufaa yanani!?

Naona Pasco anajitahidi kujifanza ati anaijua Zanzibar/Wazanzibary kiundani!? Teeh! Teeh! Teeh!

Haya yoote ajaribuyo kuyazungumza yeye leo humu-JF...tayari sisi tushayajadili/tunayajadili kila kukicha tena kwa undani mno!?

Tajitahidi nirejee tena hapa jamvini pindi nipatapo wasaa japo kiduchu!?...wajua Shariff kwa hivi sasa nimo safarini kiduchu na fursa yangu ni mughali mno!

Tuko pamoja.

Ahsanta.
 

gombesugu

JF-Expert Member
Apr 4, 2013
1,485
0
Hawa jamaa fikira zao ziko katika migongo yao. The whole East Afrucan History imekuwa distorted since colonial times. Na hawa wenzetu wanaojiita wasomi wachambuzi wanafanya tafiti zao based om distorted history.
Kuna kitabu cha John Okelo kuhusu Mapinduzi kimenadikwa na nani na hali Okelo hakusoma ni illetrate!! Kimenadikwa na mzungu mmoja hafahamiki!! Hebu watu na wasome kitabu kinachoitwa Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru watawasikia wanamapinduzi halisi waliopnga na walioshiriki.


Khawarizm,

Mkuu nimekusoma kwa utuvu ulo mwingi na nimekufahamu takriban yoote ulonena tena kiundani mno!

Huyo Mkuu Pasco...japo mimi ni mgeni mno humu-JF lakini namfahamu mno na kuheshimu posts/threads zake kadhaa na baadhi ya maoni yake mangi....lakini kwa thread hii lazim nikiri yakuwa amenistaajabisha mno,maana ameonyesha udhaifu wake khasa ukizingatia yakuwa Topic hii ni pana mno,na yataka broader perspective not just merely triangular explanation/s!

Naona ghafula ati ataka kutuaminisha yakuwa Zanzibar palikua na Watumwa/Utumwa!? Duh!

Pasco anafahamu uzuri nini maana ya utumwa...achukulie pia mfano wa ile Slavery ya wale ndugu zetu Afrikan Amerikans!

Pana

Je huo Utumwa na Utwana ulokuwapo hiyo Unguja/Zanzibar...tunamuomba na kumsihi yeye Pasco aje hapa jamvini atutajie majina/orodha ya koo/families zozote azijuazo yeye za Wazanzibary wowote wale awajuao yeye au kwenye historia ambao waliwahi kuwa Watumwa,watwana au Vijakazi kwenye hiyo Zanzibar/Unguja!?

Au labda pia Mkuu Pasco labda hafahamu yakuwa "watu weusi" wameanza kuoa katika koo/families mbalimbali za hao awaitao yeye ati ndo "Mabwana" centuries nyingi tu zilizopita!?

Hapo sizungumzii weusi yaani kuolewa tu,hasha nazungumzia Wazanzibary waliokua na asili za Kiafrika/Waafrika-Wanaume...nao pia walikuwa wakioa mbona saana tu kwenye tena families/koo zilizokua kubwa/Aristocracy za Wazanzibary waliokua na asili ya Persia,Greek,Arab,Indian Sub Continent na makabila mangine kadhaa!

Napata shaka kiduchu yakuwa huyo Pasco,asijekua achanganya baina ya ile Class Struggle ilokuwapo pale Unguja/Zanzibar wakti ule na ile Slave Market na impact yake kwenye society ya Wazanzibary!?

Niwia radhi Khawarizm,wajua nimetingwa mno na mashughuli lakini nina hakika Mkuu Pasco kwa ustaarabu alonao atatusoma hapa japo kiduchu,nami tajitahidi kipata fursa kurejea tena hapa jamvini!

Ahsanta.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom